
Watendaji wa Kata Handeni Mji waaswa kusimamia mkataba wa lishe kwa ufanisi
Na OR TAMISEMI Handeni,Tanga
MKUU wa Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, Mhe. Salum Nyamwese amewataka watendaji wa kata kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa mkataba wa lishe katika maeneo yao ili kujenga jamii yenye afya bora.
Akifungua kikao cha tathmini ya mkataba huo kwa robo ya nne mwaka wa fedha 2024/25 kwa Halmashauri ya Mji Handeni, kilichofanyika Agosti 28, 2025, Mhe. Nyamwese amesema jamii isipozingatia masuala ya lishe hujikuta ikikumbwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ongezeko la utoro na kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi.
“Hizi afua zilizowekwa lazima tuzizingatie na utekelezaji wake uwe wa kiwango cha juu. Nyie wataalamu na watendaji wa kata, ni wajibu wenu kuhakikisha jambo hili linasimamiwa ipasavyo,” amesema Nyamwese.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni, Maryam Ukwaju, amesema utekelezaji wa mkataba huo umepewa kipaumbele kwa kutenga na kutoa fedha za afua ya lishe, hatua inayolenga kuifanya Halmashauri kutoorodheshwa miongoni mwa zile ambazo hazitekelezi mkataba huo.
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2




