Recent Updates

MJASIRIAMALI MWENYE ULEMAVU AISHUKURU SERIKALI KUMNYANYUA KIUCHUMI
Na. James K. Mwanamyoto OR-TAMISEMI
Mjasiriamali mwenye ulemavu Bw. Mwita Marwa Maki, mkazi wa jiji la Dodoma ameishukuru Serikali kwa kumpatia mkopo wa asilimia 10 wa kiasi cha shilingi milioni 10 ambao ameutumia kuendeleza kazi yake ya ubunifu wa kutengeneza vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu ambavyo vinamuingizia kipato cha kuendesha maisha yake.
Bw. Maki ametoa shukrani zake kwa Serikali, wakati akizungumza na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpanga alipolitembelea banda la Ofisi ya Rais-TAMISEMI kabla ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri Tanzania Bara, uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma kuanzia tarehe 11 hadi 13 julai, 2025.
Bw. Maki amesema kuwa anaishukuru sana Serikali kwa kumpatia mkopo uliomuwezesha kuwa na karakana ndogo katika eneo la Sabasaba jijini Dodoma, ambayo inamuwezesha kutengeneza baiskeli za miguu mitatu, mageti, madirisha na bidhaa zote zinazotokana na ufundi wa chuma.
"Najivunia mafanikio yangu yaliyotokana na msaada wa Serikali, nimepata mafunzo ya ufundi chuma (welding) ya miaka miwili katika Chuo cha watu wenye Ulemavu Yombo jijini Dar es Salaam,” Bw. Maki amesisitiza.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amesema Bw. Mwita Maki ni mfano mzuri wa kuigwa kwa wale wanaodhani ulemavu ni kikwazo cha kujikwamua kiuchumi kwani amedhihirisha namna mtu mwenye ulemavu anavyoweza kuboresha uchumi wake na kuwasaidia walemavu wengine kupata vifaa saidizi kama baiskeli za miguu mitatu.
"Tunapowahimiza wazazi na walezi kuwapeleka shule watoto wenye ulemavu tunataka wapate ujuzi na uwezo wa kuendesha shughuli za kiuchumi kama ambavyo Bw. Mwita Maki ameweza licha ya ulemavu wake,” amesisitiza Dkt. Mpango.
Dkt. Mpango amesema kuwa, Serikali itaendelea kuwaunga mkono wenye ulemavu ambao wameamua kujishughulisha na ujasiriamali ili kujikwamua kiuchumi, hivyo amemtaka Bw. Mwita Maki kuendelea na jitihada zake za kuimarisha uchumi wake ikiwa ni pamoja na kuwasaidia vifaa saidizi watanzania wengine wenye uhitaji maalum.
Awali akiwasilisha mafanikio ya uwekezaji, usimamizi na uratibu wa huduma za afya msingi, Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume amesema Bw. Mwita Maki ni mlemavu aliyenufaika na mkopo wa Asilimia 10 ambao umemuwezesha kuwa na karakana inayotengeneza baiskeli za miguu mitatu ambazo anaziuza kwa kila moja kwa kiasi kisichozidi shilingi milioni 1.5

Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan yapongezwa kuunganisha nguvu na Wadau kuwapigania wasichana nchini
Mwenyekiti wa GPE Duniani, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete ameipongeza Serikali ya Tanzania chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada na hatua ilizofikia katika elimu kwa kuwezesha watoto wengi kuendelea na masomo, kuongeza ufaulu ngazi za sekondari ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu.
Mhe. Kikwete aliyasema hayo Kibasila sekondari Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kumkaribisha Mwanzilishi wa Mfuko wa Malala (Malala Fund) aliyekuja kwa mwaliko wa Kiongozi huyo. Kikwete amemtaja Malala kama shujaa wa kumpigania mtoto wa kike hususani wakati huu wa Sayansi na Teknolojia ambayo haitakiwi kumwacha nyuma mtoto yeyote.
Aidha, alisema Mfuko wa Elimu Duniani GPE umewezesha kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji wa wanafunzi na walimu kwa kujenga miundombinu ya madarasa 2980, vituo vya walimu (TRC) 252, uchapaji wa vitabu 36118000, matundu ya vyoo 7673, nyumba za walimu 64 na shule mpya 18 ambazo zimechangia kuleta mabadiliko nchini
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. QS Kipanga, alisema kuwa maboresho ya mitaala nchini yanalenga kuwahakikishia wanafunzi wote, hususan wasichana na wale wenye mahitaji maalum, mazingira salama na jumuishi ya kujifunzia yanayowasaidia kufanikisha malengo yao ikiwepo matumizi ya teknolojia za kidijitali, ikiwemo Akili Mnemba (AI) na TEHAMA
Vilevile, Mhe. Kipanga alisisitiza kuwa Serikali inaamini kuwa kumuelimisha mtoto wa kike ni njia ya msingi ya kulitendea haki Taifa kwa kulikomboa kiuchumi na kijamii lakini pia hadi sasa wanafunzi wapatao 13,272, wengi wao wakiwa wasichana, wamepata fursa ya pili ya kuendelea na elimu ya sekondari kupitia vituo vya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (IAE).
Bi. Malala Yousafzai, Mwanzilishi wa Mfuko wa Malala (Malala Fund), alisherehekea siku yake ya kuzaliwa tarehe 12 Julai, 2025, Wilayani Kongwa, Tanzania akieleza kufurahishwa na mazingira mazuri yanayoandaliwa kuwawezesha watoto wa Kitanzania kupata elimu. Malala alitoa wito kwa jamii na wadau kuungana kuwasaidia wasichana kutoka katika mazingira na historia tofauti ili wafikie ndoto zao. Alisema zaidi ya wasichana milioni mbili nchini Tanzania wanakosa fursa ya kuendelea na masomo, huku theluthi moja yao wakikatishwa masomo yao na kuolewa mapema. Malala alisisitiza kuwa jambo hili ni hasara kwa Taifa kiuchumi, na kuwa Serikali ikishirikiana na jamii wana uwezo wa kuhakikisha wasichana wote wanahitimu elimu yao.
Joyline Buntu, mwanafunzi wa Kidato cha Pili kutoka Shule ya Sekondari Kibasila, ameishukuru Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Programu ya GPE na Taasisi ya Jakaya Kikwete kwa kuunganisha nguvu pamoja na kuwezesha wanafunzi kama yeye kubaki shuleni, kujifunza kwa ufanisi, pia kujenga miundombinu bora na kufikia ndoto zao bila kukumbana na vikwazo vyovyote.
Malala Yousafzai, Mwanzilishi wa mfuko wa Malala alitembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kujionea moja ya Taasisi ambayo inatekeleza jukumu la kuwainua wasichana waliorudi shule baada ya kuanguka (school dropout) la ‘Msichana Initive’ lakini pia kuunga mkono jitihada za kuwawezesha wasichana nchini ambapo anatarajiwa kuwekeza kiasi cha shilingi Bilioni 8 mwaka 2026.

Dkt. Jakaya Kikwete: Elimu ni Silaha Dhidi ya Changamoto za Dunia
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amesema kuwa elimu ni silaha muhimu ya kupambana na changamoto mbalimbali za dunia ya sasa. Amewahimiza wadau wa elimu kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha kila mtoto, bila kujali mazingira yake, anapata haki yake ya msingi ya kupata elimu.
Akizungumza Dar es Salaam, Julai 13 katika mkutano uliowakutanisha viongozi wa kitaifa, wadau wa elimu na mashirika ya kimataifa, Dkt. Kikwete alisisitiza kuwa licha ya hatua kubwa zilizofikiwa katika kupanua fursa za elimu, bado kuna uhitaji mkubwa wa kusaidia watoto wanaotoka katika mazingira magumu ili waweze kutimiza ndoto zao.
Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, alieleza kuwa hakuna mtoto anayepaswa kuachwa nyuma katika safari ya elimu. Alibainisha kuwa uwekezaji katika elimu ya mtoto wa kike ni msingi wa maendeleo ya kijamii na ya taifa kwa ujumla. Prof. Mkenda alisema msichana anapopewa elimu, jamii nzima inanufaika kiuchumi, kijamii na kiafya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Malala Fund, Lena Alfi, naye alieleza kuwa taasisi hiyo imejipanga kushirikiana kwa karibu na serikali ya Tanzania pamoja na wadau wa ndani kwa lengo la kuleta mageuzi ya kweli katika elimu ya mtoto wa kike.
Aidha, tarehe 14 Julai, 2025, wajumbe wa kimataifa kutoka mashirika hayo wanatarajiwa kutembelea shule mbalimbali jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo imelenga kukagua hali halisi ya miundombinu ya shule na kujionea jinsi ambavyo serikali pamoja na wadau wa elimu wamewekeza katika kuboresha mazingira ya kujifunzia. Pia, ziara hiyo itasaidia kubaini maeneo yanayohitaji uboreshaji wa haraka ili kuwezesha elimu bora kwa wote.
Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF), Malala Fund, na Global Partnership for Education (GPE)

Serikali kujenga hospitali mpya 43 za kisasa
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Festo Dugange amesema serikali itajenga hospitali 43 za halmashauri katika mwaka huu wa fedha ili kuongeza wigo wa utoaji wa huduma za afya nchini
Dkt. Dugange amesema hayo wakati akifunga kikao kazi cha Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri Tanzania Bara, kilichofanyika kwa siku 3 jijini Dodoma kuanzia tarehe 11 hadi 13 julai, 2025.
Mhe. Dugange amesema ujenzi wa hospitali hizo ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati madhubuti na ya kimkakati ya maendeleo kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa.
“Ujenzi wa Hospitali 43 za Halmashauri umelenga kuongeza wigo wa utoaji wa huduma za afya kwa wananchi walioko pembezoni mwa Miji,” Dkt. Dugange amesisitiza.
Sanjari na ujenzi wa hospitali hizo, Dkt. Dugange amesema Serikali itanunua vifaa tiba kwa ajili ya hospitali 142, vituo vya afya 184, pamoja na zahanati 184 ambazo zitakarabatiwa au kujengwa katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.
Amefafanua kuwa, hatua hizi zinadhihirisha dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuwezesha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuimarisha mfumo wa utoaji wa huduma za afya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Aidha amewataka Waganga Wakuu hao wakaimarishe ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi katika vituo vya kutolea huduma za afya vilivyoko kwenye maeneo yao ya usimamizi.
Akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mhe. Dugange, Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI (Afya) Prof. Tumaini Nagu amesema kikao kazi hicho kimetoa fursa ya kujadili na kuweka mikakati ya kuboresha huduma za afya msingi kwa wananchi ili wanufaike na uwekezaji wa trilioni 1.28 uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa kujenga miundombinu ya afya msingi pamoja na ununuzi wa vifaa tiba.

Waganga Wakuu wamemtunukia Rais Tuzo, Mhe. Mpango awapongeza, atoa maelekezo mahususi.
Na John Mapepele
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa tuzo maalum ya kutambua mchango wake kwenye Sekta ya Afya na Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri hii leo.
Tuzo hiyo ameitoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya Waganga hao na kumkabidhi Makamo wa Rais, Mhe. Dkt. Philipo Mpango aliyekuwa mgeni rasmi katika Mkutano huo wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri jijini Dodoma.
Mbali na tuzo hiyo pia Waganga Wakuu wamemtunukia Makamo wa Rais tuzo hiyo pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe Mohamed Mchengerwa na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama.
Mhe. Mpango amewapongeza Waganga Wakuu nchini
kwa kazi wanayofanya ya kuwahudumia wananchi huku akiwataka waendelee
kuimarisha huduma na sekta ya afya kwa ujumla na kuzingatia maadili ya taaluma yao.
Amesisitiza kuwa Serikali itatekeleza mara moja maombi ya kuboresha stahili za wataalam hao kulingana hali halisi ya uchumi.
"Nawaelekeza Mawaziri wa Afya na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na Waziri wa Fedha washughulikie suala la ucheleweshaji wa posho za madaktari na wahudumu wa afya." Amesisitiza Mhe. Mpango
Amesema kwa sasa Serikali inapoelekea kutekeleza mpango wa Bima ya Afya kwa Wote Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatakiwa kuhakikisha zinasimamia vema ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha yanatumika kiadilifu ili kuboresha zaidi utoaji wa huduma.
Pia amewapongeza Wakuu wa Mikoa na Wilaya, pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri/Manispaa na Majiji kwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwemo ile ya afya na vifaa tiba katika Halmashauri/Manispaa/Majiji.
Amesema ili kuimarisha huduma za afya na usimamizi shirikishi, Serikali imenunua na kusambaza magari ya kubeba wagonjwa (ambulance) na mashine za kisasa za kidijiti (Digital X-ray na ultrasound) na kuagiza kuvitunza vifaa hivyo na vingine vitakavyonunuliwa ili viweze kutumika kwa muda mrefu na kutoa huduma kwa watu wengi zaidi.
Akimkaribisha Mhe. Mpango kutoa hotuba, Mhe.Mchengerwa amemshukuru Rais Samia kwa maono yake makubwa na miongozo kwenye sekta ya afya ambayo yameleta mapinduzi makubwa katika kipindi kifupi.
Mhe. Mchengerwa ametumia mkutano huo kutaja mafanikio lukuki yaliyopatikana katika kipindi hiki.
Aidha, amesema mafanikio hayo pia yanatokana na ushirikiano baina ya Wizara yake na Wizara ya Afya.
Katika mkutano huo wadau mbalimbali ya afya pia wametunukiwa vyeti vya kutambua michango yao.
News Archive

MJASIRIAMALI MWENYE ULEMAVU AISHUKURU SERIKALI KUMNYANYUA KIUCHUMI
Na. James K. Mwanamyoto OR-TAMISEMI
Mjasiriamali mwenye ulemavu Bw. Mwita Marwa Maki, mkazi wa jiji la Dodoma ameishukuru Serikali kwa kumpatia mkopo wa asilimia 10 wa kiasi cha shilingi milioni 10 ambao ameutumia kuendeleza kazi yake ya ubunifu wa kutengeneza vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu ambavyo vinamuingizia kipato cha kuendesha maisha yake.
Bw. Maki ametoa shukrani zake kwa Serikali, wakati akizungumza na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpanga alipolitembelea banda la Ofisi ya Rais-TAMISEMI kabla ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri Tanzania Bara, uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma kuanzia tarehe 11 hadi 13 julai, 2025.
Bw. Maki amesema kuwa anaishukuru sana Serikali kwa kumpatia mkopo uliomuwezesha kuwa na karakana ndogo katika eneo la Sabasaba jijini Dodoma, ambayo inamuwezesha kutengeneza baiskeli za miguu mitatu, mageti, madirisha na bidhaa zote zinazotokana na ufundi wa chuma.
"Najivunia mafanikio yangu yaliyotokana na msaada wa Serikali, nimepata mafunzo ya ufundi chuma (welding) ya miaka miwili katika Chuo cha watu wenye Ulemavu Yombo jijini Dar es Salaam,” Bw. Maki amesisitiza.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amesema Bw. Mwita Maki ni mfano mzuri wa kuigwa kwa wale wanaodhani ulemavu ni kikwazo cha kujikwamua kiuchumi kwani amedhihirisha namna mtu mwenye ulemavu anavyoweza kuboresha uchumi wake na kuwasaidia walemavu wengine kupata vifaa saidizi kama baiskeli za miguu mitatu.
"Tunapowahimiza wazazi na walezi kuwapeleka shule watoto wenye ulemavu tunataka wapate ujuzi na uwezo wa kuendesha shughuli za kiuchumi kama ambavyo Bw. Mwita Maki ameweza licha ya ulemavu wake,” amesisitiza Dkt. Mpango.
Dkt. Mpango amesema kuwa, Serikali itaendelea kuwaunga mkono wenye ulemavu ambao wameamua kujishughulisha na ujasiriamali ili kujikwamua kiuchumi, hivyo amemtaka Bw. Mwita Maki kuendelea na jitihada zake za kuimarisha uchumi wake ikiwa ni pamoja na kuwasaidia vifaa saidizi watanzania wengine wenye uhitaji maalum.
Awali akiwasilisha mafanikio ya uwekezaji, usimamizi na uratibu wa huduma za afya msingi, Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume amesema Bw. Mwita Maki ni mlemavu aliyenufaika na mkopo wa Asilimia 10 ambao umemuwezesha kuwa na karakana inayotengeneza baiskeli za miguu mitatu ambazo anaziuza kwa kila moja kwa kiasi kisichozidi shilingi milioni 1.5

Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan yapongezwa kuunganisha nguvu na Wadau kuwapigania wasichana nchini
Mwenyekiti wa GPE Duniani, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete ameipongeza Serikali ya Tanzania chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada na hatua ilizofikia katika elimu kwa kuwezesha watoto wengi kuendelea na masomo, kuongeza ufaulu ngazi za sekondari ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu.
Mhe. Kikwete aliyasema hayo Kibasila sekondari Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kumkaribisha Mwanzilishi wa Mfuko wa Malala (Malala Fund) aliyekuja kwa mwaliko wa Kiongozi huyo. Kikwete amemtaja Malala kama shujaa wa kumpigania mtoto wa kike hususani wakati huu wa Sayansi na Teknolojia ambayo haitakiwi kumwacha nyuma mtoto yeyote.
Aidha, alisema Mfuko wa Elimu Duniani GPE umewezesha kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji wa wanafunzi na walimu kwa kujenga miundombinu ya madarasa 2980, vituo vya walimu (TRC) 252, uchapaji wa vitabu 36118000, matundu ya vyoo 7673, nyumba za walimu 64 na shule mpya 18 ambazo zimechangia kuleta mabadiliko nchini
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. QS Kipanga, alisema kuwa maboresho ya mitaala nchini yanalenga kuwahakikishia wanafunzi wote, hususan wasichana na wale wenye mahitaji maalum, mazingira salama na jumuishi ya kujifunzia yanayowasaidia kufanikisha malengo yao ikiwepo matumizi ya teknolojia za kidijitali, ikiwemo Akili Mnemba (AI) na TEHAMA
Vilevile, Mhe. Kipanga alisisitiza kuwa Serikali inaamini kuwa kumuelimisha mtoto wa kike ni njia ya msingi ya kulitendea haki Taifa kwa kulikomboa kiuchumi na kijamii lakini pia hadi sasa wanafunzi wapatao 13,272, wengi wao wakiwa wasichana, wamepata fursa ya pili ya kuendelea na elimu ya sekondari kupitia vituo vya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (IAE).
Bi. Malala Yousafzai, Mwanzilishi wa Mfuko wa Malala (Malala Fund), alisherehekea siku yake ya kuzaliwa tarehe 12 Julai, 2025, Wilayani Kongwa, Tanzania akieleza kufurahishwa na mazingira mazuri yanayoandaliwa kuwawezesha watoto wa Kitanzania kupata elimu. Malala alitoa wito kwa jamii na wadau kuungana kuwasaidia wasichana kutoka katika mazingira na historia tofauti ili wafikie ndoto zao. Alisema zaidi ya wasichana milioni mbili nchini Tanzania wanakosa fursa ya kuendelea na masomo, huku theluthi moja yao wakikatishwa masomo yao na kuolewa mapema. Malala alisisitiza kuwa jambo hili ni hasara kwa Taifa kiuchumi, na kuwa Serikali ikishirikiana na jamii wana uwezo wa kuhakikisha wasichana wote wanahitimu elimu yao.
Joyline Buntu, mwanafunzi wa Kidato cha Pili kutoka Shule ya Sekondari Kibasila, ameishukuru Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Programu ya GPE na Taasisi ya Jakaya Kikwete kwa kuunganisha nguvu pamoja na kuwezesha wanafunzi kama yeye kubaki shuleni, kujifunza kwa ufanisi, pia kujenga miundombinu bora na kufikia ndoto zao bila kukumbana na vikwazo vyovyote.
Malala Yousafzai, Mwanzilishi wa mfuko wa Malala alitembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kujionea moja ya Taasisi ambayo inatekeleza jukumu la kuwainua wasichana waliorudi shule baada ya kuanguka (school dropout) la ‘Msichana Initive’ lakini pia kuunga mkono jitihada za kuwawezesha wasichana nchini ambapo anatarajiwa kuwekeza kiasi cha shilingi Bilioni 8 mwaka 2026.

Dkt. Jakaya Kikwete: Elimu ni Silaha Dhidi ya Changamoto za Dunia
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amesema kuwa elimu ni silaha muhimu ya kupambana na changamoto mbalimbali za dunia ya sasa. Amewahimiza wadau wa elimu kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha kila mtoto, bila kujali mazingira yake, anapata haki yake ya msingi ya kupata elimu.
Akizungumza Dar es Salaam, Julai 13 katika mkutano uliowakutanisha viongozi wa kitaifa, wadau wa elimu na mashirika ya kimataifa, Dkt. Kikwete alisisitiza kuwa licha ya hatua kubwa zilizofikiwa katika kupanua fursa za elimu, bado kuna uhitaji mkubwa wa kusaidia watoto wanaotoka katika mazingira magumu ili waweze kutimiza ndoto zao.
Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, alieleza kuwa hakuna mtoto anayepaswa kuachwa nyuma katika safari ya elimu. Alibainisha kuwa uwekezaji katika elimu ya mtoto wa kike ni msingi wa maendeleo ya kijamii na ya taifa kwa ujumla. Prof. Mkenda alisema msichana anapopewa elimu, jamii nzima inanufaika kiuchumi, kijamii na kiafya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Malala Fund, Lena Alfi, naye alieleza kuwa taasisi hiyo imejipanga kushirikiana kwa karibu na serikali ya Tanzania pamoja na wadau wa ndani kwa lengo la kuleta mageuzi ya kweli katika elimu ya mtoto wa kike.
Aidha, tarehe 14 Julai, 2025, wajumbe wa kimataifa kutoka mashirika hayo wanatarajiwa kutembelea shule mbalimbali jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo imelenga kukagua hali halisi ya miundombinu ya shule na kujionea jinsi ambavyo serikali pamoja na wadau wa elimu wamewekeza katika kuboresha mazingira ya kujifunzia. Pia, ziara hiyo itasaidia kubaini maeneo yanayohitaji uboreshaji wa haraka ili kuwezesha elimu bora kwa wote.
Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF), Malala Fund, na Global Partnership for Education (GPE)

Serikali kujenga hospitali mpya 43 za kisasa
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Festo Dugange amesema serikali itajenga hospitali 43 za halmashauri katika mwaka huu wa fedha ili kuongeza wigo wa utoaji wa huduma za afya nchini
Dkt. Dugange amesema hayo wakati akifunga kikao kazi cha Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri Tanzania Bara, kilichofanyika kwa siku 3 jijini Dodoma kuanzia tarehe 11 hadi 13 julai, 2025.
Mhe. Dugange amesema ujenzi wa hospitali hizo ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati madhubuti na ya kimkakati ya maendeleo kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa.
“Ujenzi wa Hospitali 43 za Halmashauri umelenga kuongeza wigo wa utoaji wa huduma za afya kwa wananchi walioko pembezoni mwa Miji,” Dkt. Dugange amesisitiza.
Sanjari na ujenzi wa hospitali hizo, Dkt. Dugange amesema Serikali itanunua vifaa tiba kwa ajili ya hospitali 142, vituo vya afya 184, pamoja na zahanati 184 ambazo zitakarabatiwa au kujengwa katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.
Amefafanua kuwa, hatua hizi zinadhihirisha dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuwezesha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuimarisha mfumo wa utoaji wa huduma za afya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Aidha amewataka Waganga Wakuu hao wakaimarishe ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi katika vituo vya kutolea huduma za afya vilivyoko kwenye maeneo yao ya usimamizi.
Akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mhe. Dugange, Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI (Afya) Prof. Tumaini Nagu amesema kikao kazi hicho kimetoa fursa ya kujadili na kuweka mikakati ya kuboresha huduma za afya msingi kwa wananchi ili wanufaike na uwekezaji wa trilioni 1.28 uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa kujenga miundombinu ya afya msingi pamoja na ununuzi wa vifaa tiba.

Waganga Wakuu wamemtunukia Rais Tuzo, Mhe. Mpango awapongeza, atoa maelekezo mahususi.
Na John Mapepele
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa tuzo maalum ya kutambua mchango wake kwenye Sekta ya Afya na Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri hii leo.
Tuzo hiyo ameitoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya Waganga hao na kumkabidhi Makamo wa Rais, Mhe. Dkt. Philipo Mpango aliyekuwa mgeni rasmi katika Mkutano huo wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri jijini Dodoma.
Mbali na tuzo hiyo pia Waganga Wakuu wamemtunukia Makamo wa Rais tuzo hiyo pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe Mohamed Mchengerwa na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama.
Mhe. Mpango amewapongeza Waganga Wakuu nchini
kwa kazi wanayofanya ya kuwahudumia wananchi huku akiwataka waendelee
kuimarisha huduma na sekta ya afya kwa ujumla na kuzingatia maadili ya taaluma yao.
Amesisitiza kuwa Serikali itatekeleza mara moja maombi ya kuboresha stahili za wataalam hao kulingana hali halisi ya uchumi.
"Nawaelekeza Mawaziri wa Afya na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na Waziri wa Fedha washughulikie suala la ucheleweshaji wa posho za madaktari na wahudumu wa afya." Amesisitiza Mhe. Mpango
Amesema kwa sasa Serikali inapoelekea kutekeleza mpango wa Bima ya Afya kwa Wote Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatakiwa kuhakikisha zinasimamia vema ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha yanatumika kiadilifu ili kuboresha zaidi utoaji wa huduma.
Pia amewapongeza Wakuu wa Mikoa na Wilaya, pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri/Manispaa na Majiji kwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwemo ile ya afya na vifaa tiba katika Halmashauri/Manispaa/Majiji.
Amesema ili kuimarisha huduma za afya na usimamizi shirikishi, Serikali imenunua na kusambaza magari ya kubeba wagonjwa (ambulance) na mashine za kisasa za kidijiti (Digital X-ray na ultrasound) na kuagiza kuvitunza vifaa hivyo na vingine vitakavyonunuliwa ili viweze kutumika kwa muda mrefu na kutoa huduma kwa watu wengi zaidi.
Akimkaribisha Mhe. Mpango kutoa hotuba, Mhe.Mchengerwa amemshukuru Rais Samia kwa maono yake makubwa na miongozo kwenye sekta ya afya ambayo yameleta mapinduzi makubwa katika kipindi kifupi.
Mhe. Mchengerwa ametumia mkutano huo kutaja mafanikio lukuki yaliyopatikana katika kipindi hiki.
Aidha, amesema mafanikio hayo pia yanatokana na ushirikiano baina ya Wizara yake na Wizara ya Afya.
Katika mkutano huo wadau mbalimbali ya afya pia wametunukiwa vyeti vya kutambua michango yao.

Prof. Nagu awafunda madaktari, ampongeza Mhe. Rais kwa maboresho makubwa ya afya.
Na John Mapepele
Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia eneo la Afya, Prof. Tumaini Nagu amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kote nchini kuendelea kuzingatia taaluma na kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni kusherekea mafanikio makubwa ambayo yamepatikana katika Sekta ya Afya Msingi yaliyofanywa na Serikali kwa kipindi cha miaka minne cha Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Prof. Nagu ameyasema hayo leo wakati akitoa neno la utangulizi katika Mkutano Mkuu wa Waganga wa Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya kikwete Jijini Dodoma ulioanza leo.
Prof. Nagu amempongeza Mhe Rais kwa maboresho makubwa aliyoyafanya katika kipindi kifupi cha uongozi wake na kuwataka madaktari hao kusimamia vizuri uwekezaji huo ili wananchi wa chini waweze kunufaika na huduma za afya zinazotolewa na Serikali kote nchini.
“Ndugu zangu sote tunatambua uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kwa ajili ya watu wake, hususani katika Sekta ya Afya, kwa ngazi ya Afya ya Msingi ambako ndipo wananchi wengi walipo kwani zaidi ya 95% ya Wananchi ndipo wanapopata huduma za afya” amefafanua, Prof. Nagu.
Aidha, amesema malengo ya mkutano huo ni kujadiliana mambo mbalimbali ikiwepo kuimarisha mfumo wa utoaji wa huduma za afya katika ngazi ya msingi, kuboresha namna za usimamizi wa rasilimali zilizopo vituoni pamoja na miundombinu, kuweka Mikakati ya pamoja kuboresha uratibu katika ngazi ya Taifa, Mikoa na Halmashauri na kutekeleza mipango ya afya.
Naye, Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amesema Waganga wa Wakuu wa Mikoa na Halmashauri ni wadau muhimu sana katika kuandaa Sera mbalimbali za afya kwani wao ndio watekelezaji wakuu wa Sera hizo hivyo maoni yao ni muhimu sana.
Mkutano huo mwenye kauli mbinu ya “Wajibu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri katika kuimarisha ubora wa huduma za afya kuelekea bima ya afya kwa wote” unatarajiwa kumfungulia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hapo kesho.

TANZANIA YAJIFUNZA KUTOA HUDUMA BORA ZA AFYA GANGNAM – KOREA
Na Angela Msimbira, Seoul – Korea Kusini
Timu ya wataalamu kutoka Tanzania imepata fursa ya kujifunza kwa vitendo namna Wilaya ya Gangnam-gu jijini Seoul, Korea Kusini, inavyotoa huduma bora za afya kwa jamii kwa kutumia mifumo ya kisasa ya TEHAMA na mbinu jumuishi za kitabibu.
Ujumbe huo ukijumuisha wataalamu wa TEHAMA, maafisa wa afya na wakurugenzi wa sera, umetembelea Kituo cha Afya ya Jamii cha Gangnam na kujifunza kwa undani namna mfumo wa PHIS (Public Health Information System) unavyotumika kusimamia afya ya jamii kwa ufanisi mkubwa.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kituo cha Afya ya Jamii cha Gangnam, Bw. Lee Jong Cheol, mafanikio ya Gangnam katika sekta ya afya yanatokana na uwekezaji mkubwa katika mifumo ya kidigitali, ushirikiano wa karibu na wananchi, pamoja na utoaji wa huduma zinazolenga kinga kuliko tiba.
“Gangnam sasa ni mfano wa kuigwa duniani. Mataifa mengi, yakiwemo kutoka Afrika kama Tanzania, yanakuja hapa kujifunza mbinu bora za uendeshaji wa huduma za afya,” amesema Bw. Lee.
Wilaya hiyo ina watoa huduma za afya 320 wanaohudumia wakazi 4,040, kupitia vituo vya afya vilivyosambazwa kimkakati kwenye maeneo yote muhimu ya jamii. Aidha, huduma zinazotolewa zinahusisha uchunguzi wa awali wa magonjwa sugu kama kisukari, shinikizo la damu, kifua kikuu, saratani, pamoja na chanjo, elimu ya lishe, na ufuatiliaji wa afya ya wazee na wenye magonjwa ya kudumu.
Bw. Lee amesema mfumo wa PHIS unaoweka taarifa za wagonjwa kwa usalama, hurahisisha uchunguzi wa magonjwa kwa haraka na kutoa ripoti za kiutendaji kwa uwazi, hivyo kusaidia kupanga mikakati ya haraka ya kuzuia magonjwa.
Amesema mfumo wa PHIS unafanana kwa na GoTHoMIS, mfumo wa TEHAMA wa Tanzania unaotumika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya za umma, kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma na ukusanyaji wa taarifa muhimu za kiafya.
“Tumejifunza namna Korea inavyoweka mkazo kwenye huduma za kinga, matumizi ya data, na kliniki za kutembea. Masomo haya ni muhimu kwa maendeleo ya mfumo wetu wa GoTHoMIS,” alisema Dkt. Paul Chaote, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
Ziara hiyo imeleta mwanga mpya katika jitihada za Tanzania kuboresha huduma za afya kupitia matumizi ya teknolojia ya kisasa, usimamizi bora, na mbinu jumuishi za utoaji huduma kwa jamii.

MHE. MCHENGERWA APONGEZA KIBAHA KWA UFAULU, ATOA MAELEKEZO MAHUSUSI
Na John Mapepele
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe, Mohamed Mchengerwa ameupongeza uongozi wa Shule ya Sekondari ya Kibaha kwa kuendelea kuwa na matokeo ya ufaulu mzuri huku akiwataka kutoshuka.
Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo jana wakati alipotembelea shule hiyo na kukagua miundombinu ya madarasa, mabweni,maabara na baadaye kushuhudia wanafunzi waliokuwa wakijiunga na kuzungumza na walimu wa shule hiyo.
Waziri Mchengerwa amesema ameridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na walimu hao kwani katika kipindi chote shule imekuwa miongoni mwa shule zenye matokeo mazuri nchini.
Amesema kutokana na ongezeko la wanafunzi wa kidatu cha tano kwa mwaka huu, walimu wanatakiwa kuweka mikakati madhubuti ili kuhakikisha wanabaki katika kiwango kilekile cha ufaulu.
"Natambua safari hii tumeongeza wanafunzi wa kidato cha tano hakikisheni mnakuja na mikakati ambayo itamaintain kiwango kilekile." Amesisitiza Mhe. Mchengerwa
Kwa mujibu wa Afisa Elimu wa Mkoa wa Pwani Jimmy Daudi Nkwamu ufaulu wa kidatu cha sita mwaka huu ni asilimia 100 ambapo wanafunzi 136 kati ya wanafunzi 140 wamepata daraja la kwanza sawa na asilimia 93.7
Kwa upande wa matokeo ya kidatu cha nne kwa mwaka 2024 amesema wanafunzi wote 92 walipata daraja la kwanza huku kukiwa hakuna daraja la tatu, nne na sifuri.
Aidha, Mhe. Mchengerwa amemuelekeza Afisa Elimu wa Mkoa wa Pwani kuhakikisha anafanya ziara katika wilaya zote za Mkoa huo na kubaini changamoto zote ili kuzipatia ufumbuzi.
"Ninakutaka kutoka ofisini na kwenda kwenye Wilaya zote kuona kama kuna changamoto na kutafuta ufumbuzi mara moja." Amefafanua Waziri Mchengerwa

TANZANIA KOREA KUFANYA MRADI WA UPANUZI WA MFUMO WA GOTHOMIS
Na Angela Msimbira, Seoul, Korea
Serikali ya Korea Kusini kupitia shirika la KOICA imeandaa Mkutano wa Kimataifa kubadilishana uzoefu kwenye kuboresha mifumo ya usimamizi wa huduma za afya kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Mkutano huu umehusisha watalaam kutoka Tanzania na Korea ikiwa ni sehemu ya ushirikiano wa Mradi wa Kupanua matumizi ya Mfumo wa GOTHOMIS unaotelekelezwa Mkoani Dodoma.
Akizungumza kwa niaba ya ujumbe wa Tanzania, Mkurugenzi Msaidizi - (Huduma za Lishe) Bw. Lutifrid Nnally, amesema ushiriki wa Tanzania unalenga kujifunza uzoefu wa Korea kwenye matumizi ya mifumo ya kidijitali katika huduma za afya.
Tanzania inatarajia kutumia uzoefu huo kufanya maboresho ya GOTHOMIS, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa kutumia teknolojia kama telemedicine, akili bandia (AI) na mifumo ya taarifa za kiafya.
Ushiriki huu ni hatua muhimu katika mageuzi ya sekta ya afya, hasa kwa maeneo ya vijijini, ili kuhakikisha huduma bora, za haraka na kwa gharama nafuu zinawafikia wananchi wote

PROF. NAGU AFUNGA MKUTANO WA MWAKA WA HUDUMA ZA AFYA KWA MIKOA NA HALMASHAURI ZOTE TANZANIA BARA.
Na OR- TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI ( Afya) Prof. Tumaini Nagu amefunga rasmi mkutano wa mwaka wa tathimini ya utekelezaji wa huduma za Afya na usafi wa mazingira kwa mikoa na halmashauri zote, uliokuwa ukifanyika jijini Mwanza.
Mkutano huo ulioanza Julai 2, yamehitimiswa Leo julai 5, 2025 katika ukumbi wa Rock City Mall Jijini Mwanza, ambapo mkutano huo ulikuwa na lengo la kutoa fursa ya kutathimini hali ya utoaji wa huduma afya na Usafi wa Mazingira, kubainisha maeneo yaliyofanya vizuri, maeneo yenye changamoto na sehemu zinazohitaji ubunifu kwa lengo la la kuboresha huduma na kuikinga jamii.
Aidha, Prof. Nagu amewataka washiriki wote kutumia mkutano huo, na kuutendea haki kwa kutoa taarifa kamili na Sahihi kwa jamii Ili kuweza kupunguza magonjwa ya mlipuko, huku akiwataka kuweka kipaumbele na kusemea maeneo yenye changamoto ili yaweze kupatiwa ufumbuzi mapema.
“ Mkutano huo wa siku nne naimani tutatumia tuliyojifunza na, tuendelee kuhimizana na kutoa taarifa kwa wakati Ili kudhibiti magonjwa mlipuko yasiendelee”. Amesema Nagu.
Hata hivyo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Jesca Lebba ameongeza mkutano huo kufanyika Mwanza, ametumia jukwaa hilo kuomba waganga wakuu pia kushiriki katika vikao vingine vijavyo kwa lengo la kushirikana na maafisa hao, huku akiwataka kwenda kusambaza kile walichojifunza kwa maana afua tiba ni muhimu Ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili jamii.
“Naaminii tukiendelea kufanya kazi kwa pamoja tutatoka wote katika afua za Afya na usafi wa mazingira”. Ameeleza Dkt. Jesca.
Kwa upande wake, mratibu mkuu wa mkutano wa mwaka wa tathimini ya utekelezaji wa huduma za afya na usafi wa mazingira katika mikoa na halmashauri Tanzania Bara, Seleman Yondu amewataka Washiriki na kuwasihi suala la kuzingatia na kufuata sheria na taratibuu za katika kutimiza wajibu wao. Aidha , amewaasa kuzingatia kufanya kazi kwa bidii, weledi na kuzingatia ubunifu unaoleta utendaji unaoleta matokeo.
Mkutano huo mwenye lengo la kuwapa kupitia utekelezaji, kubadilishana ujuzi na uzoefu miongoni mwa Maafisa Afya ngazi ya Mkoa na Halmashauri. Mkutano huo ulikuwa na kauli mbiu “utekelezaji wa afua za Afya na usafi wa mazingira ni msingi wa kinga endelevu dhidi ya magonjwa na Ustawi wa Jamii”.

SERIKALI YAHIMIZA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA MALEZI NA MAKUZI YA AWALI YA MTOTO NCHI NZIMA
OR - TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Afya Prof. Tumaini Nagu, amewakumbusha na kuwataka Makatibu Tawala wa Mikoa, Maafisa Lishe na Maafisa Maendeleo ya Jamii kuhakikisha wanatekeleza kikamilifu Programu ya Kitaifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (ECDI 2030) ili kuwawezesha watoto kukua katika mazingira bora na kuzifikia ndoto zao.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha uwasilishaji wa viashiria vya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kilichofanyika leo Julai 2, 2025 Jijini Dodoma, Prof. Nagu amesisitiza umuhimu wa utekelezaji wa programu hiyo kuanzia ngazi ya Mkoa hadi ngazi ya jamii.
“Ndugu washiriki, natumia fursa hii kuwakumbusha kwenda kutekeleza kikamilifu programu hii ya kitaifa ili kuwawezesha watoto wetu kukua na kufikia utimilifu wao, ndoto zao zitimie na waweze kuwa na mchango mkubwa kwa taifa letu,” alisema Prof. Nagu.
Ameongeza kuwa ni muhimu kwa Mikoa na Halmashauri zote kutenga bajeti mahsusi kwa ajili ya kuchochea utekelezaji wa programu hiyo katika maeneo yao.
Awali, Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF), Bwana Abbas Mtemba, alieleza kuwa kama Taifa bado kuna changamoto kubwa ya kuhakikisha watoto wote wanapata fursa sawa za ukuaji wa kiafya, kielimu, kiakili na kijamii.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (TECDEN), Bi. Mwajuma Kibwana, aliwasilisha takwimu za kitaifa zinazoonesha kuwa asilimia 47 pekee ya watoto wenye umri wa miezi 24 hadi 59 walio katika hatua ya ukuaji timilifu, huku asilimia 53 wakiwa bado wanakumbwa na changamoto mbalimbali katika malezi na makuzi yao.
Kikao kazi hicho kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makatibu Tawala wa Mikoa kutoka Mikoa 15, Maafisa Lishe wa Mikoa na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Maafisa lishe watakiwa kumaliza udumavu, ukondefu kwa Watoto, vitambi na vilibatumbo kwa watu wazima
OR - TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI Prof. Tumaini Nagu amewataka Maafisa Lishe kuimarisha elimu ya lishe kwa jamii ili kudhibiti udumavu na ukondefu kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 pamoja na uzito uliopitiliza kwa watu wazima.
Prof. Nagu ametoa agizo hilo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa uratibu wa masuala ya lishe nchini kwa maafisa lishe wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa waliokutana Jijini Dodoma kwa muda wa siku mbili kujadili namna ya kufanya maboresho katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku.
Katika maelekezo yake kwa watendaji hao, Prof. Nagu amesema Taifa linawategemea sana kubadilisha afya za watanzania hasa kwa kutoa elimu zaidi na kuishauri jamii juu ya ulaji bora ili kukabiliana na matatizo ya lishe.
“Nyie ndio jiwe la msingi kuhakikisha kuwa takwimu mbovu za lishe tulizonazo zinabadilika, tufanye kazi kweli ili tuwe na sababu ya kutembea kifua mbele kwamba tumeibadilisha jamii, kwa kuhakikisha tunatoa elimu juu ya ulaji bora na tunatekeleza program zinazowekwa kitaifa zenye lengo la kuboresha afya ya jamii yetu kupitia lishe bora” alisema Prof. Nagu.
Awali akisoma risala ya maafisa lishe hao January Dalushi amewasilisha ombi kwa Serikali na kuielekeza Taasisi ya MSD kuagiza Chakula Dawa ili vituo viweze kununua kwa urahisi, huku wakiomba Maafisa Lishe wawe moja ya Wataalam wanaoajiriwa kwenye Taasisi hiyo ili kutoa ushauri wa kitaalam kwenye bidhaa mbalimbali za Lishe zinazonunuliwa na Bohari ya Dawa ya Taifa.
Ajenda ya lishe inatajwa kuwa miongoni mwa vipaumbele muhimu vya kiuchumi ulimwenguni kote kutokana na athari za matatizo ya lishe katika ukuzaji wa uchumi na kuleta maendeleo endelevu ya ulimwengu ifikapo 2030.

WAZIRI MCHENGERWA AWAFUNDA MA RC WAPYA
Na John Mapepele
Mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwaapisha na kutoa maelekezo kwa viongozi kadhaa aliowateua ikiwa ni pamoja na Wakuu wa Mikoa, Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amekutana na kuwafunda.
Mhe. Mchengerwa amewataka kuzingatia maelekezo yote waliyopatiwa na Mhe. Rais huku akisisitiza kuwa wanatakiwa kuwatumikia wananchi kwa kuwa Serikali ni ya wananchi na wasisite kuwasiliana na Wizara wapatapo changamoto.
"Ndugu zangu nadhani mmeiona dhamira ya Mhe. Rais ya kuwataka kwenda kuwatumikia wananchi.Mimi siwezi kuongeza chochote nawaombeni mkayazingatie yale yote aliyowaelekeza" amesisitiza Mhe Mchengerwa
Katika hotuba yake baada ya kuwaapisha Wakuu wa Mikoa hao wapya Mhe. Rais ametoa maelekezo mahususi manne ikiwa ni pamoja na kuwataka kutunza amani na usalama wa wananchi katika mikoa yao kwa kuzingatia kuwa Tanzania inakwenda kwenye uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
Aidha amesisitiza kufanya usimamizi madhubuti wa fedha za Serikali ili zitumike kwa kuzingatia thamani ya huduma au bidhaa zinazonunuliwa.
Pia amewaagiza kuhakikisha Wakuu wote wa Mikoa nchini wanasimamià ukusanyaji wa mapato ya ndani bila kutumia nguvu.
Aidha ameelekeka kwenda kuwasikiliza wananchi na kusimama katikati yao huku akisisitiza kujishusha kwa wananchi.
"Kuna fedha nyingi lakini mara nyingi uongozi wa wananchi unafikiria kuwekeza katika vitu vingine badala ya kuwekeza katika mahitaji ya wananchi.Mathalan katika baadhi Halmashauri miundombinu mibovu lakini fedha inayopatikana inawekezwa katika biashara nyingine hiyo siyo sawa". Amefafanua Mhe Rais
Mkuu Mpya wa Mkoa wa Kigoma akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wakuu wa mikoa wapya katika kikao na Waziri Mchengerwa aliyeambatana na Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Adolf Ndunguru na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia TAMISEMI amesema wanakwenda kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Rais na kushirikiana na Wizara mama ya TAMISEMI ili kuwatumikia wananchi na kuboresha maisha yao.

NIMESAINI NOTISI ZA KUVUNJA MABARAZA YA MADIWANI - MCHENGERWA
Na. James K. Mwanamyoto OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kwa kuzingatia mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa sheria, tayari amekwisha saini notisi za kuvunjwa kwa Mabaraza ya Madiwani katika Mamlaka za Wilaya na Mamlaka za Miji, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Waziri Mchengerwa amesema hayo leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI jijini Dodoma.
Mhe. Mchengerwa amesema kuwa, notisi hizo za Kuvunjwa kwa Mabaraza ya Madiwani katika Mamlaka za Wilaya, na Mamlaka za Miji, 2025 zitatangazwa kwenye Gazeti la Serikali hivi karibuni.
Mhe. Mchengerwa amefafanua kuwa, notisi hizo zinaelekeza kwamba vikao vya Halmashauri na Kamati zake zinapaswa ziwe zimekoma siku saba kabla ya kuvunjwa kwa Bunge hapo tarehe 27 Juni, 2025.
“Vikao vya Halmashauri na Kamati zake zinapaswa kuwa zimekoma ifikapo tarehe 20 Juni, 2025 hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri atawajibika kwa kufanya kikao chochote cha Halmashauri au Kamati yake baada ya tarehe hiyo,” Waziri Mchengerwa amesisitiza.
Baada ya mabaraza ya madiwani kufikia ukomo tarehe 20 Juni 2025, Mhe. Mchengerwa ameelekeza masuala yote ya kiutendaji katika Halmashauri kusimamiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri, ambaye atakuwa Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kipindi cha mpito, akisaidiana na Wakuu wa Idara watakaokuwa kama wajumbe wa kamati.
Sanjari na hilo, Waziri Mchengerwa ameelekeza kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hataruhusiwa kuanzisha miradi au uwekezaji mpya ikiwa ni pamoja na kubadilisha au kurekebisha mradi, uwekezaji au uamuzi wowote uliopitishwa na Halmashauri kabla ya kuvunjwa.
“Matumizi mabaya ya mamlaka au kutotekeleza kwa ufanisi majukumu ya kiutawala kwa mujibu wa notisi hizi, kutamfanya Mkurugenzi kuwajibika binafsi kwa mujibu wa Sheria,” Mhe. Mchengerwa amehimiza.
Pia, Waziri Mchengerwa ameelekeza kwamba katika kikao cha kwanza cha Baraza jipya la Madiwani baada ya uchaguzi kufanyika, Mkurugenzi wa Halmashauri atapaswa kuwasilisha taarifa ya maamuzi na mwenendo wa vikao vya menejimenti vilivyofanyika wakati wa kipindi cha mpito.
Aidha, Waziri Mchengerwa amewashukuru na kuwapongeza Madiwani wote waliomaliza muda wao wa uongozi kwa kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.

MANYARA BINGWA RIADHA WASICHANA NA WAVULANA MITA 1,500
OR-TAMISEMI
Wanariadha wanaoshiriki Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi kutoka Mkoa wa Manyara, wameibuka kidedea katika mbio za mita 1,500 kwa upande wa Wasichana na Wavulana.
Mariam Gadiye, ameipa Manyara ubingwa kwa upande wa Wasichana, baada ya kutumia muda wa dakika 5:55:74 katika fainali iliyofanyika juni 15,2025 kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu Kleruu Iringa.
Manyara pia imewika katika mbio hizo za mita 1,500 Wavulana, baada ya Joshua Kidaghadawa kuibuka mshindi kwa kukimbia dakika 4:20:64 akifuatiwa na Apolinary D Apolinary pia wa Manyara aliyetumia dakika 4:26:68.
Nafasi ya tatu wavulana ilienda kwa Oreshiki Ndakaya kutoka Mkoa wa Arusha, aliyetumia dakika 4:26:92 na kuhitimisha Fainali hiyo ya UMITASHUMTA 2025 Riadha mita 1,500.
Aidha mkoa wa Kagera umefanikiwa kuibuka na ubingwa wa riadha upande wa Mita 400,kufuatia ushindi wa Dominko Mikoduni aliyetumia muda wa sekunde 54:90 akifuatiwa na Maseto Elenjori wa Arusha sekunde 55:27.
Wasichana mita 400 Ubingwa umeenda Mkoa wa Shinyanga, baada ya Rehema Nyalu kukimbia kwa muda wa dakika 01:03:41 akifuatiwa na Catarina Charles wa Mwanza dakika 01:04:38.
Katika fainali ya Mita 100, Janeth Mhebule kutoka mkoa wa Mwanza alimaliza katika nafasi ya kwanza akitumia muda wa sekunde 13:13, na upande wa Wavula Mkoa Mara uliibuka na ushindi kupitia kwa Anold Mkomangiwa ubingwa aliyetumia sekunde 11:65

MHE MCHENGERWA AWATAKA MA RC, DC KUONGOZA JOGGING KWENYE MAENEO YAO
Na John Mapepele
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini kuwaongeza wananchi katika maeneo yao kufanya "jogging" na mazoezi ili kuimarisha afya.
Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo leo Juni 14, 2025 mara baada ya kuongoza na kuhitimisha mbio za pole pole (jogging) za kilomita 10 zilizoratibiwa na Wizara yake katika eneo la Mji wa Serikali wa Mtumba jijini Dodoma.
"Hamasa hii ya kufanya mazoezi iliasisiwa na viongozi wetu wakuu kuanzia enzi za Baba wa taifa letu Mwalimu Nyerere hadi Rais wetu wa sasa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan lengo likiwa kuimarisha afya na kujikinga na magonjwa nyemelezi hivyo na sisi tuna wajibu wa kuendelea kuwahamasisha watumishi wa Serikali na wananchi kwa ujumla kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye " amefafanua Waziri Mchengerwa
Aidha, amewataka watumishi wa TAMISEMI kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi wao pamoja na familia zao ili jamii yote iweze kuimarisha afya.
Amesema utamaduni wa kufanya mazoezi ukijengeka siyo tu kwamba utasaidia kuimarisha afya bali utasaidia kupunguza gharama za kutibu magonjwa ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na tabia bwete.
Pia Waziri Mchengerwa ametoa wito kwa watanzania kuwa na tabia za kupima afya zao badala ya kungojea hadi wanapoumwa.
Mbio hizo za pole zilizohudhuriwa na mamia ya watumishi wa TAMISEMI ziliishia katika jengo la Ofisi ya TAMISEMI ambako kulikuwa na zoezi la upimaji wa afya kwa hiari.
Kwa upande mwingine, Mhe. Mchengerwa amesema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo na Wizara ya Elimu zinaratibu Mashindano ya Michezo kwa Shule za Msingi ( UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISSETA) ambapo amefafanua kuwa mashindano hayo yanasaidia kuibua vipaji vya wachezaji.
Amesema Serikali imeendelea kuboresha mashindano hayo ili kuwajengea utamaduni wa wanafunzi kufanya mazoezi na kupenda michezo katika umri mdogo.

MANYARA NA MWANZA MABINGWA RIADHA MITA 800
OR -TAMISEMI
Catarina Charles kutoka Mkoa wa Mwanza na Joshua Gidawaghaida wa Manyara, wameibuka washindi katika fainali ya riadha mita 800 Wasichana na Wavulana, katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi na Sekondari.
Fainali hiyo imefanyika Asubuhi ya tarehe 14 juni 2025, katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Kleruu Manispaa ya Iringa ambapo Catarina aliyeibuka mshindi wa mita 800 kwa Wasichana alitumia dakika 2:30:22 na kwa wavulana Joshua alitumia dakika 2:11:7.
Naye Joyce Maganga aliuwakilisha vema Mkoa wa Mara kwa kushika nafasi ya pili akitumia dakika 2:32:13, na Mariam Gadiye wa Manyara akashika nafasi ya tatu akitumia dakika 2:33:27.
Upande wa Wavulana Isack Michael wa Kilimanjaro alishika nafasi ya pili kwa kukimbia dakika 2:14:63 na Manyara ikashika nafasi ya tatu baada ya Apolinary P Apolinary kukimbia kwa dakika 2:15:91.
Mchezo wa riadha uko katika hatua mbalimbali kwenye UMITASHUMTA 2025, ambapo licha ya fainali ya mita 800, June 14,2025 pia kumefanyika nusu fainali ya Mita 400 kupokezana vijiti, mita 1,500, fainali ya mita 200 na fainali ya kuruka yote ikiwa ni kwa wasichana na wavulana.

HAKIKISHENI MNAKUWA WABUNIFU KATIKA KUANDAA MIRADI YA MAENDELEO- ADOLF NDUNGURU
Na.Asila Twaha, OR - TAMISEMI
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ndugu Adolf Ndunguru amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi, Sehemu ya Mipango na Uratibu Makatibu Tawala Wasaidizi Uchumi na Uzalishaji, Maafisa Mipango na Uratibu wa Halmashauri na Waweka Hazina wa Halmashauri kuhakikisha wanakuwa wabunifu na wataalamu wenye uthubutu katika kuhakikisha kila Halmashauri inakuwa na miradi ya maendeleo itakayoandaliwa na kutekelezwa kwa kuzingatia miongozo na ushauri wa kitaalamu.
Ndunguru ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo kwa wataalamu hao yalikuwa yamefanyika kwa awamu mbili ampapo awamu ya kwanza yamefanyika kuanzia tarehe 3-6 Juni, 2025 na awamu pili yalianza tarehe 10-13 Juni, 2025.
“Serikali ina imani kubwa sana nanyinyi tekelezeni majukumu yenu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kazi na muwe wepesi wa kueleza mapema changamoto kama zinatokea ili zishughulikiwe kwa wakati” amesema Ndunguru
Amewataka kwa waweka hazina wanatumia mifumo ya ndani kutunza namba za siri za kuingilia kwenye mfumo wa mapato, kufuatilia fedha zilizokusanywa na hazijawasilishwa benki kwa wakati, kufanya usuluhishi wa kibenki kwa akaunti zote za halmashauri na vituo vya kutolea huduma kwa wakati, matumizi ya TAUSI App (Toleo la Kiganjani) kuhakiki uhalali wa stakabadhi, vibali na leseni na kudhibiti ugawaji wa Float kwa wahasibu wa mapato na wakusanya ushuru.
Ndunguru amesema, dhamira ya Serikali ya kuanzisha na kutekeleza miradi kwa njia ya Special Purpose Vehicle (SPV) na Public-Private Partnership (PPP) ni kuhakikisha inafanikiwa na Ofisi ya Rais -TAMISEMI itaendelea kutoa elimu kwa viongozi wa mikoa, wilaya na halmashauri kwa kuwashirikisha viongozi wa kisiasa ili kuhakikisha wanaelewa vyema malengo ya miradi hiyo ili kuondoa mwingiliano wa majukumu na hivyo kuwezesha utekelezaji wake kwa ufanisi katika maeneo yenu.
“Hakikisheni mnakamilisha uingizaji wa bajeti ya mwaka 2025/26 na bakaa ya 2024/25 katika mfumo wa malipo kwa muda uliopangwa ili kuwezesha kuanza kwa matumizi ya fedha” amesisitiza Ndunguru
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais -TAMISEMI Bi. Beatrice Kimoleta amemueleza Katibu Mkuu kuwa pamoja na wataalamu hao kujengewa uwezo pia wamepata fursa ya kufundishwa mada mbalimbali ikiwemo mada ya uandaaji wa maandiko ya miradi ya kimkakati.
Beatrice ametoa wito kwa wataalamu hao kuhakikisha kuwa mafunzo na elimu waliyoipata inafika pia kwa watumishi wanaowasimamia ili kuongeza tija katika usimamizi wa shughuli za Serikali katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo usimamizi wa ukusanyaji wa mapato, miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

WAVU KWAENDELEA KUNOGA UMITASHUMTA
OR-TAMISEMI
Timu ya wasichana kutoka Makao Makuu Dodoma imeonyesha ubabe kwenye mchezo wa wavu kwa kuichapa timu ya wenyeji Iringa kwa seti 3-0.
Dodoma walionyesha kiwango cha juu cha mchezo, wakitawala seti ya kwanza kwa ustadi mkubwa na kuipora Iringa matumaini ya ushindi. Jitihada za Iringa kujibu mashambulizi hazikuzaa matunda baada ya Dodoma kurejea kwa moto zaidi na kushinda seti mbili zilizofuata, na hatimaye kukamilisha ushindi wa seti 3-0.
Katika michezo mingine ya wasichana, Mkoa wa Tabora ulishindwa kuhimili vishindo vya Mtwara na kuambulia kichapo cha seti 0-3, matokeo yaliyoonyesha uimara wa kikosi cha kusini mwa Tanzania.
Kwa upande wa wavulana, mchezo uliovutia kati ya Manyara na Singida uligeuka kivutio baada ya Manyara kuibuka na ushindi mwembamba wa seti 3-2, katika pambano lililoshuhudia ushindani mkali kutoka pande zote mbili.
Katika michezo mingine, Mkoa wa Arusha – wanaoitwa watoto wa kitalii – waliwaliza wachimba madini kutoka Geita kwa kuwachapa kwa seti 3-0, huku Dar es Salaam nao wakijihakikishia pointi tatu muhimu kwa kuifunga Njombe kwa seti 3-0.
Mashindano haya yanaendelea kuvutia hisia kali kutoka kwa wapenzi wa michezo, huku kila timu ikipambana kwa bidii kutafuta nafasi ya kutwaa ubingwa wa mwaka huu.

CRICKET YAENDELEA KUSHIKA KASI UMITASHUMTA IRINGA
OR-TAMISEMI
Timu za mchezo wa Cricket zimeendelea kuoneshana ubabe kwenye mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi, yanayoendelea kitaifa Mkoani Iringa.
Kwa upande wa Wavulana, timu ya Mkoa wa Morogoro ilionesha ubabe baada ya kuifunga Dar es Salaam kwa mikimbio 132 kwa 63 kwenye mchezo wa awali uliochezwa katika viwanja vya shule ya Sekondari Lugalo juni 13, 2025.
Kwa upande wa Cricket Wasichana, timu ya mkoa wa Tanga iliibuka mshindi kwa mikimbio 44 dhidi ya Dodoma iliyopata mikimbio 42, katika mchezo mwingine uliofanyika kwenye uwanja huohuo wa Shule ya Sekondari Lugalo.
Mchezo mwingine wa kusisimua wa Cricket wavulana, ulizikutanisha Dodoma na Morogoro, ambapo matokeo yaliipelekea Dodoma kuibuka mshidi wa mikimbio 85 kwa 83.
Mchezo wa Cricket, unachezwa kwa mara ya kwanza katika UMITASHUMTA 2025, na mwaka huu unahusisha jumla ya mikoa minne ya Tanga,Dodoma, Morogoro na Dar es Salaam.
Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA, yanaandaliwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo.

MARA YAENDELEZA UBABE HANDBALL WASICHANA
OR-TAMISEMI
Timu ya Mpira wa Mikono (Handball) Wasichana kutoka Mkoa wa Mara, imeshinda mchezo wa nne mfululizo katika mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi yanayoendelea mkoani Iringa.
Katika mchezo uliochezwa leo tarehe 13 Juni 2025 kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Iringa Wasichana, Mkoa wa mara uliibuka na ushindi mnono baada ya kuifunga Pwani magoli 26-12.
Kwa matokeo hayo sasa timu ya mkoa wa Mara inaongoza kundi C, ikiwa imebakiwa mchezo mmoja dhidi ya Shinyanga, huku timu zingine katika kundi hilo zikiwa ni Morogoro Iringa na Dodoma.
Katika michezo mingine ya kikapu Wasichana iliyochezwa asubuhi ya leo, Tanga iliifunga Ruvuma magoli 10-0, na Mbeya ikatoshana nguvu ya magoli 10-10 dhidi ya Katavi.
Upande wa Wavulana, timu ya Mkoa wa Arusha ilikubali kipigo cha magoli 15-6 kutoka kwa Njombe kwenye mchezo wa awali uliochezwa kwenye uwanja huohuo wa Shule ya Sekondari Wasichana Iringa.
Mashindano ya UMITASHUMTA yaliyofunguliwa rasmi tarehe 9 Juni 2025 na Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa, yanaendelea kushika kasi katika viwanja vya Kichangani, Shule ya Sekondari Lugalo,Shule ya Sekondari Wasichana Iringa na Chuo cha ualimu Kleruu.

GEITA YAENDELEZA UBABE KIKAPU WASICHANA
Timu ya Mpira wa Kikapu Wasichana kutoka Mkoa wa Geita, imeendelea kufanya vizuri katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi yanayofanyika kitaifa mkoani Iringa.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa asubuhi ya leo Tarehe 12 Juni 2025, katika viwanja vya Kichangani, Geita iliichapa Manyara kwa Vikapu 32-7.
Mchezo mwingine ulizikutanisha timu za mikoa ya Dar es Salaam na Mbeya, uliomalizika kwa Mbeya kukubaki kipigo cha jumla ya Vikapu 8-19.
Wenyeji wa UMITASHUMTA kwa mwaka uliopita 2024 Mkoa wa Tabora, nao waliendelea kujiimarisha katika hatua ya makundi, kwa kuiadhibu Songwe na kupata ushindi wa 19-8.
Mchezo wa Mpira wa Kikapu unachezwa kwa mara ya pili katika mashindano ya UMITASHUMTA, ukiwa ulianza rasmi katika mashindano ya mwaka uliopita 2024, huku timu ya Mkoa wa Arusha ikiwa ndio mabingwa watetezi kwa upande wa Wasichana.
Mashindano haya ya UMITASHUMTA na yale ya UMISSETA,yanaratibiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI,ikishirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo.

MWANZA YAIADHIBU PWANI SOKA MAALUMU WASICHANA
OR-TAMISEMI
Timu ya soka ya Wasichana maalumu kutoka mkoa wa Mwanza, imeibuka na ushindi mnono dhidi ya Pwani katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi na Sekondari yanayoendelea mkoani Iringa.
Mchezo huo umepigwa juni 11, 2025 katika uwanja wa Kichangani Manispaa ya Iringa, ikiwa ni muendelezo wa mashinda ya UMITASHUMTA 2025.
Mwanza imeshinda kwa Jumla ya magoli 5-0 hivyo kuifanya kujiweka vizuri kusonga mbele katika hatua zinazofuata.
Kwa upande wa Soka maalumu Wavulana, timu ya soka ya Mkoa wa Dar es salaam, ilipata ushindi mnono baada ya kuifunga Shinyanga jumla ya magoli 5-1.
Michezo hiyo ya soka maalumu wasichana na wavulana, iko kwenye hatua ya Makundi na inatarajiwa kuendelea kesho Juni 12,2025 katika viwanja vya Kichangani.
Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA 2025, yanaratibiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI, ikishirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

SANAA ZA MAONESHO ZAANZA RASMI UMITASHUMTA 2025 MKOANI IRINGA
OR-TAMISEMI
Sanaa za Maonesho ni miongoni mwa michezo inayoshindaniwa katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) yanayofanyika kitaifa mkoani Iringa.
Mashindano haya yanajumuisha vikundi vya ngoma, kwaya, na waimbaji binafsi. Leo Juni 11, 2025, mikoa mbalimbali imeanza kushindana katika fani ya kwaya kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu Kleruu, Manispaa ya Iringa.
Leah Kihimbi, Mratibu wa Sanaa za Maonesho kwa mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA 2025, amesema sanaa hizi ni jukwaa la kuibua na kuendeleza vipaji vya watoto katika fani mbalimbali za sanaa.
> "Sanaa imebadilika sana siku hizi. Sio tu burudani tena, bali sasa ni ajira rasmi. Tuna mifano hai ya wasanii waliofanikiwa kupitia sanaa, ndani na nje ya nchi. Hapa tunawaandaa wasanii watakaokuwa na taaluma pia," amesema Leah.
Ameongeza kuwa mikoa 26 inashiriki mashindano ya mwaka huu, na anaamini kupitia maonesho haya, vipaji vipya vitazaliwa na kulelewa ili kufikia mafanikio katika miaka ijayo.
Mbali na ngoma za asili na kwaya, Sanaa za Maonesho pia zinajumuisha muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Fleva, unaopata umaarufu mkubwa miongoni mwa vijana.
Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA huandaliwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Kauli mbiu ya mashindano ya mwaka huu ni:
"Viongozi Bora ni Msingi wa Maendeleo katika Taaluma, Sanaa na Michezo – Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu."

KILIMANJARO, RUVUMA NA NJOMBE MABINGWA RIADHA MAALUMU UMITASHUMTA 2025
Wakimbiaji kutoka mikoa ya Kilimanjaro,Njombe na Ruvuma,wameng'ara katika mchezo wa riadha maalumu (Wasichana na Wavulana) katika mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi.
Mchezo wa riadha umeanza rasmi leo juni 11,2025 kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Kleruu Manispaa ya Iringa, ambapo mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA yanafanyika Kitaifa mwaka huu.
Katika mbio za leo upande wa Wasichana Mita 100 maalumu, Neema Efrahim kutoka Kilimanjaro na Careen Mohamed kutoka mkoa wa Mwanza, waliongoza wakifuatiwa na Martha Emmanue kutoka Songwe na Pendo Mohamed wa Singida.
Nao wavulana Mita 100 maalumu waliongozwa na Atumani Muhagama kutoka Mkoa wa Ruvuma, akifuatiwa na Edward Kimai wa Mkoa wa Mara huku Yohana Robert wa Dodoma akimaliza katika nafasi ya tatu.
Mratibu wa Mchezo wa riadha katika UMITASHUMTA & UMISSETA 2025 Neema Chongolo, amesema kuwa wanatarajia ushindani mkubwa kama ambavyo imekuwa katika miaka iliyopita.
"Kama unavyojua riadha huwa inakuwa na ushindani mkubwa kutokana na maandalizi ambayo inafanywa na mikoa wanapotoka wanamichezo, kwa hiyo mwaka huu pia tutarajie hivyohivyo" amesema Neema
Kuhusu riadha maalumu amesema mwaka huu mikoa imehamasika kuleta wachezaji wengi, jambo linalodhihirisha kuendelea kukua kwa mchezo wa riadha kwenye UMITASHUMTA.

Mtwara Wasichana Yaendeleza Ubabe UMITASHUMTA 2025
Na OR-TAMISEMI
Timu ya mpira wa wavu ya wasichana kutoka mkoa wa Mtwara ambao ni mabingwa watetezi imeanza kwa kishindo kampeni yake ya kutetea ubingwa katika mashindano ya UMITASHUMTA 2025.
Mtwara imeonesha dhamira ya kutetea ubingwa baada ya kuibuka na ushindi wa seti 3-1 dhidi majirani zao mkoa wa Lindi katika mchezo wa kusisimua uliochezwa kwenye viwanja vya Kleruu, Iringa.
Mtwara walionyesha kiwango cha juu na kujiamini tangu mwanzo, na kushinda seti ya kwanza mabla ya Lindi kujibu mapigo na kusawazisha kwa kuchukua seti ya pili.
Hata hivyo uhodari na umakini wa Mtwara uliamua hatma ya mchezo, wakichukua seti mbili zilizofuata na hivyo kuibuka na ushindi wa jumla wa 3-1.
Katika michezo mingine ya ufunguzi, timu ya wavulana ya Kilimanjaro iliwaduwaza Tabora kwa ushindi wa seti 3-0, ikionyesha kiwango bora na kasi ya hali ya juu,huku wenyeji Iringa ikiungwa mkono na mashabiki wake wa nyumbani, iliibuka kidedea dhidi ya Kagera kwa ushindi wa seti 3-1, katika mchezo mwingine uliovutia mashabiki wengi.
Mashindano ya UMITASHUMTA 2025 yanaendelea kesho kwa michezo mingine ya makundi, ambapo kila timu itakuwa vitani kuwania nafasi ya kufuzu hatua za michuano

FANYENI MSAWAZO SAHIHI WA WATUMISHI KATIKA SEKTA YA AFYA KATIKA HALMASHAURI ZENU – MHE. DKT. DUGANGE
OR - TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia afya Mhe. Dkt. Festo Dugange amewalekeza Wakurugenzi wa Halmashauri kufanya msawazo wa watumishi wa sekta ya afya ili kukizi mahitaji ya wananchi wakati ambapo Serikali inaendelea kutoa vibali vya ajira katika sekta hiyo.
Dkt. Dugange amesema hayo tarehe 9 Juni, 2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Selemani Jumanne Zedi, Mbunge wa Jimbo la Bukene aliyeuliza
Je, lini Serikali itamaliza tatizo la upungufu wa watumishi wa kada ya Afya - Bukene.
“Katika maeneo yote ya zahanati yenye mtumishi mmoja fanyeni msawazo sahihi wa ndani wa watumishi kutoka kwenye vituo vyenye watumishi wengi ili kuendelea kutoa huduma muhimu kwa wananchi” Mhe. Dkt. Dugange
Serikali inaendelea kutoa vibali vya ajira kila mwaka, ambapo kuanzia mwaka wa fedha 2020/21 hadi 2024/25 jumla ya watumishi wa kada ya afya 34,720 wameajiriwa na kupangiwa vituo.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2020/21 hadi 2024/25 halmashauri ya Wilaya ya Nzega imepangiwa jumla ya watumishi 111 ambao wamepangwa katika hospitali ya wilaya, vituo vya afya na zahanati. Kati ya hao, jimbo la Bukene limepelekewa jumla ya watumishi 59.
Serikali itaendelea kuajiri watumishi wa sekta ya afya kwa awamu na kuwapanga katika maeneo yenye upungufu wa wataalamu hao ikiwemo halmashauri ya wilaya ya Nzega.

MHANDISI SEFF AWATAKA MAKANDARASI MIRADI YA DHARURA (SERC) KUZINGATIA MASUALA YA USALAMA KAZINI NA UTUNZAJI MAZINGIRA
Dar es Salaam
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff amewataka makandarasi wanaotekeleza kazi za ukarabati na matengenezo ya barabara vivuko na madaraja katika maeneo yaliyoharibiwa na mvua za El nino nchini kutekeleza mikataba yao kwa wakati huku wakizingatia masuala ya msingi ikiwemo usalama mahali pa kazi pamoja na utunzaji wa mazingira.
Mhandisi Seff ameyasema hayo wakati wa kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam kati ya TARURA na Makandarasi hao wanaotekeleza miradi hiyo nchi nzima.
“Hakikisheni katika utekelezaji wa miradi yote mnakamilisha kwa wakati pia mnazingatia masuala yote ya usalama na mazingira kama ilivyoainishwa kwenye makubaliano ya jumla ya miradi hii”Alisisitiza.
Naye, Mratibu wa miradi ya Benki ya Dunia kutoka TARURA Mhandisi Humphrey Kanyenye amesema kwamba wao kama waratibu wa miradi hiyo wapo tayari kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha kila mkandarasi anatekeleza majukumu yake kwa ufanisi ikiwemo utunzaji wa mazingira ili kuepuka kwenda kinyume na matakwa ya utekelezaji wa miradi ya benki ya dunia.
Wakati huohuo Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Geofrey Mkinga amewahakikishia ushirikiano makandarasi kuhakikisha wanakimbizana na muda na kukamilisha miradi hiyo yenye tija kwa mkoa wake pamoja na nchi nzima kwa wakati kwani Dar es Salaam ni moja ya mkoa wenye miradi hiyo ya dharura.
Aidha, katika kikao hicho makandarasi walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali kwa uelewa zaidi kabla ya kuanza utekelezaji wa kazi ambapo walijibiwa na kuhakikishiwa kuwa TARURA kwa niaba ya Katibu Mkuu OR TAMISEMI itahakikisha hakuna mkwamo wowote kwani dhamira ya Serikali ni kuona miradi inakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa.
Miradi ya SERC inatekelezwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa DMDP II ambapo mtekelezaji mkuu ni Katibu Mkuu OR-TAMISEMI ambapo amekasimu utekelezaji huo kwa Mtendaji Mkuu TARURA.

Vumbi Latimuka UMITASHUMTA Iringa: Dodoma, Songwe Zatingisha katika Mpira wa Mikono
OR-TAMISEMI
Mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya taifa yameanza kwa kishindo katika viwanja mbalimbali vya michezo vilivyopo mkoani Iringa, huku viwanja vya Chuo cha Ualimu Klerruu, Shule ya Sekondari ya Wasichana Iringa, na Lugalo vikianza kutimua vumbi kufuatia mechi za hatua ya makundi.
Katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Iringa, michezo ya mpira wa mikono kwa upande wa wavulana imepigwa kwa ushindani mkubwa. Timu ya Songwe ilianza kwa kishindo kwa kuichapa Kigoma kwa mabao 15–9, huku Morogoro ikiitandika Shinyanga kwa magoli 16–11.
Mkoa wa Dodoma umeonyesha uwezo mkubwa baada ya kuifunga Kilimanjaro kwa magoli 20–6 kabla ya kuendeleza ubabe kwa kuichapa Singida kwa mabao 18–10 na kujinyakulia pointi muhimu katika kundi lao.
Mashindano haya yanaendelea kuvutia mashabiki wengi huku wachezaji wakionesha vipaji vya hali ya juu katika kuwania nafasi za juu kuelekea hatua ya makundi.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA RASMI MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025
OR-TAMISEMI, Iringa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amezitaka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kushirikiana kikamilifu katika kukamilisha mradi wa ujenzi wa shule 56 za kuendeleza vipaji vya michezo.
Mhe. Majaliwa ametoa agizo hilo leo, Juni 9, 2025, wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISSETA), yaliyofanyika katika Viwanja vya Kichangani, Kata ya Kihesa, Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa.
Aidha, amezitaka Ofisi ya Rais – TAMISEMI pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhakikisha kuwa ratiba za michezo zinawekwa rasmi kwenye mipango ya kila shule na kutekelezwa ipasavyo ili kutoa nafasi kwa wanafunzi kushiriki michezo mara kwa mara kwa lengo la kukuza vipaji.
> "Katika shule zetu tunahitaji ratiba za michezo ili vijana wetu baada ya masomo waweze kushiriki katika shughuli za michezo. Hili litasaidia kuinua vipaji na kuwaandaa kwa mashindano haya ya kitaifa," alisema Waziri Mkuu.
Mhe. Majaliwa amevitaka vyama vya michezo vya kitaifa kupeleka wataalamu kwenye mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA ili kuwabaini wachezaji wenye vipaji maalum watakaoendelezwa kwa lengo la kuunda timu bora za taifa.
Aidha, amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote kuhakikisha walimu wa michezo wanapewa mafunzo maalum ya kisasa kuhusu sheria, mbinu na mabadiliko ya michezo, na kuwapeleka kwenye vyuo vya michezo vilivyopo nchini ili kuongeza ufanisi wa ufundishaji.
Waziri Mkuu pia ameagiza Kituo cha Mafunzo cha Malia kutumika kikamilifu kwa ajili ya kuwajengea uwezo walimu wa michezo ili kusaidia kukuza vipaji vya wanafunzi katika ngazi ya shule.
Vilevile, amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa michezo hayavamiwi na shule zote za msingi na sekondari zinakuwa na viwanja kwa ajili ya michezo mbalimbali inayoshirikishwa kwenye mashindano haya.
Ameitaka TAMISEMI, kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kuandaa mpango mkakati wa kitaifa utakaohakikisha kila shule inakuwa na miundombinu ya michezo, ikiwemo viwanja vya riadha, ili kuimarisha ushiriki wa wanafunzi katika michezo.
Pia, amezihimiza taasisi hizo kushirikiana na wadau wa michezo, kama makampuni ya biashara yanayodhamini michezo, kuendeleza vipaji vilivyoibuliwa mashuleni kwa lengo la kuzalisha wanamichezo bora.
Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu ameitaka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoa vibali kwa shule binafsi na academies zinazolenga kukuza vipaji vya michezo kuanzia ngazi ya awali, ili ifikapo umri wa miaka 14 vijana wawe wameimarika kitaaluma na kimwili.
Mwisho, amewataka Watanzania wote kujenga tabia ya kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kuwa na afya bora ambayo ndio msingi wa taifa lenye nguvu.

BIL. 2.4 ZATUMIKA MWENYE MICHEZO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025
SERIKALI YA AWAMU YA SITA IMEFANYA JUHUDI KUBWA KUIMARISHA MICHEZO SHULENI
OR-TAMISEMI
Zaidi ya shilingi Bilioni 2.4 zimetengwa na serikali kupitia Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa mwaka 2025 kwaajili ya Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa shule za Msingi na Sekondari.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainab Katimba wakati wa uzinduzi wa Mashindano hayo kitaifa katika viwanja vya Kichangani kata ya Kihesa Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa.
"Nitumie nafasi hii kumshukuru sana Mhe.Rais kwa kuendelea kutuwezesha na kutupatia fedha za kutosha kuandaa na kuendesha mashindano haya kila mwaka, jambo ambalo limeendelea kukuza sekta ya michezo Nchini" Amesema
"Michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA imekuwa na mchango mkubwa katika kuandaa wanamichezo wa timu za Taifa ambao wamekuwa wakiliwakilisha Taifa katika michezo mbalimbali" ameeleza Mhe.Katimba
Aidha Mhe.Katimba amesema kuwa michezo ya shule imekuwa sehemu ya kuimarisha Muungano kutokana na ushiriki wa wanafunzi kutoka Tanzani Bara na Visiwani Zanzibar.
Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA inafanyika Mkoani Iringa, ikiwa ni zaidi ya miaka 30 tangu yalipofanyika kwa mara ya mwisho Mkoani humo.

WAZIRI MKUU MAJALIWA KUFUNGUA RASMI UMITASHUMTA & UMISSETA 2025 LEO
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, leo Juni 9,2025 anatarajiwa kufungua rasmi mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari yanayofanyika Kitaifa Mkoani Iringa.
Ufunguzi huo utafanyika katika viwanja vya michezo Kichangani Manispaa ya Iringa, na kuhudhuriwa na wanamichezo zaidi ya 3,000 kutoka mikoa yote ya Tanzania, ambao tayari wameshawasili Mkoani humo.
Maandalizi ya zoezi hilo la ufunguzi yameshakamilika, likiwa lilitanguiiwa na ufunguzi wa Baraza la UMITASHUMTA lililofanyika jana tarehe 8 Juni 2025 katika viwanja vya shule ya Sekondari Lugalo-Iringa.
UMITASHUMTA & UMISSETA inaandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Utamaduni na Michezo.
Kauli mbiu ya Mashindano ya mwaka huu ni "Viongozi bora ni msingi wa maendeleo na Taaluma, Sanaa na Michezo,Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu"

MIKOA YAENDELEA KUWASILI IRINGA KUSHIRIKI MASHINDANO YA UMITASHUMTA 2025
OR- TAMISEMI
Wanamichezo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wameendelea kuwasili mkoani Iringa kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) yanayotarajiwa kuanza rasmi tarehe 9 Juni, 2025.
Mashindano haya, pamoja na yale ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Sekondari (UMISSETA), yanafanyika kitaifa katika Mkoa wa Iringa, na yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Akizungumza mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Shule ya Sekondari Iringa Wasichana, Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Ngara, Mwalimu James John Ling’wa, alisema Mkoa wa Kagera umejiandaa kikamilifu kushiriki katika mashindano ya mwaka huu.
> “Tumejiandaa vizuri. Tumefika tukiwa na wanafunzi zaidi ya 100 na tuna uwakilishi wa kila mchezo. Tunamshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuipa michezo hii umuhimu mkubwa,” alisema Mwalimu Ling’wa.
Kwa upande wake, Kocha wa timu ya mpira wa miguu ya Mkoa wa Mwanza, Mainu David Kayombo, amesema wamewasili mapema Iringa ili kuwapa wachezaji muda wa kuzoea hali ya hewa na mazingira, ili waweze kushindana kwa ufanisi zaidi.
Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA 2025 yanaandaliwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Kaulimbiu ya mashindano ya mwaka huu ni:
"Viongozi bora ni msingi wa maendeleo ya Taaluma, Sanaa na Michezo. Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu."

OR – TAMISEMI yasisitiza ubunifu katika kuwekeza Miradi ya Maendeleo - Kimoleta
Ofisi ya Rais – TAMISEMI imewataka Makatibu Tawala wasaidizi sehemu za mipango, uratibu, uchumi na uzalishaji, wakuu wa idara za mipango na uratibu na waweka hazina wa halmashauri kubuni miradi ya maendeleo kwa kuzingatia mtaji wa rasilimali walizonazo katika maeneo yao.
Wito huo umetolewa tarehe 6 Juni, 2025 mkoani Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Bi. Beatrice Kimoleta kwa niaba ya Katibu Mkuu OR – TAMISEMI, wakati akihitimisha mafunzo ya uendeshaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo yaliyotolewa kwa muda wa siku nne kwa maafisa hao yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo zaidi kabla ya kuanza kutekelezwa kwa bajeti ya Serikali ya mwaka 2025/2026.
Bi. Kimoleta amesema imani ya Serikali baada ya mafunzo hayo ni washiriki kuwa wabunifu, kila mkoa na halmashauri hatua itakayopimwa kwa kuangalia namna maandiko ya uanzishwaji wa miradi ya vyanzo vipya vya mapato yalivyozingatia ubunifu na mtaji wa rasilimali walizonazo katika maeneo husika.
“Hatutegemei tena kuona kila halmashauri inawasilisha andiko la kujenga vituo vya mabasi (stendi) yaani halmashauri zaidi ya 80 nyote mna wazo moja, tunachokiamini kuanzia sasa ni kuona maandiko yenye mawazo tofauti tofauti hasa yaliyozingatia kuwa eneo hili tuna rasilimali hii tukifanya mradi fulani utakuwa na tija kwa maendeleo ya jamii yetu, alisema Kimoleta.

SIMAMIENI MAABARA ZOTE ZA HOSPITALI ZA HALMASHAURI ZIPATE ITHIBATI
OR - TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia afya Prof. Tumaini Nagu amewaelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa (RMO’s) kuhakikisha wanasimamia upatikanaji wa ithibati katika maabara za hospitali zote za Halmashauri zilizopo katika Mikoa yao.
Prof. Nagu ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao cha majumuisho wa ziara yake ya usimamizi shirikikishi katika Mkoa wa Pwani kilichofanyika katika Halmashauri ya mji wa kibaha mkoani hapo.
“Ithibati ndio alama ya ubora, ukiwa nayo maana yake wewe umekidhi vigezo hivyo huduma zako ni bora, hivyo tunaanza na maabara zote katika ngazi ya afya msingi kuhakikisha tunapata ithibati ya ubora wa huduma zetu” amesisitiza
Aidha, Prof. Nagu amewataka watumishi kutoa huduma zenye ubora kwa kuzingatia miongozo (SOP) ya utoaji wa huduma katika maeneo ya kazi.
“Lazima tuzingatie miongozo ya utoaji wa huduma. Hivyo naelekeza standard operation procedures (SOP’s) zipatikane katika maeneo husika na zitumike kuhakikisha huduma zinazotolewa ni bora. Aidha, vifaa kinga (PPEs) zipatikane na zitumiwe na watoa huduma hususani katika maeneo kama ya kutakasia nguo, maabara, chumba cha kuhifadhi maiti pamoja na maeneo ya kuchoma taka” amesema Prof. Nagu.
Prof. Nagu pia, ameelekeza upimaji wa maeneo yote ya kutolea huduma za afya na kupata hati ya umiliki wa aridhi ili kuondoa changamoto ya migogoro ya ardhi.

MCHENGERWA: HAKUNA FURSA KWA WANAFUNZI KUBADILI SHULE WALIZOPANGIWA
Na. James K. Mwanamyoto OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kuwa, uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo umefanyika kwa kuzingatia ufaulu na nafasi zilizopo, hivyo hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yoyote ya shule kutokana na ukosefu wa nafasi za kufanya mabadiliko hayo.
Waziri Mchengerwa amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi kwa mwaka 2025.
Waziri Mchengerwa amesema jumla ya wanafunzi 214,141 wakiwemo wasichana 97,517 na wavulana 116,624 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi ikijumuisha wanafunzi 1,028 wenye mahitaji maalum
“Muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano utaanza tarehe 08 Julai, 2025, waliopangwa wanapaswa kuanza kuripoti shuleni kuanzia tarehe 06 Julai, 2025 na siku ya mwisho ya kuripoti ni tarehe 21 Julai, 2025, na waliopangwa kwenye Vyuo vya Elimu ya Ufundi watapokea maelekezo ya namna ya kujiunga kutoka katika vyuo walivyopangiwa,” Mhe. MChengerwa amesisitiza.
Akizungumzia ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja, Mhe. Mchengerwa ameainisha kuwa, watahiniwa 223,372 (41.23%) walipata ufaulu wa Daraja la I – III, hali inayoonesha kuwa ufaulu wa watahiniwa wa mwaka 2024 umeongezeka kwa asilimia 5.36% ikilinganishwa na ufaulu wa Daraja la I – III wa watahiniwa 198,394 (35.87%) wa mwaka 2023.
Aidha, Waziri Mchengerwa amewapongeza wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi na kuwahimiza kuendelea kufanya bidii katika kujifunza ili waweze kufanikiwa kujiunga na mafunzo ya Elimu ya Juu baada ya kuhitimu Kidato cha Sita na Vyuo vya Elimu ya Ufundi.
Sanjari na hilo, Mhe. Mchengerwa amewapongeza walimu, wazazi na walezi wote kwa juhudi walizozifanya katika malezi na ufundishaji hali iliyowezesha wanafunzi kufaulu vizuri, na amewataka kuendelea kuwa na moyo wa kusimamia na kufuatilia maendeleo ya watoto shuleni.
Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga na Kidato cha Tano katika Shule za Sekondari na Vyuo vya Elimu ya Ufundi vya Serikali umefanyika kwa kuzingatia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023 na Mtaala ulioboreshwa, hivyo wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka Shule za Serikali, zisizo za Serikali na watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.

RC SERUKAMBA AMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA KWA KUIPA IRINGA UWENYEJI WA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025
OR-TAMISEMI
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Peter Serukamba, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuiamini na kuipa heshima Mkoa wa Iringa kuwa mwenyeji wa mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA kwa mwaka 2025.
Akizungumza leo, Juni 6, 2025, na waandishi wa habari mjini Iringa, RC Serukamba aliwahamasisha wananchi kuwapokea kwa moyo wa ukarimu wageni wanaoendelea kuwasili kushiriki mashindano hayo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani.
"Hili ni tukio muhimu sana kwa Mkoa wa Iringa, kwa kuwa ni mara ya kwanza baada ya mashindano haya kufanyika kwa mfululizo mkoani Tabora hadi mwaka 2024. Tunamshukuru sana Mhe. Rais kwa heshima hii ya kipekee," alisema RC Serukamba.
Aidha, alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia ufunguzi rasmi wa mashindano hayo utakaofanyika tarehe 09 Juni 2025, ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb).
Mashindano ya UMITASHUMTA yamepangwa kuanza rasmi tarehe 08 Juni 2025 hadi 17 Juni 2025, yakifuatiwa na UMISSETA yatakayodumu kuanzia 08 Juni hadi 30 Juni 2025.
Kwa mwaka huu, mashindano hayo yanatarajiwa kuvutia zaidi ya washiriki 10,000 wakiwemo wanafunzi, walimu wa michezo, maafisa pamoja na viongozi kutoka sekta mbalimbali za michezo nchini.
Michezo itakayoshindaniwa ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, mpira wa netiboli, mchezo wa kengele kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kuona, pamoja na burudani ya muziki wa kizazi kipya.
Mashindano haya yatafanyika katika shule na viwanja mbalimbali ndani ya Mkoa wa Iringa, vikiwemo Shule ya Sekondari Wasichana Iringa, Shule ya Lugalo na Ualimu kleruu.

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI – PROF. NAGU
OR-TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Prof. Tumaini Nagu, amesema kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kutoa suluhisho la kudumu kwa changamoto zinazowakabili wananchi, hususan katika sekta ya afya.
Prof. Nagu ametoa kauli hiyo alipotembelea mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Muhoro, kilichopo katika Halmashauri ya Mji wa Rufiji, mkoani Pwani, ambacho kimekuwa kikikumbwa na tatizo la mafuriko ya mara kwa mara.
> “Kituo chetu cha sasa cha Muhoro kimekuwa na changamoto ya mafuriko kila mara. Ili kukabiliana na hali hiyo, Serikali imeamua kujenga kituo kipya katika eneo ambalo halifikiwi na maji kwa urahisi. Hii ni hatua ya kutoa suluhisho la kudumu kwa wananchi wa Kata ya Muhoro na maeneo ya jirani,” alisema Prof. Nagu.
Aliongeza kuwa Serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 700 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo hicho, ambacho kinatarajiwa kuanza kutoa huduma ifikapo mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.
Aidha, Prof. Nagu amewataka watumishi wa afya wa kituo hicho kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi mara tu kituo kitakapokamilika, kama ilivyo dhamira ya Serikali ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi na weledi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Rufiji, Bw. Simon Berege, amesema kukamilika kwa kituo hicho kutakuwa ni msaada mkubwa si kwa wakazi wa Kata ya Muhoro pekee, bali pia kwa wananchi kutoka maeneo mengine ya halmashauri hiyo, pamoja na baadhi ya wananchi kutoka mkoa jirani wa Lindi.

WALIMU NCHINI WATAKIWA KUTUMIA TAALUMA ZAO KULETA MAPINDUZI YA KIMAENDELEO
Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amewataka walimu wote nchini kuhakikisha wanatumia taaluma na weledi wao katika kufundisha na kuleta mapinduzi ya kimaendeleo na fikra kwa jamii ya watanzania.
Mhe. Katimba ametoa maelekezo hayo leo Juni 05,2025 Jijini Arusha kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Chengerwa wakati akizindua zoezi la ugawaji wa vifaa vya TEHAMA katika shule za Sekondari nchini kupitia Programu ya Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP).
“Niwaase walimu muendelee kufanya kazi kwa bidii, kuendana na mabadiliko ya Kisera yanayoendelea kufanyika katika siku za karibuni ikiwemo kutekeleza vema mtaala ulioboreshwa, ni muhimu kujituma na kuhakikisha tafsiri ya mitaala na sera ya elimu inafanyika kwa vitendo.” Amesema Katimba.
Katika kusisitiza hilo Mhe. Katimba amesema jamii ya kitanzania inamtazama mwalimu katika hatua zote za mabadiliko ya mwanafunzi hasa katika ulimwengu wa TEHAMA ambao kwa sasa unashika kasi ulimwenguni.
Aidha, ameongeza kuwa Ofisi ya Rais - TAMISEMI itaendelea kushirikiana na Wizara za kisekta na Wizara Mtambuka ili haki na maslahi ya walimu yapatikane, kulindwa na kuhakikisha wanafanya kazi katika mazingira tulivu yaliyoboreshwa na kupata huduma kwa upendo.
Kwa upande wake Joseph Mkude, Mkuu wa wilaya ya Arusha akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema matumizi ya TEHAMA kwa wanafunzi yatakwenda kuongeza uelewa na ufaulu kwa wanafunzi.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Dkt. Selemani Shindika amesema vifaa hivyo vinavyogawiwa vinagarimu kiasi cha shilingi bilioni 12 na vitagawiwa kwa shule 422 za Sekondari ili kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji kwa njia ya kisasa kwa kutumia TEHAMA ili kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia Duniani.

WAGANGA WAKUU WA MIKOA HAKIKISHENI HOSPITALI ZA WILAYA ZINALEA VITUO VYA AFYA – Prof. NAGU
OR-TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia afya Prof. Tumaini Nagu amewaelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa (RMO`S) Kuhakikisha hospitali zote za Wilaya nchini zinalea vituo vilivyopo chini yao ili kufanikisha upatikani wa huduma bora za afya kwenye vituo vyote vya ngazi ya afya Msingi.
Prof. Nagu ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani yenye lengo la kuangalia upatikanaji wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa jamii katika Mkoa huo.
“Waganga Wakuu wa Mikoa wote hakikisheni huduma bora zinazotolewa katika hospitali za Wilaya, vivyo hivyo hospitali hizo zilee vituo vya afya vilivyopo chini yake navyo viweze kutoa huduma bora na vituo vya afya vitalea zahanati za maeneo husika” amesisitiza Prof. Nagu.
Aidha, Prof. Nagu amewapongeza watumishi wa hospitali ya Wilaya ya Mkuranga kwa uhamasishaji mkubwa kwa wananchi kushiriki katika uchangia mkubwa wa damu na kufanya kuwe na hazina ya kutosha ya damu.
“Tumeona kuna damu nyingi kwenye majokofu yenu ya kuhifadhia damu na kuna utunzaji mzuri, pia katika maabara yenu kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wananchi kuchangia damu, hii imetokana na elimu ambayo mmekuwa mkiitoa kwa wananchi” alisema Prof. Nagu.
Pia, ameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kwa kuwa na maabara bora yenye ithibati ambayo inahakikishia ubora wa majibu ya vipimo hivyo kuwezesha matibabu sahihi.

KRIKETI KUAANZA KUCHEZWA UMITASHUMTA na UMISSETA 2025
OR- TAMISEMI
Jumla ya wanafunzi 3,215 wanatarajiwa kushiriki katika Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA ya mwaka 2025, ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi kuanzia tarehe 7 hadi 30 Juni, mkoani Iringa.
Akizungumza kuhusu maandalizi ya mashindano hayo, Mratibu wa Michezo hiyo, Bw. Yusuf Singo, alisema maandalizi yamekamilika kwa kiwango kikubwa na wachezaji kutoka mikoa mbalimbali wanasubiriwa kuwasili kwa ajili ya kuanza mashindano hayo.
“Mashindano haya ni jukwaa muhimu la kuibua vipaji kwa vijana wetu. Tumejipanga vizuri kuhakikisha yanakwenda kwa mafanikio,” alisema Bw. Singo.
Michezo itakayoshindaniwa ni pamoja na mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana, netiboli, mpira wa wavu, goli, mpira wa miguu maalum kwa watu wenye ulemavu, riadha, tenisi, mpira wa kikapu, mpira wa mikono, sanaa za maonesho, pamoja na nidhamu na usafi.
Kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa mashindano haya, mchezo wa kriketi utaingizwa rasmi. Mikoa itakayoshiriki mchezo huo ni Dodoma, Tanga, Morogoro na Dar es Salaam.
Mashindano haya yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa (Mb), siku ya Jumatatu tarehe 9 Juni, 2025 katika viwanja vya Kichangani, mkoani Iringa.
Mashindano ya UMITASHUMTA (kwa shule za msingi) na UMISSETA (kwa shule za sekondari) ni sehemu muhimu ya kukuza michezo na malezi ya vipaji vya wanafunzi nchini Tanzania.

SERIKALI KUZIFANYIA UKARABATI SHULE KONGWE ZILIZOCHAKAA.
OR – TAMISEMI
Serikali kupitia bajeti yake ya mwaka 2025/2026 inakusudia kuzifanyia ukarabati shule zote kongwe za msingi na sekondari zilizochakaa ili kuzirejesha katika mwonekano wake wa awali.
Kauli hiyo imetolewa leo Juni 04, 2025 bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI (AFYA) Mhe. Dkt. Festo Dugange wakati akijibu maswali ya Waheshimiwa Wabunge katika kipindi cha maswali na majibu kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.
Naibu Waziri Dkt. Dugange amesema tayari OR – TAMISEMI imeianisha shule zote kongwe na chakavu zinazohitaji ukarabati wa haraka na imefanya tathmini ya uhitaji wa fedha kwa ajiri ya ukarabati wa shule hizo awamu kwa awamu.
Amesema katika bajeti ya Serikali ijayo shule zote zilizo ainishwa zimepewa kipaumbele ambapo zitakarabatiwa awamu kwa awamu kulingana na kiasi cha fedha kutoka Serikali Kuu pamoja na upatikanaji wa fedha kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri.

MHE. MCHENGERWA AWAFUNDA WALIMU, AWATAKA KUWA WAZALENDO NA KUZINGATIA MAADILI
Na John Mapepele
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa rai kwa walimu nchini kuwa wazalendo na kuzingatia weledi ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
Mhe. Mchengerwa ametoa rai hiyo kwenye mkutano wa walimu na wadau wa elimu wa Wilaya ya Rufiji uliofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari ya Wasichana Bibi Titi Mohamed, ambapo yeye mwenyewe pia alitunukiwa tuzo ya heshima ya kutambua mchango wake katika Sekta ya Elimu wilayani Rufiji.
"Katika hali ya kawaida Serikali imeboresha mazingira na miundombinu ya sekta ya elimu kilichobaki ni kwa sisi walimu kutanguliza uzalendo ili kuinua kiwango cha elimu katika ngazi zote". Amesisitiza Mhe. Mchengerwa
Aidha, amesisitiza walimu kutambua wajibu wao na kwamba Serikali haitaweza kusita kuwachukulia hatua za kinidhamu Walimu na Maafisa Elimu ambao watakuwa wazembe katika utekelezaji wa majukumu yao.
Katika taarifa ya Wilaya ya Rufiji kwa Mhe. Waziri, iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Rufiji, Bwana Simon Berege, inaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko la wanafunzi wanaohitimu darasa la Saba kutoka 3135 mwaka 2020 hadi wanafunzi 3715 mwaka 2024.
Idadi ya shule za Awali na Msingi zimeongezeka kutoka 48 mwaka 2021 Hadi 63 mwaka 2025 ikiwa ni ongezeko la shule 15 sawa na asilimia 31.3.
Pia vyumba vya madarasa vimeongezeka kutoka vyumba 377 mwaka2921 hadi vyumba 566 mwaka 2025 ikiwa ni ongezeko la vyumba vya madarasa 189 sawa na asilimia 50. 1
Aidha, katika mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa, Halmashauri ya Mji wa Rufiji imefanikiwa kushinda kwa nafasi ya kwanza katika michezo ya mpira wa miguu, pete na riadha huku ikishika nafasi ya pili kwenye mpira wa mikono hivyo kushika nafasi ya pili ya ujumla katika mashindano hayo.
Katika mkutano huo Mhe.Waziri Mchengerwa alikabidhi makombe hayo kwa shule na baadaye kupokea msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na Benki ya CRDB.

UPATIKANAJI WA DAWA NGAZI YA AFYA MSINGI WARIDHISHA – PROF. NAGU
OR-TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Prof. Tumaini Nagu, amesema hali ya upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi nchini ni ya kuridhisha.
Prof. Nagu ametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi katika Hospitali ya Wilaya ya Chalinze, mkoani Pwani, yenye lengo la kukagua hali ya upatikanaji wa huduma za afya, lishe na ustawi wa jamii.
“Tumejionea wenyewe kuwa upatikanaji wa dawa katika kituo hiki ni wa kiwango cha juu, na hali hii siyo hapa pekee bali ni katika vituo vingi nchini. Kwa sasa tupo kwenye wastani wa asilimia 85 ya upatikanaji wa dawa katika ngazi ya afya ya msingi,” alisema Prof. Nagu.
Ameeleza kuwa mafanikio haya yametokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye kila mwezi hutenga zaidi ya shilingi bilioni 16.6 kwa ajili ya ununuzi wa dawa.
Prof. Nagu amevitaka vituo vyote vya afya kuhakikisha vinatunza dawa kwa uangalifu na kwa kuzingatia taratibu za kitaalamu ili kuzuia upotevu au uharibifu.
Aidha, amewahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya kwa Wote, ili kuhakikisha wanapata huduma za afya kwa urahisi mahali popote nchini pindi wanapokumbwa na changamoto za kiafya.

TAMISEMI yawanoa maafisa kusimamia na kuendesha miradi ya maendeleo kuelekea utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2025/2026
OR – TAMISEMI.
Ofisi ya Rais – TAMISEMI imewakutanisha Makatibu Tawala Wasaidizi Sehemu za Mipango Uratibu, Uchumi na Uzalishaji, Wakuu wa Idara za mipango na uratibu na waweka hazina wa Halmashauri katika mafunzo maalum ya pamoja kuhusu uendeshaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Akifungua mafunzo hayo leo June 3, 2025 Jijini Dodoma, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI Bw. Adolf Ndunguru amesema mafunzo hayo ni sehemu ya kuwaandaa vyema maafisa viungo hao muhimu katika utendaji kazi wa Serikali katika Mamlaka za Serikali za Mikoa na Tawala za Mitaa ili kuwa tayari katika utekelezaji wa vipaumbele vya bajeti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Katibu Mkuu Ndunguru ameyataja maeneo yatakayogusiwa katika mafunzo hayo kuwa ni ugharamiaji wa miradi kwa njia mbadala - (AlternativeFinancing), mwongozo wa makampuni mahsusi ya kuanzisha na kusimamia miradi ya vitega uchumi vya Halmashauri (SPV – Special Purpose vehicle), Malipo kwa nijia ya internet banking na ukusanyaji wa Mapato na Usuluhishi wa Kibenki (Revenue collection and Reconciliation).
Awali Mkurugenzi wa Sera na Mipango Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. John Cheyo, amesisitiza umuhimu wa mafunzo hayo kuwa ni pamoja na kujifunza namna bora ya utekelezaji wa masuala kadha mapya ambayo ni sehemu ya ubunifu katika bajeti ya mwaka 2025/2026.

MRADI WA TACTIC KUBORESHA MAZINGIRA YA KUFANYIA BIASHARA MANISPAA YA SINGIDA
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba (Mb) amesema kukamilika kwa utekelezaji wa miradi ya uboreshaji miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) awamu ya pili katika Manispaa ya Singida kutaleta mabadiliko chanya kwenye huduma, manunuzi na mazingira bora ya kufanyia biashara kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wa Mkoa wa Singida.
Mhe. Katimba amebainisha hayo leo Jumatatu Juni 02, 2025, mkoani Singida katika Manispaa ya Singida mara baada ya kushuhudia utiaji saini Mkataba wa ujenzi wa soko la Kimataifa la Vitunguu, ujenzi wa barabara za katikati ya mji na viwandani kilomita 7.52, ujenzi wa mtaro wa maji ya mvua wa kilomita 2.6 pamoja na Ofisi ya uratibu.
Akizungumzia Ujenzi wa soko la vitunguu, Mhe. Katimba amebainisha kwamba jengo litakalojengwa litakuwa la ghorofa mbili, likiwa na maeneo maalum ya kuchambua na kukaushia vitunguu, maduka na vyumba vya huduma za kifedha, likiwa na uwezo wa kuhudumia wafanyabiashara 3000 kwa wakati mmoja, makadirio yakiwa ni kuingiza mapato ya shilingi milioni 505 kwa mwaka tofauti na milioni 300 za sasa zinazotokana na wafanyabiashara 1069 wanaoweza kuhudumiwa na soko la sasa.
Aidha, katika maelezo yake kando ya kupongeza waratibu wa mradi huo kwa kutoa nafasi kwa mkandarasi mzawa, Mhe. Katimba amemuagiza Mkandarasi M/s Sihotech Engeneering Company Limited kukamilisha mradi huo kwa wakati, ili tija ionekane mapema kwa wananchi wanaotarajiwa kuwa wanufaika wa mradi huo.
Amewasihi pia wananchi wa Manispaa ya Singida kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi anayetekeleza mradi huo, pamoja na kutunza miundombinu hiyo pale itakapokamilika ili iweze kuwa na tija iliyokusudiwa kwa muda mrefu zaidi.
Mhe. Katimba ameziagiza Halmashauri zote nchini zenye miradi ya TACTIC kusimamia vyema uendeshaji wa masoko na vituo vya mabasi ili kuzalisha mapato yaliyotarajiwa na Serikali kwa maendeleo ya maeneo yao.

Serikali yatoa Tsh. bilioni 30 kuwezesha ujenzi wa vituo vya afya kata za kimkakati
Serikali imetoa shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa vituo vya afya katika maeneo mbalimbali ya kimkakati kwenye majimbo 120 yaliyoainishwa na waheshimiwa wabunge kupitia bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa leo (June 02, 2025) bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange wakati akijibu maswali ya waheshimiwa wabunge katika kipindi cha maswali na majibu kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.
Akijibu swali la nyongeza la Mhe. Dorothy Kilave mbunge wa jimbo la Temeke aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa na serikali katika kujenga kituo cha afya kata ya Sandali jimbo la Temeke Mhe. Dkt. Dugange amesema licha ya serikali kujenga vituo vya afya katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Temeke lakini itaendelea kutenga fedha ili kuhakikisha kata zote za kimkakati zinakuwa na vituo vya afya.
“Serikali inaendelea kuboresha huduma za afya kote nchini na niwahakikishie waheshimiwa wabunge kuwa hii ni dhamira ya dhati ya serikali kuhakikisha inasogeza huduma za afya karibu na wananchi na itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kujenga vituo vya afya katika kata zote za kimkakati”. alisema Mhe. Dkt. Dugange.
Serikali yatoa Tsh. bilioni 30 kuwezesha ujenzi wa vituo vya afya kata za kimkakati.
Serikali imetoa shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa vituo vya afya katika maeneo mbalimbali kwenye majimbo 120 yaliyoainishwa na waheshimiwa wabunge kupitia bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa leo (June 02, 2025) bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange wakati akijibu maswali ya waheshimiwa wabunge katika kipindi cha maswali na majibu kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.
Akijibu swali la nyongeza la Mhe. Dorothy Kilave mbunge wa jimbo la Temeke aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa na serikali katika kujenga kituo cha afya kata ya Sandali jimbo la Temeke Mhe. Dkt. Dugange amesema licha ya serikali kujenga vituo vya afya katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Temeke lakini itaendelea kutenga fedha ili kuhakikisha kata zote za kimkakati zinakuwa na vituo vya afya.
“Serikali inaendelea kuboresha huduma za afya kote nchini na niwahakikishie waheshimiwa wabunge kuwa hii ni dhamira ya dhati ya serikali kuhakikisha inasogeza huduma za afya karibu na wananchi na itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kujenga vituo vya afya katika kata zote za kimkakati”. alisema Mhe. Dkt. Dugange.

SANAA ZA MICHEZO ZINAPEWA KIPAUMBELE KATIKA UMITASHUMTA & UMISSETA
Ngoma za asili, kwaya na Muziki wa Kizazi kipya (Bongo Flavor) ni sehemu ya fani ambazo zimekuwa zikishindaniwa katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa shule za Msingi na Sekondari (UMITASHUMTA & UMISSETA).
Mratibu wa michezo- TAMISEMI, Yusuph Singo amesema kupitia sanaa, wanafunzi wanapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao katika kucheza ngoma zenye asili ya makabila ya mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar, kuimba nyimbo zenye ujumbe wa kizalendo na kuburudisha kupitia muziki wa kizazi kipya.
Mikoa inayoshiriki UMITASHUMTA & UMISSETA 2025 Mkoani Iringa inatarajiwa kuwa na uwakilishi wa vikundi vya ngoma, kwaya na waimbaji wa muziki wa kizazi kipya kwa ajili ya kushindana na kumpa mshindi wa mashindano ya mwaka huu.
Mashindano hayo yenye kauli mbiu isemayo "Viongozi bora ni msingi wa maendeleo ya Taaluma, Sanaa na Michezo, Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu" yataanza Mei 7 2025 na yanatarajiwa kufunguliwa rasmi Mjini Iringa tarehe 9 Mei 2025 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.
Ofisi ya Rais-TAMISEMI ndio mratibu na msimamizi wa UMITASHUMTA & UMISSETA 2025 ikishirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, na Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo.

UMITASHUMTA & UMISSETA 2025 KUFANYIKA KITAIFA MKOANI IRINGA.
OR-TAMISEMI
Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania UMITASHUMTA na yale ya Shule za Sekondari UMISSETA kwa mwaka 2025 yanatarajiwa kufanyika Mkoani Iringa kuanzia Juni 7,2025.
Mashindano hayo yatajumuisha wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar, yakihusisha michezo mbalimbali kama soka kwa wavulana na Wasichana,Mpira wa kikapu, Netiboli,Wavu na Riadha.
Michezo mingine ni mpira wa Goli ambao ni maalum kwa ajili ya wanafunzi wenye uono hafifu, pamoja na Sanaa za Michezo na Burudani ambayo inahusisha ngoma za asili, kwaya na Muziki wa Kizazi kipya (Bongo Flavor).
Mashindano hayo pia yatajumuisha michezo mingine kwa wanafunzi wenye ulemavu, ikiwepo soka Wasichana na Wavulana pamoja na Riadha.
UMITASHUMTA & UMISSETA 2025 inaratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo.

RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametoa muda wa wiki mbili kwa uongozi wa wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga eneo la kariakoo kuanza kufungua njia ili kuruhushu shughuli za kibiashara kufanyika kwa ufanisi wakati serikali ikielekea kufanya uzinduzi wa soko jipya la Kariakoo
Akizungumza Dar es Salaam Mei 28,2025 na waandishi wa habari RC Chalamila amesema wakati maandalizi ya uzinduzi wa soko jipya yakiendelea ni muhimu Machinga Kariakoo kufungua njia za kuingia ili kupeleka bidhaa kwenye soko jipya la Kariakoo.
"Soko limeshakamilika kwa asilimia 98 hivyo natoa muda wa wiki mbili kuanzia leo Mei 28,2025 Machinga waliopo barabarani Kariakoo wakaondoka kwenda maeneo waliyopangiwa" alisisitiza Chalamila.
Kuhusu wafanyabiashara waliokuwepo kwenye Soko la Kariakoo awali kabla halijaungua Chalamila alisema wote waliokuwepo kuhakikiwa na watarejeshwa kama ambavyo Rais Dkt Samia alivyoelekeza na watapaswa kujaza mikataba,kulipa kodi na kwamba Mkoa huo umefanikiwa kuondoa udalali wa upangishaji maeneo kwa kutuia mfumo wa kidijitali wa TAUSI.
Kwa upande wake Meneja Mkuu Shirika la Masoko Kariakoo Ashraph Abdulkarim alisema Shirika hilo linaendelea kuratibu wafanyabiashara waliokuwepo kurejea kwenye Soko hilo kulingana na mpangilio wa biashara.
Abdulkarim aliongeza kusema idadi ya wafanyabiashara 1150 kati ya 1520 waliohakikiwa tayari wamesajiliwa kwenye mfumo wa TAUSI ili kurejea sokoni na kuwa maeneo mengine ya wazi yaliyobaki yatatangazwa kupitia mfumo huo ili yapate wapangaji wapya.

Vituo vya kulele watoto vyabainika kuendeshwa bila kuwa na miongozo ya Serikali Kigoma.
OR - TAMISEMI
Serikali imetoa wito kwa wamiliki na waendeshaji wa vituo vya malezi na makuzi ya Watoto wadogo mchana kufuata taratibu,kanuni na miongozo ya uanzishwaji na uendeshaji wa vituo hivyo ili kuhakikisha wanatoa huduma bora zinazokidhi viwango ambavyo ni afya bora kwa Watoto,elimu ya awali, maelzi yenye mwitikio, lishe bora, ulinzi na usalama.
Wito huo umetolewa na Mratibu wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto Ofisi ya Rais- TAMISEMI Shabani Muhali, baada ya kubaini baadhi ya vituo vya malezi na makuzi vya kuhudumia watoto wadogo mchana mkoani Kigoma kufanya shughuli za Malezi na Makuzo bila kuwa na miongozo ya serikali ya uanzishaji na uendeshaji wa vituo hivyo.
Akiongea kwa niaba ya timu maalumu ya tathmini na ufuatiliaji shughuli za malezi na makuzi Ofisi ya Rais - TAMISEMI katika ziara maalumu ya ufuatiliaji na tathimini juu ya mwenendo wa utolewaji wa huduma za malezi na makuzi katika vituo hivyo, Shabani amesema timu hiyo imegundua mapungufu mengi ikiwa ni Pamoja na walezi kutokuwa na elimu sahihi ya malezi huku baadhi ya vituo vikiendeshwa bila mwongozo maalum maarufu kama kiongozi cha Mlezi.
Kufuatia hatua hiyo Shabani amesema maelekezo ya serikali ni kuhakikisha vituo vyote vya kutolea hudma za malezi na makuzi kwa Watoto wadogo mchna vinasajiliwa na kuendeshwa kwa kufuata miongozo maalum ili kutimiza dhamira njema ya uanzishwaji wa vituo hivyo.
Timu hiyo imekagua vituo mbalimbali vya kulelea watoto wadogo mchana katika wilaya za Kakonko na Kasulu Mkoani Kigoma na inaendelea na ziara yake Mkoani Mbeya, ikiwa ni kufanya ufuatiliaji na tathmini, na pia kutoa ushauri chanya katika kuboresha huduma za malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.

Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa
Na OR-TAMISEMI, Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI (ELIMU) Mhe. Zainab Katimba amewapokea wageni kutoka Bunge la Taifa la Zambia ambao wamekuja kutembelea na kujifunza jinsi Mfumo wa Serikali za Mitaa unavyotekelezwa Tanzania Bara.
Akiongea na wageni hao ambao ni Waheshimiwa Wabunge la Taifa la Zambia katika ukumbi wa Sokoine TAMISEMI Jijini Dodoma leo tarehe 28 Mei, 2025 kwa niaba ya Mhe. Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Katimba alisema Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ndiyo ina mamlaka mapana na muhimu yakiwepo Uratibu na Usimamizi wa shughuli za Serikali ngazi ya Mikoa na Serikali za Mitaa, kujengea uwezo wa Serikali za Mitaa, uendelezaji na utekelezaji wa Sera, upangaji na ufuatilaji wa fedha za Serikali za Mitaa.
Masula mengine ameyataja kuwa ni usimamizi na utoaji wa huduma hasa elimu, afya, na miundombinu, kukuza ugatuaji wa madaraka na utawala bora pamoja na kuwezesha mahusiano baina ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa na utatuzi wa migogoro katika ngazi ya Halmashauri na ngazi ya msingi pamoja na utoaji wa huduma kwa wananchi.
“majukumu haya ni muhimu katika kuhakikisha maendeleo jumuishi, uboreshaji wa utoaji wa huduma kwa wananchi, na utawala shirikishi – maadili tunayoamini yanashirikishwa katika nchi zetu zote mbili” alisisitiza Mheshimiwa Katimba.
Akiongea kwa niaba ya Waheshimiwa Wabunge wenzake, Mheshimiwa Twaambo Mutinta (Mb), Mkuu wa Msafara na Mwenyekiti wa Kamati ya Serikali za Mitaa, Makazi na Masuala ya Machifu (Chiefs’ Affairs) alishukuru kwa mapokezi mazuri yaliyofanywa na ofisi ya Rais - TAMISEMI na kusema nchini Zambia Mfumo wa Ugatuaji wa Madaraka ulianza mwaka 2016 na hivyo watakuwa na wakati mzuri wa kujifunza hapa Tanzania na kubadilishana ujuzi kwani umuhimu mkubwa unaonekana katika kupeleka rasilimali na maamuzi karibu na wananchi haya yote ni moja ya vitu ambavyo tunatarajia tutashirikishwa katika ziara hii.
Naye Angelista Kihaga Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa Ofisi ya Rais TAMISEMI akiwasilisha mada kwa ugeni huo, amesema Idara ya Serikali za Mitaa ni moja ya idara za Ofisi ya Rais -TAMISEMI ambayo inalo jukumu kubwa la kuratibu na kusimamia kazi za Mamlaka za Serikali za MitaaTanzania Bara. Idara hiyo ina sehemu tatu ambazo ni sehemu ya Usimamizi wa Rasilimali Fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sehemu ya Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sehemu ya Usimamizi wa Utoaji Huduma na Utawala Bora katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Kihaga aliongeza kuwa Halmashauri zinafanya kazi chini ya Mfumo wa Ugatuzi wa Madaraka (Decentralization by Devolution) lakini zinakuwa na uhusiano wa karibu na Serikali Kuu kupitia mwelekeo wa kisera, usaidizi wa kifedha na uangalizi wa kiutawala unaotolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI lakini pia Sekta na wizara nyingine. Serikali kuu inaziongoza Halmashauri katika kupanga mipango na bajeti, utoaji wa huduma na ufuatiliaji wa utendaji wao kupitia Sekretarieti za Mikoa
Halmashauri zinajumuisha timu za Usimamizi wa Halmashauri (CMTs) zikiongozwa na mkurugenzi anayeunda sehemu ya Wataalaam na sehemu nyingine inayoundwa na Waheshimiwa Madiwani ambapo kwa pamoja huunda Baraza. Aidha, kuna Madiwani wa kuchaguliwa kutoka kwenye Kata na kutoka Viti Maalum na Halmashauri kamili ndiyo wanaotoa maamuzi ya mwisho katika baraza hilo.

Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa
Angela Msimbira, Pwani
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Serikali za Mitaa, Bw. Sospeter Mtwale, amefunga rasmi mafunzo ya uongozi kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa, yaliyolenga kuwaongezea maarifa, ujuzi na mbinu bora za kiuongozi kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi katika ngazi za mikoa.
Akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo mkoani Pwani, Bw. Mtwale aliwataka washiriki wa mafunzo kwenda kusimamia kwa weledi na uwajibikaji miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.
“Nendeni mkasimamie miradi ya maendeleo kwa kuchukua hatua stahiki pale mnapoona mambo hayaendi sawa. Ufuatiliaji wa miradi ufanyike kwa pamoja na si kwa upande mmoja pekee,” amesisitiza Mtwale.
Ameongeza kuwa ufuatiliaji wa pamoja huimarisha uelewa wa pamoja miongoni mwa watumishi wa umma, na hivyo kuwezesha matumizi bora ya rasilimali chache zilizopo, hatua inayochochea ufanisi wa utekelezaji wa miradi kwa manufaa ya wananchi.
Bw. Mtwale pia amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi kuwa viongozi wa mfano kwa kujenga ushirikiano kazini na kuimarisha timu za kazi zenye mshikamano.
“Kiongozi bora ni yule anayeweza kuwaunganisha watumishi na kufanya kazi kwa ushirikiano kama timu. Epukeni migogoro inayotokana na maslahi binafsi na gawanyo wa watumishi,” ameongeza.
Amehimiza pia umuhimu wa utoaji wa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia maadili ya kazi na kuepuka ubaguzi wa aina yoyote ikiwemo wa kisiasa, kidini au lugha zisizo na staha.
“Toeni huduma kwa usawa kwa watu wote. Hii ndiyo picha halisi ya Serikali inayowajali wananchi wake,” amesisitiza.
Mafunzo hayo yamewapa washiriki mbinu na nyenzo muhimu kuwa viongozi mahiri, waadilifu na wachapakazi, walioko tayari kutoa huduma bora kwa jamii na kuhakikisha maendeleo ya Taifa yanasimamiwa kikamilifu.

Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu
Na OR – TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya afya Prof. Tumaini Nagu amefanyiwa mapokezi makubwa na Viongozi, menejimenti na watumishi wa ofisi hiyo ambapo ameahidi ushirikiano ili kufikia malengo ya Serikali.
Prof. Nagu ameyasema hayo wakati akiongea na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Adolf Ndunguru, baadhi ya Viongozi, menejimenti na watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI baada ya mapokezi yake katika ofisi za Wizara zilizopo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma na kuomba ushirikiano na kuahidi kufanya kazi kwa pamoja ili kufikia dhamira na maono ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kumwamini na kumteua ili aisimamie Sekta ya Afya hususani Afya ya msingi chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI na amepokea kwa unyenyekevu mkubwa uteuzi wake na kuahidi kushirikiana kwa vitendo lakini anaamini uzoefu huongezeka kila siku na yupo tayari kufanya kazi na Viongozi na watumishi wa ofisi hiyo.
Prof. Nagu afafanua kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa maelekezo yake kwa kusisitiza kuboresha huduma za afya ya msingi, huduma ambazo zinatakiwa kuwafikia wananchi kwa wakati na dhamira yake ni kuyafanya mazingira ya afya kuwa bora, hivyo kama sehemu ya ofisi ambayo anakutana na wazoefu watamsaidia na kushirikiana naye ili kuyafanya hayo kwa vitendokwani kidole kimoja hakivunji chawa.
“lakini naomba itoshe sana kusema nakushukuru Katibu Mkuu (Bw. Adolf Ndunguru) pamoja nanyi nyote ambao mmenipokea siku ya leo, na hii ni ‘surprise’ kubwa, ishara kubwa kwamba mpo tayari kushirikiana nami na hilo ndilo ninaloliomba, tushirikiane ili tuweze kuwatumikia watanzania na yale maono ya Mheshimiwa Rais, basi yakatekelezeke kwa kumuunga mkono Rais wetu” alilisisitiza Prof. Tumaini Nagu
Katibu Mkuu Adolf Ndunguru Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Adolf Ndunguru amemkabidhi Kiongozi huyo Mpango Mkakati wa Taasisi na Muundo wa Ofisi ya Rais TAMISEMI na kusesema kuwa anamjua Naibu Katibu Mkuu (AFYA) Prof. Tumaini Nagu kama mtu mzoefu katika Sekta ya Afya na anaamini kuwa atafanya kazi nzuri na kwamba Ofisi ya Rais TAMISEMI yenye Idara na Vitengo 17 imempokea na itakuwa tayari kupokea maagizo yake na kuyafanyia kazi ili kuweza kufikia malengo na maono ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi. Emma Lyimo akitoa neno kabla ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Adolf Ndunguru katika kikao kifupi cha menejimenti kumkaribisha Prof. Tumaini Nagu, amesema anayo furaha kubwa ya Kiongozi huyo mahiri kujiunga na familia ya Ofisi ya Rais TAMISEMI lakini pia kupata wasaa wa kukutana na kufahamiana na Viongozi, menejimenti na watumishi Ofisi ya Rais TAMISEMI.

MAHUSIANO MAZURI NI NGUZO MUHIMU KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU-MHE.SAJINI
Na Angela Msimbira, Kibaha – Pwani
Mahusiano mazuri kazini yameelezwa kuwa msingi muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya kiserikali katika ngazi mbalimbali.
Hayo yamesemwa leo Mei 26, 2025 na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Jumanne Sajini, alipokuwa akitoa mada kuhusu Muundo wa Serikali, Taratibu za Utendaji kazi Serikalini na Mawasiliano ndani ya Serikali kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa wanaoshiriki mafunzo ya uongozi yanayoendelea Kibaha, mkoani Pwani.
Mhe. Sajini amesema kuwa mahusiano mazuri ya kikazi baina ya viongozi, watumishi na wadau wengine ni msingi wa usimamizi bora wa rasilimali watu na utekelezaji wa mipango ya maendeleo.
“Ni muhimu sana kuwa na mahusiano chanya kazini, kwa sababu nyinyi ndiyo kiungo kati ya Serikali Kuu, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Uhusiano mzuri huleta mshikamano, hurahisisha utekelezaji wa sera, na huongeza ari ya kazi miongoni mwa watumishi,” amesema Mhe. Sajini.
Ameongeza kuwa uongozi wa kisasa unahitaji viongozi waliobobea si tu katika usimamizi wa kazi, bali pia katika kujenga mazingira rafiki ya kazi, yanayozingatia mawasiliano mazuri, heshima na ushirikiano wa karibu.
Mafunzo hayo ambayo yanaendelea kwa siku kadhaa yanalenga kuwaongezea viongozi hao maarifa na mbinu bora za uongozi, ili waweze kusimamia kwa weledi sekta wanazoziongoza, huku wakikuza maendeleo ya kiuchumi, biashara na uwekezaji katika mikoa yao.
Kwa mujibu wa mafunzo hayo, mada mbalimbali zinazotolewa zitawawezesha washiriki kuboresha mbinu za utendaji, kuongeza tija mahala pa kazi, na kujenga utamaduni wa kushirikiana katika kufanikisha malengo ya Serikali.

MAPEPELE AWANOA MAAFISA HABARI WA TAMISEMI, AWATAKA WAWE WAZALENDO
Na Mwandishi Wetu, OR- TAMISEMI
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasilino Serikali na Msemaji Mkuu wa Wizara ya TAMISEMI, John Mapepele ametoa wito kwa Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri zote nchini kutanguliza uzalendo na weledi wakati wa utoaji wa taarifa ili habari hizo ziwe na tija kwa taifa.
Mapepele ametoa wito huo mwisho wa juma wakati akiwasilisha maada kuhusu Mawasilino ya Kimkakati ya Kutangaza Nafanikio ya Sekta za Afya, Elimu na Miundombinu chini ya TAMISEMI kwa Maafisa Habari zaidi ya 200 wa Mikoa na Halmashauri zote nchini jijini Dodoma kwenye kikao kazi cha siku mbili kwa MaafisaHabari hao kilichoratibiwa na Wizara hiyo.
Kikao kazi hicho kilichofunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Mohamed Omary Mchengerwa na kufungwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa kimejadili pamoja na mambo mengine, mikakati mbalimbali ya kutangaza mafanikio ya Serikali, pia kuwajengea uwezo Maafisa Habari hao kwa mada mbalimbali za kitaaluma hususan matumuzi ya mifumo ya kidigitali kwenye utoaji wa taarifa na kuja na maazimio kadhaa ya kuboresha utendaji kazi.
Aidha, Mapepele amesema kumekuwa na mafanikio makubwa katika miradi ya maendeleo ambayo imetekelezwa katika mikoa na Halmashauri zote nchini ambayo haijatangazwa ipasavyo na Maafisa Habari katika maeneo hayo na kuwataka kuwa wabunifu wa kutoa taarifa hizo
"Ndugu zangu Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya mapinduzi makubwa kwenye sekta ya miundombinu ambapo tumeshuhudia mabarabara, madaraja, vituo vya mabasi na masoko yakitengenezwa kila uchao, ukiachia mbali madarasa, zahanati, vituo vya afya na vifaa tiba kwenye kila kona hivyo ni wajibu wetu sisi Maafisa Habari wa Halmashauri na Mikoa kuwa wazalendo na kuisemea Serikali yetu ili wananchi waweze kujua na kutumia huduma hizi kikamilifu". Amefafanua Mapepele
Akifungua kikao kazi hicho Mhe. Mchengerwa amewataka Maafisa Habari wote wa TAMISEMI kuhakikisha wananchi wanapata habari sahihi kwa wakati za utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao ya kazi.
"Mmebeba dhamana kubwa ya kuhakikisha wananchi wanapata habari sahihi hivyo msiache watanzania walishwe habari potofu". Amesisitiza Mhe. waziri Mchengerwa
Akifunga kikao kazi hicho, Katibu Mkuu Msigwa ameipongeza Wizara ya TAMISEMI kwa kuratibu kikao kazi hiki ambapo ameshauri kiwe kinafanyika kila mwaka ili kufanya tathmini wa utendaji wa kazi na kujadiliana masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi wa kundi hili kubwa la Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri nchini katika kutoa taarifa za miradi ya maendeleo.
Mara baada ya kumalizika kikao kazi hiki, Maafisa Habari hao walipata fursa ya kutembelea Mji wa Serikali wa Mtumba na kujionea kukamilika kwa Mji huo

SOKO LA KISASA LA NYAMA CHOMA LAZINDULIWA VINGUNGUTI
Na John Mapepele
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe.Mohamed Mchengerwa amezindua soko la kisasa la nyama choma la Kumbilamoto vingunguti, Ilala jijini Dar es Salaam na kushuhudia utiaji wa mikataba ya miradi 6 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 7.7
Mara baada ya kuzindua soko hilo ambalo limegharimu takribani shilingi milioni 727 amepongeza uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kufanikisha mradi huo ambapo amezitaka Halmashauri nyingine kuiga mfano huo.
Aidha, amefafanua kuwa soko hilo litakwenda kuwapatia ajira wananchi wengi huku akisisitiza kuendelea kulitunza ili lisiharibike kwenye kipindi kifupi.
Mhe. Mchengerwa ameongeza kuwa kukamilika kwa soko hilo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kufafanua kuwa Serikali ya awamu ya sita tayari imekamilisha miradi mingi kama iilivyoahidi.
Wakati huo huo Waziri Mchengerwa amezitaka Halmashauri zote nchini kutimiza malengo zilizojiwekea ya ukusanyaji mapato ili ziweze kutekeleza miradi ya maendeleo huku akizitaka kuendelea kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo yenye tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Akizungumzia kuhusu wakandarasi wazawa, Mhe Mchengerwa amezitaka Halmashauri na mikoa yote nchini kuwapa kipaumbele wakandarasi wazawa huku akitoa wito kuwachukulia hatua wakandarasi wanaofanya vibaya katika kazi wanazopewa.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogole amemhakikishia Mhe. Mchengerwa kuwa mikataba yote iliyosainiwa inakwenda kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka na kwamba wananchi watakwenda kunufaika na miradi hiyo.
Katika uzinduzi wa soko hilo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Zungu ambaye pia ni Mbunge wa Ilala amewataka watanzania kutojihusisha na uvunjaji wa amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu
Bi. Amina Selemani ambaye ni miongoni mwa mfanyabiashara katika soko hilo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kutoa fedha za kujenga soko hilo ambalo limetoa ajira kwa akina mama wengi.
“Kwa kweli tunamshukuru Mheshimiwa Rais wetu kwa upendo huu wa kutuletea mradi huu wa soko ambao umekuwa ni ukombozi kwa maisha yetu”. Amefafanua Amina

DKT. Biteko asisitiza wazazi kuthamini nafasi ya familia katika malezi na makuzi ya mtoto.
OR – TAMISEMI
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, ameitaka jamii kuthamini nafasi ya familia katika makuzi na malezi ya mtoto, kama hatua ya msingi katika kudhibiti vitendo vya watoto kukimbia familia zao na kuwa watoto wa mitaani.
Naibu Waziri Mkuu Dkt. Biteko ametoa agizo hilo leo Mei 24, 2025, katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia na kilele cha Kongamano la Malezi lililofanyika jijini Mwanza.
Ameeleza kuwa ni muhimu kuzingatia malezi bora ya mtoto tangu akiwa tumboni kwa mama hadi anapofikia umri wa miaka 18, na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekuwa ikitekeleza Programu Jumuishi za Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kwa kipindi cha 2021 hadi 2026.
Dkt. Biteko amezindua Mwongozo wa taifa wa uanzishaji na uendeshaji wa vikundi vya wazazi vya malezi na matunzo ya mtoto, na mwongozo wa Watoto kwa muktadha wa dini ya Kikristo na Kiislamu pamoja na kuzindua kampeni maalum ya malezi kwa Watoto.

Mhe. Rais Samia amtaka Prof. Nagu kuboresha huduma ya afya ya msingi.
Na John Mapepele
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtaka Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia eneo la Afya katika Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Prof. Tumaini Nagu kuhakikisha kwamba huduma ya afya ya msingi inaboreshwa kwa wananchi.
Mhe. Rais ametoa maelekezo hayo leo, Mei 24, 2025 Ikulu ya Dar es Salaam mara baada ya kumuapisha kushika washifa huu baada ya kumteua hivi karibuni.
Mhe. Rais amefafanua kwamba tayari Serikali imeshafanya maboresho makubwa katika eneo hili kazi iliyobaki ni kuendelea kusimamia kikamilifu ili kuimarisha eneo hili.
" Toka mwaka 2020 Serikali imefanya mambo makubwa katika eneo hili kuanzia kwenye ukarabati wa zahanati kongwe, vituo vya afya, ongezeko la vifaa tiba na wataalam". Amesisitiza Mhe. Rais
Pia Mhe.Rais amemtaka Profesa Nagu kwa kushirikiana na viongozi atakaowakuta kwenda kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi kwenye sekta hiyo muhimu kwa taifa letu.
Aidha, amemtaka katika utendaji wa kazi kupunguza urasimu huku akizingatia miongozo, sheria na kanuni katika utendaji wa kazi.
Katika uapisho huo, Waziri wa Ofisi ya Rais- TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa, Katibu Mkuu, Adolf Ndunguru na Watendaji kadhaa wa Wizara pia wameshiriki.

MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI
Na. James K. Mwanamyoto OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Maafisa Habari Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Seriksali za Mitaa kuhakikisha wananchi wanapata habari sahihi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao ya kazi.
Waziri Mchengerwa ametoa wito huo leo, wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Habari wa Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi za Ofisi ya Rais-TAMISEMI kinachofanyika katika Ukumbi wa Jiji la Dodoma uliopo kwenye Mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma.
“Mmebeba dhamana kubwa ya kuhakikisha wananchi wanapata habari sahihi hivyo msiwaache watanzania walishwe habari potofu” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Mhe. Mchengerwa amesema kuwa, Maafisa Habari nchini ni rasilimaliwatu muhimu hivyo wakitambua wajibu wao na kujiimarisha kiutendaji ni wazi kuwa wananchi watapata taarifa sahihi kwa wakati.
“Iwapo kila mmoja wenu akiwa mzalendo na kutambua wajibu wake, habari mtakazozitoa ndio zitaaminiwa na kupokelewa na watanzania kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ambayo imeshamiri hivisasa,” Waziri Mchengerwa amehimiza.
Waziri mchengerwa amesema, ana amini kwamba maafisa habari waliopo wana weledi na ujuzi unaowawezesha kutoa taarifa sahihi zenye tija kwa wananchi na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Sanjari na hilo, Waziri Mchengerwa ameelekeza Maafisa Habari wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa washiriki kwenye ziara za viongozi ili wapate uelewa utakaowawezesha kutangaza kwa ufanisi mafanikio ya Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Aidha, Waziri Mchengerwa amewaelekeza waajiri katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha Maafisa Habari wanaokaimu ukuu wa vitengo ambao wana sifa, wapewe vitengo ili waweze kutekeleza kikamilifu jukumu la kuuhabarisha umma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya taasisi zao ikiwa ni pamoja na kutangaza mafanikio yaliyopatikana kwenye eneo la utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambalo limepewa kipaumbele na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo
OR-TAMISEMI
Serikali kupitia Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) imefanikiwa kuanzisha vituo 206 vya kijamii vya kulelea watoto wadogo mchana na kusajili vituo binafsi 4,178 nchi nzima tangu mwaka 2021.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Husein Mtanda, amesema vituo hivyo vinahudumia jumla ya watoto 11,675 huku vya binafsi vikihudumia watoto 6,154.
Aidha, jumla ya walezi 445 wamepatiwa mafunzo ya malezi na makuzi ili kuhakikisha utoaji bora wa huduma katika vituo hivyo. Mtanda alisisitiza kuwa uwekezaji katika malezi ya awali ni msingi wa kukuza rasilimali watu yenye tija kwa familia na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Bw. Sebastian Kitiku, amesema mkutano wa tathmini wa siku mbili unawaleta pamoja Maafisa Lishe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na wadau wa maendeleo ili kujadili mafanikio na changamoto za utekelezaji wa programu hiyo.
Naye, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ustawi wa Jamii, Bi. Subisya Kabuje, amesisitiza kuwa washiriki wa mkutano huo wamejipanga kuibua njia bora za kuimarisha utekelezaji wa PJT-MMMAM.

SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI
OR-TAMISEMI
Serikali imethibitisha kuwa inaendelea na hatua za awali kuelekea ujenzi wa daraja la kudumu linalounganisha Kijiji cha Negero katika Wilaya ya Kilindi, mkoani Tanga, ili kuboresha miundombinu na kuchochea shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo.
Akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kilindi, Mhe. Omar Mohamed Kigua, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba, amesema serikali tayari imeshakamilisha usanifu wa daraja hilo, ambao uligharimu shilingi milioni 70 na kukamilika mwezi Machi 2025.
“Serikali inatambua umuhimu wa daraja hili kwa maendeleo ya wananchi wa Kijiji cha Negero. Hivi sasa tupo kwenye hatua ya kupitia taarifa ya usanifu ili kupata gharama halisi za ujenzi. Baada ya hatua hiyo kukamilika, daraja litaombewa fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wake,” alisema Mhe. Katimba wakati akihutubia Bunge Jijini Dodoma.
Kwa sasa, wananchi wa eneo hilo wanategemea kivuko cha chuma kwa waenda kwa miguu (Pedestrian Suspension Bridge) chenye urefu wa mita 100, kilichojengwa na kukamilika mwezi Desemba 2021 kwa gharama ya shilingi milioni 66.68, ili kuwasaidia kuvuka Mto Negero kwa urahisi.
Mhe. Katimba aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja hususan katika maeneo ya vijijini ili kurahisisha usafiri na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi.

MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Mei 20, 2025 ameshiriki kwenye zoezi la kuboresha taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Ikwiriri - Rufiji.
Mara baada ya kuboresha taarifa zake, Mhe. Mchengerwa amewataka wananchi kote nchini kutumia muda wa siku mbili zilizobaki kuboresha taarifa zao.
" Naomba kutoa wito kwa wananchi kwenda kuboresha taarifa zao katika kipindi hiki kifupi cha siku mbili ili waweze kupata haki yao ya msingi ya kupiga kura kwa maendeleo ya taifa letu" amesisitiza Mhe waziri
Aidha, amefafanua kuwa zoezi la kuboresha taarifa ni la muhimu kwa kuwa taarifa hizo zinaweza pia kutumika na Serikali ili kuleta maendeleo.
Pia Waziri Mchengerwa ametoa wito kwa watanzania kutumia vizuri hali yao ya kupiga kura wakati utakapofika.

Msovela: Fanyeni Kazi Kama Timu Kuleta Maendeleo
Na Angela Msimbira, Pwani
Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Albert Msovela, amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ushirikiano na mshikamano ili kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mikoa yao.
Akizungumza leo Mei 20, 2025, katika mafunzo ya uongozi kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa yanayofanyika katika Chuo cha Uongozi mkoani Pwani, Msovela amesema kuwa ushirikiano ni nguzo muhimu katika kufanikisha malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuwaletea wananchi maendeleo ya haraka na yenye tija.
“Ni muhimu tufanye kazi kama timu moja. Miradi ya maendeleo haiwezi kutekelezwa kwa ufanisi ikiwa kila mmoja atafanya kazi kivyake. Ushirikiano, mawasiliano na uwajibikaji ni mambo ya msingi,” amesisitiza Msovela.
Aidha, ameongeza kuwa Makatibu Tawala Wasaidizi wanapaswa kuratibu kwa ufanisi shughuli zote za maendeleo, kufuatilia utekelezaji wake kwa karibu, na kutoa taarifa sahihi kwa wakati ili kusaidia serikali kufanya maamuzi yenye tija.
Msovela amesema viongozi hao ni kiungo muhimu kati ya wananchi na Serikali, hivyo ni lazima wawe karibu na wananchi, kusikiliza changamoto zao na kushirikiana nao katika kuzitafutia suluhisho la kudumu.

SERIKALI KUKAMILISHA UJENZI WA VITUO VYA AFYA.
OR-TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange amesema Serikali itaendelea kutenga na kupeleka fedha kwenye halmashauri zote nchini kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya vituo vya afya ili viweze kutoa huduma stahiki kwa wananchi.
Mhe.Dkt. Duagange ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki aliyetaka kujua
lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Mwasayi ambacho kimepelekewa vifaa tiba lakini hakina majengo ya kutosha.”
“Mheshimiwa Spika, Kituo cha afya Mwasayi kilianza kutoa huduma katika ngazi ya zahanati mwaka 1962 na kupandishwa hadhi mwaka 1977 na kuanza kutoa huduma ngazi ya kituo cha afya.
Aidha, majengo ya kituo hiki ni machache na chakavu.”
Amesema, katika mwaka wa fedha 2024/25, Serikali imetenga shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wazazi na jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya Mwasayi.

MAKATIBU TAWALA WASAIDIZI WAPEWA SOMO USIMAMIZI WA MIRADI NA USULUHISHI WA AKAUNTI
Angela Msimbira, PWANI
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Sospeter Mtwale, amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa kuhakikisha wanazisimamia Halmashauri zote kufanya usuluhishi wa akaunti za kibenki, hususani tunapoelekea mwishoni mwa mwaka wa fedha wa Serikali.
Akizungumza leo Mei 19, 2025 katika ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa yanayofanyika mkoani Pwani, Mtwale amesema bado kuna baadhi ya Halmashauri ambazo zimekuwa na akaunti ambazo hazijafanyiwa usuluhishi kwa muda mrefu, hali inayokwamisha uwajibikaji na utawala bora wa fedha za umma.
“Mikoa ni taasisi wezeshi. Hakikisheni kuwa mnazisimamia Halmashauri zilizo chini yenu kuhakikisha usuluhishi wa akaunti unafanyika kikamilifu kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha,” amesisitiza.
Aidha, amewakumbusha viongozi hao wajibu wao wa msingi katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali katika maeneo mbalimbali ya mikoa, akiwataka kuhakikisha miradi hiyo inakidhi viwango na kuendana na thamani ya fedha inayotolewa na serikali.
Katika hatua nyingine, ametoa wito kwa Makatibu Tawala Wasaidizi kushirikiana kikamilifu katika kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa wakati na kwa weledi, ili kupunguza idadi ya hoja za ukaguzi zinazojitokeza kila mwaka.
“Serikali ina sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya usimamizi wa rasilimali watu na fedha. Ikiwa viongozi mtaisimamia kikamilifu, hoja za ukaguzi zitapungua kwa kiasi kikubwa. Nendeni mkalisimamie hili kwa umakini mkubwa,” amesisitiza.
Mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa serikali kupitia Taasisi ya Uongozi na Ofisi ya Rais – TAMISEMI wa kuimarisha uwezo wa viongozi wa ngazi ya mikoa katika kusimamia utekelezaji wa sera na miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.

Mhandisi Mativila aridhishwa Utekelezaji wa Miradi ya Barabara ya Mtili-Ifwagi na Sawala-Iyegeya
Iringa
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila ametembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa barabara za Mtili–Ifwagi na Sawala-Iyegeya, ambapo ameonesha kuridhishwa na miradi hiyo.
Barabara hizo zinazojengwa na TARURA kwa lengo la kurahisisha usafirishaji wa mazao ya chai, misitu, mbogamboga na mazao mengine kufika sokoni kwa wakati.
Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana huku akitoa wito kwa wakandarasi kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia muda uliopangwa.
Wananchi nao wametoa pongezi kwa serikali kwa kuwaletea maendeleo yanayoonekana na yanayogusa maisha yao ya kila siku.
Barabara hizo zinatarajiwa kurahisisha usafiri, kukuza biashara na kuongeza upatikanaji wa huduma muhimu kama afya na elimu katika maeneo ya vijijini.

Serikali kutumilia Bilioni 208.9 kuwezesha kaya duni laki mbili na elfu 60 kwa miaka sita
OR – TAMISEMI
Serikali inakusudia kutumia Dola milioni 77.4 sawa na shilingi Bilioni 208.9 kuzijengea uwezo kaya duni laki mbili na elfu 60 za wakulima na wavuvi kwa kuziwezesha kitaalam na kuziunganisha na taasisi za kifedha hususani TADB kwa muda wa miaka sita mfululizo ili ziweze kujiimarisha kiuchumi kupitia uzalishaji wa mazao ya uvuvi na kilimo.
Kaya hizo ambazo ni sawa na watanzania milioni moja na laki tatu waliopo kwenye Mikoa 11 ya Tanzania Bara zinajengewa uwezo kupitia Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) katika mradi unaolenga kuimarisha Mifumo jumuishi ya usalama wa chakula na lishe kwenye Halmashauri 41 zinazounda mMikoa hiyo.
Ili kuwezesha utekelezaji chanya wa programu ya AFDP, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu ambayo inaratibu programu hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI ambao ni watekelezaji imewakutanisha Makatibu Tawala wa Mikoa yote 11, pamoja na maafisa viungo kwenye halmashauri husika ili kujenga uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa programu hiyo.
Akifungua kikao kazi hicho kinachoendelea mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Bi. Beatrice Kimoleta, amewasisitiza watendaji hao kusimamia kikamilifu pesa zote zitakazotolewa kwa lengo la kuwezesha utekelezaji wa mradi akikemea ubadilishwaji wa matumizi ya pesa za miradi.
“Hapa naomba nisisitize hizi pesa zisitumike kinyume na taratibu zilizoelekezwa katika utekelezaji wa programu hii, Serikali inahitaji kuona matokeo chanya kama yanavyolengwa na programu, isitokee mkabadilisha hata shilingi ya matumizi ya pesa hizi, kufanya hivyo itakuwa ni kama dhuluma kwa walengwa, na sitarajii mtu yeyote kubadilisha matumizi” alisema Bi. Kimoleta.
Awali akitoa taarifa ya Programu hiyo Bw. Salimu Mwinjaka ambaye ni mratibu wa programu ya AFDP ameitaja mikoa itakayonufaika na programu hiyo kuwa ni Morogoro, Manyara, Singida, Dodoma, Tabora, Mwanza, Lindi, Pwani, Shinyanga, Geita na Tanga.
Aidha amesema tamati ya programu ya AFDP Serikali inatamani kuona ikiwa na meli zake za uvuvi katika bahari ya hindi, wananchi upande wa visiwani Zanzibar kunufaika na uwepo wa zao la mwani, upotevu wa mazao ya samaki kupungua, uwepo wa mbegu bora za mahindi, alizeti na mimea mingine jamii ya kunde pamoja na kuanzishwa kwa viwanda vya kutengeneza chakula cha samaki, hatua itakayowezesha uwepo wa vifaranga vya samaki vyenye ubora.

Naibu Katibu Mkuu Mwambene aendesha kikao kazi kati ya Serikali na Umoja wa Ulaya
Na OR – TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Atupele Mwambene akimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. Adolf Ndunguru kama Mwenyekiti wa Kamati Tendaji, amefungua na kuendesha kikao kazi cha Kamati Tendaji ya Mradi wa Green and Smart Cities Programme ambacho awali kilipokea taarifa ya utekelezaji wa kazi zinazoendelea na zitatolewa maamuzi katika kikao cha mwisho kinachotarajiwa kufanyika tarehe 14 Julai, 2025.
Kwa upande wa Wadau wa Maendeleo Mwenyekiti mwenza Bw. Marc Stalmans Mkuu wa ushirikiano wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya kwa Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki ameshiriki kikao hicho na kufurahia mipango na makubaliano baina ya Umoja wa Ulaya na Serikali ya Tanzania.
Aidha, kikao hicho kimepitisha masuala ya utekelezaji wa Mradi wa Green and Smart Cities kwa kuidhinisha Serikali ya Denmark kujiunga na Mradi huo ambapo Shilingi Bilioni 56 zinatarajiwa kupokelewa Serikalini, kuidhinisha matumizi ya fedha za mkopo wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Shilingi Bilioni 189 na kuielekeza timu ya utekelezaji iweze kuongeza kasi ya utekelezaji wa Mradi.
Kikao hiki cha Kamati Tendaji kimewahusisha Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Fedha, Wizara ya Maji, Makatibu Tawala wa Mikoa ya Tanga na Mwanza, Watendaji kutoka Ofisi za Serikali zilizohudhuria, Wawakilishi kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, mashirikia na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.

SERIKALI ITAENDELEA KUTENGA BAJETI KWA AJILI YA UNUNUZI WA MAGARI YA WAGONJWA.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa magari ya wagonjwa kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya nchini.
Mhe. Katimba ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Minza Simon Mjika, katika kipindi cha Maswali na Majibu aliyeuliza “Je, lini Serikali itapeleka Magari ya Wagonjwa katika Vituo vya Afya Ilamba Ndogo na Mwasengela - Meatu.?”
“katika mwaka 2023/24 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu imepokea magari 3 ya kubebea wagonjwa na kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Meatu, ambapo magari mawili ya kubebea wagonjwa ya Kituo cha Afya Iramba ndogo na Kituo cha Afya Mwansengela yameachwa katika hospitali ya Wilaya ya Meatu kwa muda”
Amesema Magari hayo yatapelekwa kwenye vituo hivyo pindi majengo ya kutolea huduma za upasuaji wa dharura yatakapokamilika magari.
Amesema Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya za dharura na rufaa kwa kununua magari ya wagonjwa na kuyapeleka katika vituo vya huduma za afya.

Watumishi wa Soko la Kariakoo Wapatiwa Mafunzo ya afya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi, amewataka watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo kujenga utamaduni wa kupima afya angalau mara moja kwa mwaka.
Prof. Janabi alitoa ushauri huo alipokuwa akizungumza wakati wa mafunzo ya siku moja kwa watumishi wa shirika hilo yaliyofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jana Mei 9, 2025.
Katika mada yake kuhusu ugonjwa wa kiarusi, alieleza kuwa mtindo mbaya wa maisha, shinikizo la juu la damu, unywaji pombe kupita kiasi, na ulaji wa vyakula vyenye sukari na mafuta mengi ni sababu kuu zinazochangia ugonjwa huo.
"Ni muhimu kufanya uchunguzi wa afya zenu kila mwaka ili kuepuka kugundua magonjwa mkiwa katika hatua za mwisho au uzeeni, hali ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa kwa afya zenu," alisisitiza Prof. Janabi ambaye ni mtaalamu bingwa wa magonjwa ya moyo.
Prof.Janabi aliongeza kuwa dunia inakabiliwa na magonjwa mengi hatari kama vile moyo, shinikizo la damu, kisukari, figo, na kiarusi, ambayo yanasababisha vifo vingi. Hivyo, upimaji wa afya wa mapema ni muhimu ili kujua dalili na kupata matibabu stahiki.
Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, CPA. Ashraph Abdulkarim, alieleza kuwa shirika limeandaa mafunzo hayo kama sehemu ya mkakati wa kuwajengea uwezo watumishi wake ili waweze kufahamu hali zao za afya na kuchukua hatua za mapema kudhibiti magonjwa.
CPA Abdulkarim alishukuru Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kutoa mafunzo kwa watumishi 35 ambao wana jukumu muhimu la kuhudumia wafanyabiashara na wananchi katika soko hilo.
Katika mada nyingine, Dkt. Garvin Kweka aliwaasa watumishi kuwa waaminifu kwa wenzi wao na kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI kwa kuepuka ngono zembe na matumizi mabaya ya vileo.
Naye Afisa Mwelimishaji kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Ilala, Bi. Mary Mwakyusa, aliwaonya watumishi dhidi ya vitendo vya rushwa wanapohudumia wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo.

WANANCHI RUFIJI WAMPONGEZA MCHENGERWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
Na. James K. Mwanamyoto OR-TAMISEMI
WANANCHI wa Rufiji mikoani Pwani wameeleza kufurahishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo jimboni humo ikiwemo ujenzi wa barabara, shule, zahanati na vituo vya afya.
WANANCHI hao pia wamempongeza Mbunge wa Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa jitihada zake za kuhakikisha huduma za jamii zinapatikana kwa uhakika na ubora.
Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya kikazi ya Mwenyekiti wa UWT taifa Mhe. Mary Chatanda aliyoifanya Wilayani Rufiji kwa siku mbili, kwa lengo la kukagua utetelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020/2025.
Mkazi wa ikwiriri Bw. Abdallah Moba amesema jitihada za Mhe. Mchengerwa za kujenga barabara ya Kituo cha Afya Ikwiriri zimewawezesha wananchi kufika kwa urahisi katika kituo hicho ili kupata huduma za afya msingi.
Bi. Mariam Hamza ambaye ni Mama Lishe amesema kuwa, kabla ya barabara ya Kituo cha Afya Ikwiriri kujengwa wateja wake walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya vumbi pindi bodaboda zinapopita, hali iliyopelekea kuwapoteza wateja lakini hivisasa changamoto hiyo imetatuliwa.
Bw. Sirajidini Hassan ambaye pia ni dereva bodaboda ambaye shughuli zake anazifanya nje ya Kituo cha Afya Ikwiriri, amemshukuru Waziri Mchengerwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuijenga barabara hiyo ya Kituo cha Afya Ikwiriri na kuiwekea taa kwani hapo awali watu hususani wanawake walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya kuporwa mali zao kutokana na kiza kilichokuwepo wakati usiku.
Bw. Ramadhan Hamza ambaye pia ni dereva bodaboda, amemshukuru Waziri Mchengerwa kwa kuhakikisha Barabara ya Kituo cha Afya Ikwiriri inajengwa, na hatimaye kuwawezesha wagonjwa kufika kwenye kituo hicho cha afya kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuwawezesha madereva bodaboda kujiongezea kipato.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema amefanya kazi usiku na mchana ya kuleta mabadiliko wilayani Rufiji kwa kushirikiana na viongozi wa kata zote, lengo likiwa ni kuboresha upatikianaji wa huduma za kijamii ambapo wananchi hivisasa wanafurahia huduma zinazotolewa katika sekta ya elimu, afya na barabara.
Mhe. Mchengerwa amesema: “Tumefanya kazi usiku na mchana kuhakikisha tunaibadilisha Rufiji, tulianza ujenzi wa shule, ujenzi wa zahanati, ujenzi wa vituo vya afya na miundombinu ya barabara na mingineyo,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Mhe. Mchengerwa ameongeza kuwa, walikubaliana kwamba ndoto ya wanarufiji ni kuleta mabadiliko, hivyo ana uhakika mwananchi yeyote akiulizwa hivisasa ataeleza namna ndoto hiyo ilivyotimia katika kipindi hiki cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ikwiriri Dkt. Tegemei Mtambo ameishukuru Serikali kwa kuwapatia milioni 140 zilizowezesha ujenzi wa jengo la huduma za mionzi na huduma tayari imeanza kutolewa, ambapo awali wananchi walilazimika kusafiri zaidi ya kilomita 30 kufuata huduma hiyo katika Hospitali ya Wilaya na Hospitali ya Misheni Mchukwi.
Sanjari na hilo, Dkt. Mtambo ameishukuru Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kuwapatia X-Ray ya kisasa inayowahudumia wananchi, aidha amemshukuru Waziri Mchengerwa kwa kutimiza ahadi yake ya kumleta Mteknolojia wa Mionzi ikiwa ni pamoja usimamizi wa maboresho yote yaliyofanyika kiasi cha watu kuamini kuwa Kituo cha Afya Ikwiriri ndio Hospitali ya Wilaya ya Rufiji.

RHMT NA CHMT SIMAMIENI MIRADI YA AFYA – DKT. MFAUME
Mkurugenzi wa Idara ya Afya Lishe na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume amezielekeza timu za usimamizi wa afya ngazi za Mikoa (RHMT) na ngazi za Halmashauri (CHMT) na timu za usimamizi wa vituo vya afya kusimamia miradi ya afya inayotekelezwa katika maeneo yao Kwa ukaribu zaidi.
Dkt. Mfaume amesema hayo wakati wa majumuisho ya Mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya ziara yake ya Usimamizi shirikikishi ya upatikanaji wa huduma za afya, Lishe na Ustawi wa Jamii katika mkoa huo.
“Mara nyingi RHMT na CHMT tumekuwa tukichelewa sana kujishirikisha na miradi, jengo likianza hadi kukamilika hatujatembelea kulikagua wakati sisi ndio wataalamu na watumiaji wakubwa wa majengo hayo” amesema Dkt. Mfaume
Amesema kutokana na timu hizo kutofatilia miradi hiyo kwa ukaribu imesababisha miradi mingi kutekelezwa kinyume na Miongozo na maelekezo ya maeneo ya utoaji wa huduma za afya yanavyotakiwa kuwa.
“Kutokana na miongozo yetu, majengo yanajengwa na kuna viwango vyake katika kila eneo kama na maabara n.k, na yanafuatana toka mgonjwa anaingia eneo la kupata huduma (OPD) hadi katika maeneo ya kufulia na vichomea taka hivyo nahimiza kujishirikisha na kutoa ushauri wa kitaalam kwa mafundi wetu” amesisitiza
Aidha, Dkt. Mfaume amezitaka Halmashauri kuhakikisha majengo mbalimbali ya kutolea huduma za afya ambayo yamekwisha kukamilika kuanza kutoa huduma kwa wakati kwa lengo la kuwahudumia wananchi kama ambavyo Serikali imekusudia.
Pia amezitaka Halmashauri kuendelea kuajiri watumishi kwa mkataba ili kuendelea kupunguza uhaba wa watumishi katika maeneo ya kutolea huduma za afya, hasa katika maeneo yenye watumishi wachache.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Aman Mafuru amesema ziara hiyo ya Mkurugenzi imekuwa kama jicho la wazi la kujitathmini kama Mkoa kwa namna unavyotekeleza majukumu yake katika Sekta ya afya.
“Katika ziara hii ya usimamizi yapo mambo mengi umeyaona na kutolea maelekezo na tayari sisi kama Mkoa tumeanza katika baadhi ya maeneo na tunaendelea kwa yale bado”.

UJENZI WA UZIO KWENYE SHULE, SERIKALI YAJA NA MKAKATI MAALUM*
OR- TAMISEMI
Serikali imesema tayari imeweka bajeti na michoro (Master Plan) kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika shule zote za Hsekondari za mikoa kama hatua ya kuimarisha ulinzi wa mali za shule na usalama wa wanafunzi.
Akijibu maswali kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais– TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa, Naibu Waziri Mhe. Dkt. Festo Dugange ameliambia bunge leo Mei 09,2025 kuwa pamoja na hatua hiyo wakurugenzi wa halmashauri kupitia mapato ya ndani waendelee kutenga fedha za ujenzi wa uzio kwa ajili ya usalama wa wanafunzi na mali za shule kwenye maeneo yao kadiri ya upatikanaji wa fedha.
Naibu Waziri Dugange ametoa maelekezo hayo wakati akijibu swali la Mheshimiwa Dkt. Angelina Mabula mbunge wa jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza aliyeuliza kuwa ni lini Serikali itajenga uzio katika Shule za Msingi ambazo hazina uzio maeneo ya Mijini.
Katika majibu yake Naibu Waziri Dkt. Dugange amesema “Katika mwaka 2022/23 na 2023/24 serikali imetoa shilingi bilioni 5.57 kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika shule 185 za watoto wenye mahitaji maalumu, lakini pia Vilevile, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimekuwa zikitenga fedha kupitia mapato ya ndani kujenga uzio ili kuimarisha ulinzi katika maeneo yenye changamoto za kiusalama.”

Dkt. Mfaume azishauri Halmashauri kupima maeneo ya kutolea huduma za afya
OR-TAMISEMI
Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume, amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha zinapima maeneo yaliyojengwa vituo vya kutolea huduma za afya ili kupata hati miliki za maeneo hayo.
Dkt. Mfaume ameyasema hayo alipokuwa katika ziara yake ya ukaguzi wa huduma za afya, lishe na ustawi wa jamii katika mkoa wa Dar es salaam, ambapo alitembelea katika kituo cha afya cha Toangoma kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
“Ni lazima tupime maeneo yetu, tuweke mipaka rasmi na kuhakikisha yanakuwa na hati miliki ili kuzuia uvamizi kutoka kwa wananchi na kuimarisha utoaji wa huduma za afya,” amesema Dkt. Mfaume
Amesema vituo vingi vya kutolea huduma za afya baadhi ya maeneo ni ya muda mrefu hivyo hakuna sababu ya msingi inayopelekea vituo hivyo kutopimwa na kuwa na umiliki wa hati.
Aidha, Dkt. Mfaume amewataka Waganga Wafawidhi wa vituo vya afya na kamati za usimamizi wa vituo vya kutolea huduma za afya kushirikiana na viongozi wa Serikali za Mitaa, viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa Dini kwani wao ndio mara nyingi huwa karibu na wananchi.
“Hatuwezi kuchora mstari kati yetu sisi wataalam na viongozi katika maeneo yetu, hasa tunapoelekea katika utekelezaji wa mpango wa bima ya afya kwa wote lazima tuungane na viongozi hawa ili kufikisha elimu kwa wananchi” amesisitiza.

Afrika yaaswa kuungana kuimarisha elimu mtandao, mifumo na uchumi wa kidigitali
Na Fred Kibano, D'Salaam
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amefungua kongamano la Kimataifa la elimu mtandao Afrika na kuzitaka nchi za Afrika kuungana ili kuleta mapinduzi ya elimu mtandao na kujenga uchumi wa kidigitali.
Mheshimiwa Dkt. Biteko ameyasema hayo leo wakati akifungua kongamano la Kimataifa la 18 la elimu mtandao kwa Afrika ‘eLearning Africa’ kwa niaba ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam leo tarehe 7 Mei, 2025 Jijini Dar es Salaam na kutoa wito kwa nchi za Afrika kuungana pamoja ili kuleta mapinduzi ya elimu mtandao na kujenga Uchumi imara wa kidigitali miongoni mwao.
“mustakabali wa Afrika ni kuungana pamoja na kuimarisha miundo ya ushirikiano inayoruhusu uundaji wa suluhu za kidigitali zinazolengwa kulingana na mahitaji ya Afrika ambayo yatasaidia kuleta mageuzi ya kidijitali ambayo ni jumuishi na yenye matokeo, kushughulikia changamoto mahususi zinazokabili kanda mbalimbali na kuchangia ustawi wa muda mrefu wa Afrika” alisema Biteko.
Aidha, ameitaka Afrika kuendelea kuelimisha na kuendeleza rasilimali watu, kuwashirikisha wataalamu wenye ujuzi ndani na nje ya Afrika ili kuchangia kujenga uchumi imara wa kidigitali ambao utasaidia kuongeza uwezo wa kujitegemea na kuwezesha ukuaji endelevu wa uchumi wa kidijitali.
Kwa upande wake Mhe. Prof. Adolf Mkenda amesema lengo kuu la elimu mtandao kwa Afrika (ELearning Africa) ni kupanua ufikaji wa elimu na mafunzo bora lakini pamoja na maboresho ya Sera ya Elimu, Serikali imewekeza katika uwezo wa kimsingi kupitia ushirikiano wa Sekta ya Umma na Binafsi, inawezesha pia walimu, Viongozi wa shule na wakufunzi kujumuisha teknolojia katika ujifunzaji, huku ikichunguza matumizi ya AI katika ujifunzaji ambayo pia itasaidia katika utungaji Sera.
“Hatua muhimu ni Sera ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya 2014 iliyosasishwa (toleo la 2023), ambayo inatanguliza ujumuishaji wa kidijitali katika ufundishaji na ujifunzaji. Hii inakamilishwa na Mkakati wa Kitaifa wa Elimu ya Dijiti na Miongozo ya utekelezaji, ikijumuisha ile ya matumizi ya AI katika elimu” anasisitiza Prof. Mkenda.
Kongamano hilo linalofanyika kwa mara ya pili hapa nchini limewakutanisha wadau zaidi ya 1500 wa Sekta mbalimbali kutoka nchi za Afrika pamoja na Wadau wa Maendeleo wakiwemo wataalamu, wabunifu, watafiti, wawekezaji na wafanyabiashara ili kujadiliana, kubadilishana uzoefu na kupanga mikakati ya pamoja kama Afrika jinsi ya kutumia teknolojia ya kidigitali katika kuendeleza Sekta ya Elimu kwa ajili ya kujiletea maendeleo likiwa na Kauli Mbiu inayosema “Kufikiri Upya Elimu na Maendeleo ya Rasilimali Watu kwa ustawi wa Baadae wa Afrika”

Serikali na Imagine Wazindua Mradi wa MsingiTek Kuboresha Stadi za KKK kwa Shule 500
Angela Msimbira MANYARA
Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na shirika la Imagine imezindua rasmi mradi wa MsingiTek utakaotekelezwa katika mikoa 5 na halmashauri 10, ukihusisha shule 500 za Tanzania Bara.
Akiongea kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu Atupele Mwambwene, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Elimu Bi.Suzan Nussu amesema lengo la mradi ni kuboresha stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) kwa madarasa ya awali (darasa la I–III), kwa kutumia vishikwambi vyenye programu maalum zinazomsaidia mwanafunzi kujifunza kwa njia shirikishi na ya kuvutia.
Ameendelea kufafanua kuwa mradi wa msingTek utarahisisha kazi ya ualimu, kupunguza utoro, na kuongeza motisha kwa wanafunzi.
Pia amewaelekeza viongozi wa sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kushirikiana kwa karibu na walimu kuhakikisha mradi huo unafanikiwa na kuweza kupanuliwa zaidi.

Mwenendo wa urejeshaji mikopo kwenye halmashauri unaridhisha- Dkt. Dugange.
OR - TAMISEMI
Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI imesema mwenendo wa urejeshaji wa mikopo yote iliyotolewa kwa vikundi vya wanawake, wajasiliamali, watu wenye ulemavu na vijana kabla ya Aprili 2023 ni wenye kuridhisha na Serikali imeendelea kusimamia ili kuhakikisha pesa yote iliyokopeshwa inarejeshwa.
Hayo yamesemwa leo Mei 08, 2025 bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange wakati akijibu swali la msingi la Mheshimiwa Mwantumu Haji Mbunge wa Viti Maalum aliyetaka kujua ni lini Serikali itaanza kuwapatia Mikopo Wajasiriamali Wadogo Wanawake na Vijana.
Katika majibu yake Naibu Waziri Dkt. Dugange amesema, Serikali ilifanya tathimini juu ya utaratibu wa mwanzo uliokuwa ukitumika kutoa na kurejesha mikopo na ilibaini uwepo wa mianya ya kufanya vikundi kutorejesha mikopo kwa ufanisi na kwa wakati unaotakiwa ndiyo maana serikali ilisitisha mikopo hiyo na kuandaa kamati mpya, utaratibu na kanuni kwa ajili ya kusimamia mikopo hiyo katika maeneo yote ya halamashauri.
“Mheshimiwa Spika, Serikali ilisitisha kwa muda utoaji wa mikopo ya asilimia 10 katika mamlaka za serikali za mitaa Aprili 2023 kwa lengo la kufanya maboresho. Aidha, mikopo hii ilianza kutolewa tena tarehe 01 Julai, 2024 kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa na Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu za mwaka 2024” alisema Naibu Waziri Dkt. Dugange.
Aidha aliongeza kuwa “Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2024/25, Serikali kupitia halmashauri ilitoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 82.84 kwa vikundi 8,275 vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 40.71 zilitolewa kwa vikundi vya wanawake, shilingi bilioni 36.64 kwa vikundi vya vijana, na shilingi bilioni 5.48 kwa vikundi vya watu wenye ulemavu”.Amefafanua Mhe. Dugange

Mhe. Chatanda ashuhudia utiaji saini wa Bilioni 13.3 kuboresha miundombinu Rufiji, Mhe. Mchengerwa azindua Ligi ya ”Mchengerwa Mtu Kazi”.
Na John Mapepele
Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mhe. Mary Pius Chatanda ameshuhudia utiaji saini wa mikataba mitano ya bilioni 13.3 zilizotolewa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ili kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja wilayani Rufiji, huku Mhe. Mchengerwa akizindua rasmi Ligi ya ”Mchengerwa Mtu Kazi” inayoanza leo Mei 8, 2025 na kutoa vifaa (jezi na mipira) kwa timu zote 169 kutoka kwenye kata 13 zinazoshiriki mashindano hayo vyenye gharama ya milioni 67 pamoja na fedha taslimu milioni 25 ikiwa ni zawadi za washindi.
Tukio hili la utiaji saini limefanyika Mei 7, 2025 mara baada ya kukamilika kwa ziara ya siku mbili ya Mhe. Chatanda kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo, katika eneo la uwanja wa stendi wa Ikwiriri na kushuhudiwa na maelfu ya wananchi wa wilaya hiyo huku wasanii kadhaa wakitumbuiza kwa burudani za muziki.
Akitoa taarifa ya miradi hiyo, Meneja wa Wakala za Barabara Vijijini na
Mijini (TARURA) mkoa wa Pwani, Leopold Runji amefafanua kuwa gharama hizo zinahusisha ukarabati wa barabara ya Nyamwage yenye Kilomita 28, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya Chumbi- Kiegele yenye kilomita 1.4, ukarabati wa barabara ya Mohoro- Mtanga kilomita 12.3 na Mohoro Ndundutawa yenye kilomita 7.5.
Pia ukarabati wa barabara ya Nyamwage- Mpakani- Nambunju na ujenzi wa barabara za lami katikati ya mji wa Ikwiriri ambapo amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia kuiunganisha wilaya hiyo na maeneo mbalimbali ya mikoa ya Tanzania.
Mhe. Chatanda amemshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha za miradi na kufafanua kwamba kwa kufanya hivyo siyo tu ametekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa mafanikio makubwa bali ameleta mapinduzi katika sekta ya miundombinu kote nchini.
Amempongeza Mhe. Mchengerwa kwa kusimamia utekelezaji wa miradi yote kwa kiwango cha juu huku akitoa wito kwa maeneo mengine nchini kuiga utekelezaji huo.
”Ndugu zangu hapa ni vema tuwe wakweli, unaweza ukaletewa fedha za maendeleo lakini ukashindwa kutekeleza lakini,hivyo nampongeza mbunge wenu kwa kusimamia utekelezaji wa miradi hii ambayo inakwenda kuleta tija kubwa kwa wananchi katika Wilaya ya Rufiji” amefafanua Mhe. Chatanda
Mbali na kukagua miradi ya Serikali pia ameshuhudia ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa chama, pia ameshuhudia mradi mkubwa wa ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa wilaya unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 2.5 unaofadhiliwa na Mbunge wa Rufiji Mhe. Mchengerwa kwa kupitia marafiki na wadau mbalimbali.
Akizungumzia kuhusu miradi ya elimu katika wilaya hiyo, Mhe. Chatanda amesema amefurahishwa na kazi nzuri ya ongezeko kubwa la Shule za Msingi na Sekondari na kutoa wito kwa wananchi kuwapeleka watoto wao katika shule hizo ili kuunga mkono maono ya Mhe. Rais ya kuwakomboa wananchi kielimu pia kwa manufaa makubwa ya taifa na vizazi vyao.
Mbunge wa Rufiji Mhe. Mchengerwa amesisitiza kuwa Serikali imefanya kazi kubwa ya ujenzi wa shule ambapo amesema wakati anaingia kwenye ubunge kulikuwa na na Shule za Msingi 40 tu ambapo sasa kuna shule 63 na upande wa Vituo vya Afya, awali kulikuwa na vituo 3 na sasa vimefika 9, huku asimshukuru Mhe. Rais Samia kwa maono makubwa ya kuwaletea maendeleo watanzania.
Aidha, Mhe. Chatanda alipotembelea na kukagua ukarabati wa hospitali ya Wilaya ya Rufiji na ujenzi wa kichomea taka katika eneo la Utete uliogharimu takribani milioni 900 na kuwataka wananchi kutumia huduma hizo ikiwa ni pamoja na wanaume kuwa msitari wa mbele kuwapeleka wake zao kwenye huduma za kliniki ili kujua afya za wenza wao na watoto.
Akizungungumzia kuhusu ukatili wa kijinsia, amewataka wazazi kuwalea watoto wao katika misingi maadili ili waweze kuja kuwa wazazi bora badala ya kuwaacha kujifunza kwenye mitandao.
Wakati huo huo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kupiga kura huku akisisitiza kuchagua CCM kwa kuwa ndicho chama kilichowaletea maendeleo.

DC Simanjiro Azindua Mradi wa MsingiTek Ataka Vifaa vya TEHAMA Vilindwe na Usalama wa Wanafunzi Uimarishwe
Angela Msimbira Simanjiro, MANYARA
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mkoa wa Manyara,Mhe.Fakii Raphael Lulandala ameongoza uzinduzi wa Mradi wa MsingiTek wilayani humo, akitoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamia kwa umakini utunzaji na matumizi sahihi ya vifaa vya TEHAMA vinavyotolewa na Serikali na Wadau wa Maendeleo.
Akizindua mradi huo leo Mei 7, 2025 katika shule ya msingi Losinyai, Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkuu huyo wa Wilaya amewataka Viongozi hao kuhakikisha vifaa kama vishikwambi vinavyotolewa kupitia mradi wa MsingiTech vinatunzwa ipasavyo na kutumika kama ilivyokusudiwa — kusaidia kujenga Stadi za msingi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kwa wanafunzi wa madarasa ya awali.
“Ni wajibu wa kila Halmashauri kuhakikisha vifaa hivi havipotei wala kuharibika, bali vinatumika kuongeza ufanisi wa ujifunzaji. Huu ni uwekezaji mkubwa wa Serikali na wadau wake kwa ajili ya kizazi kijacho,” amesisitiza.
Mradi wa MsingiTek unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na shirika la Imagine unalenga shule 500 katika mikoa mitano ya Tanzania Bara. Katika Wilaya ya Simanjiro, shule za msingi zilizohusika katika awamu ya kwanza ni pamoja na Shule ya Msingi Losinyai, Shule ya Msingi Emboreet, na Shule ya Msingi Naisinyai, ambapo wanafunzi wamekabidhiwa vishikwambi vyenye programu maalum za masomo ya awali.
Pia, amezihimiza Halmashauri kuhakikisha zinakuwa na mikakati thabiti ya kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya unyanyasaji, hasa kwa kuzingatia mazingira ya matumizi ya teknolojia.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa upatikanaji wa chakula shuleni kama njia ya kupunguza utoro na kuongeza umakini wa wanafunzi darasani.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la Imagine Tanzania Bi. Jaqline Mgumia amesema shirika hilo linafurahia kushirikiana na Serikali katika kutekeleza mradi wa MsingiTech, ambao unalenga kuleta mapinduzi chanya katika ujifunzaji kwa watoto wadogo kwa kutumia teknolojia.
“Tumeshuhudia matokeo chanya katika maeneo tuliyofikia. Watoto wanapata hamasa ya kujifunza kupitia michezo ya kielimu kwenye vishikwambi, na walimu nao wamerahisishiwa kazi ya kufundisha,” amesema Bi. Mgumia
Akiwahutubia wanafunzi wa Shule ya Msingi Losinyai, Mhe. Lulandala amewasihi wanafunzi hao kuvitunza vishikwambi walivyopewa, huku akisisitiza kuwa vifaa hivyo ni mali ya Umma na vina thamani kubwa kwa maendeleo yao.

Katimba atembelea banda la TAMISEMI kwenye Kongamano la Kimataifa na Maonesho ya Elimu Mtandao Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri anayeshughuhulikia Elimu Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe.Zainab Katimba atembelea banda la TAMISEMI kwenye Kongamano la Kimataifa na Maonesho ya Elimu Mtandao Jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Zainab Katimba ametembelea banda la maonesho la Ofisi ya Rais -TAMISEMI kwenye Kongamano la 18 la kimataifa na Maonesho ya Elimu Mtandao, Mafunzo na Maendeleo ya Kukuza Ujuzi yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam kuanzia leo Mei 7 hadi 9, 2025.
Mheshimiwa Katimba amejionea jinsi Mfumo wa Taarifa za Shule (SIS) unavyofanya kazi kwa kukusanya taarifa za shule za kila siku kupitia moduli mbalimbali zilizounganishwa na Mfumo huo.
Pia amepata maelezo ya namna ya darasa janja (smart class) linavyofanya kazi za kufundisha na kutoa mafunzo kama sehemu ya Elimu Mtandandao (eLearning).
Maonesho na Kongamano hilo la Elimu Mtandao yanajulikana kama “eLearnging Africa’ yanafanyika kwa mara ya pili Tanzania na mara ya kwanza yalifanyika mwaka 2007, yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiwahusisha wadau mbalimbali kutoka Wizara, Taasisi, Mashirika ya Kimataifa na Wadau wengine na Kauli Mbiu yake ni “Kufikiri Upya Elimu na Maendeleo ya Rasilimali Watu kwa ustawi wa Baadae wa Afrika”

KERO YA MAJI KIJIJI CHA MLOKA, MBUNJU MVULENI NA NDUNDUTAWA YAPATIWA UFUMBUZI.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa, ameshuhudia hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya Maji itakayojengwa katika Vijiji vitatu vya Mloka, Mbunju Mvuleni pamoja na Ndundutawa ambayo itahudumia Wananchi 16, 593 hali itakayosaidia kupunguza kero ya Maji katika maeneo hayo.
Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilayani Rufiji Mhandisi Alkam Sabuni, alisema ujenzi wa Miradi ya Maji katika Vijiji hivyo utagaharimu kiiasi cha Shilingi 791,068,682.56.
"Katika Kipindi Cha Mwezi Juni 2025 hadi Oktoba 2025 Wananchi wapatao 16,593 wa Vijiji vitatu vya Mloka, Mbunju Mvuleni na Ndundutawa wanaenda kunufaika na huduma ya Maji safi na salama na yenye kutosheleza, ambapo miradi hii itakapokamilika itaongeza hali ya upatikanaji wa Maji kutoka asilimia 86.6 ya sasa hadi asilimia 97.3" alisema Sabuni
Hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba ya ujenzi wa miradi hiyo imefanyika katika Kijiji Cha Mloka Kata ya Mwaseni Jana Mei 6, 2025.
Sabuni aliongeza kuwa RUWASA Wilayani Rufiji inatoa huduma katika Vijiji 38 vyenye Jumla ya Watu 157,412 kwa Mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa alisema uwepo wa miradi iyakapokamilika itasaidia kupunguza adha ya Wananchi kwenda kuchoma Maji katika Mto Rufiji.
"leo tumeandika historia katika changamoto ambazo tumekuwa tukizipata kwa muda mrefu leo tumezimaliza na matarajio yangu kwamba Mkandarasi sasa ataanza kazi mara Moja" alisema Mchengerwa.

SERIKALI KUENDELEA KUKARABATI VITUO VYOTE KONGWE, VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA.
Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI imesema itaendelea kukarabati hospitali zote Kongwe kupitia mpango mkakati wa ukarabati, na upanuzi wa hospitali kongwe za halmashauri ,vituo vya afya Pamoja na Zahanati ili kuboresha miundombinu ya huduma za afya kote nchini.
Hayo yamesemwa leo Mei 07, 2025 bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange wakati akijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shally Raymond, mbunge wa viti maalum mkoa wa Kilimanjaro kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa , aliyetaka kujua ni lini serikali itaipa kipaumbele cha ukarabati wa miundombinu zahanati ya Rononi iliyoko Uru Kasikizini Mkoani humo.
Katika majibu yake Naibu Waziri Dkt. Dugange amesema tayari serikali imeweka mpango mkakati wa ukarabati na upanuzi wa vituo vyote kongwe vya kutolea huduma za afya, ambapo tayari ukarabati na upanuzi umeanza katika ngazi ya hospitali kongwe za halmashauri, na baada ya hospitali za halmashauri, vitafutata vituo vya afya na zahanati zote kongwe ambazo zinahitaji ukarabati.
Hata hivyo Naibu waizri Dkt. Dugange ameelekeza wakurugenzi katika halmashauri zenye vituo vya kutolea huduma za afya vinavyokabiliwa na uhaba wa vifaa Pamoja na changamoto ndogondogo kama vile samani kutumia fedha za mapato ya ndani kumaliza changamoto hizo haraka iwezekanavyo.

MHE. CHATANDA AMPONGEZA RAIS KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI
Na Mwandishi Wetu..
Mwenyekiti wa UWT- CCM Taifa, Mhe. Mary Pius Chatanda amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya bilioni 25 inayotekelezwa wilayani Rufiji na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.
Mbali na kumpongeza Mhe. Rais Samia, pia amempongeza Mbunge wa Rufiji kwa kusimamia utekelezaji wake ambapo amesema miradi hiyo imesimamiwa vizuri na ina tija kubwa kwa wananchi.
"Hapa naomba niungane na watanzania wote kumpongeza Rais wetu kipenzi Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo ameifanya nchi nzima, na hapa leo Rufiji tunashuhudia kazi nzuri ambayo imetekelezwa kupitia miradi hii" amesisitiza Mhe Chatanda
Mhe Chatanda ambaye yupo kwenye ziara ya siku mbili katika jimbo la Rufiji amekagua mradi wa ujenzi wa daraja la Mbambe linalojengwa kwa urefu wa mita 81 na ujenzi wa barabara ya lami inayounganisha barabara kuu ya kilomita 3 itakayogharimu bilioni 24.1.
Mkataba wa daraja hilo ulisainiwa na Wakala wa Barabara Tanzania na Mkandarasi M/S Nyanza Road Works Ltd ya Mwanza ambapo kazi hiyo inatarajia kukamilika katika kipindi Cha miezi 6 kuanzia sasa.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa daraja hilo Mhe. Mchengerwa alifafanua kuwa mradi wa ujenzi wa daraja hilo ni moja ya mikakati ya Serikali ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii wilayani Rufiji maeneo jirani.
Rashid Salum Mkazi wa Ikwiriri amemshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo ambapo amesema kukamilika kwake kutakuwa msaada mkubwa kutokana na adha kubwa walihokuwa wakipata hapo awali.
Aidha, Mhe. Chatanda ameshuhudia utiaji saini wab mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji katika vijiji vya Mloka, Mbinju Mvuleni na Ndundutawa ambapo pia ameshuhudia zoezi la kupewa mabati 45 na Mhe. Mbunge vijana wa bodaboda wa kijiji cha Mloka ili kuezekea eneo la kuegesha bodaboda zao.
Akitoa taarifa ya mradi huo, Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini ( RUWASA) Wilaya ya Rufiji Mhandisi Alkam Omari pamoja na uwekezaji mkubwa ambao umefanywa na Serikali katika kuwapatia wananchi maji safi na salama, mahitaji ya maji yamezidi kuongezeka ambapo amesema mradi huu unakwenda kuwa suluhisho.

RHMT NA CHMT SIKILIZENI KERO NA MAONI KUTOKA KWA WANANCHI – DKT. MFAUME.
OR-TAMISEMI
Mkurugenzi wa Idara ya Afya Lishe na Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume amezielekeza timu za usimamizi wa afya ngazi ya Mkoa (RHMT) na ngazi ya Halmashauri (CHMT) kusikiliza kero na maoni kutoka kwa Wananchi pindi wanapotembelea kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwaajili ya ziara za kikazi na ukaguzi.
Dkt. Mfaume amesema hayo alipotembelea Hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kukagua upatikanaji wa huduma za afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Katika Manispaa hiyo.
“Mara nyingi RHMT na CHMT tumekuwa tukifanya ziara za ukaguzi katika maeneo ya kutolea huduma za afya bila kusikiliza mrejesho wowote kutoka kwa wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa ziara hizo” amesema Dkt. Mfaume.
Amesema tusipopita na kusikiliza kero au maoni ya wananchi namna wanavyopokea huduma, uwekezaji wote ambao serikali umefanya katika ujenzi wa vituo vya afya, hospital na zahanati utakuwa hauna maana hivyo ni muhimu sana kuwasikiliza wananchi.
Aidha, Dkt. Mfaume amevielekeza vituo vya kutolea huduma za afya kwa kushirikiana na CHMT kutumia vizuri vitengo vya Mawasiliano Serikalini (GCU) katika kutangaza huduma zinazotolewa na vituo hivyo.
“Kuna huduma nyingi kubwa na muhimu sana ambazo hivi sasa Nchini zinatolewa hadi ngazi ya vituo vya afya lakini wananchi wetu hawana taarifa hivyo ni muhimu vituo na halmashauri kutumia wataalamu wetu katika vitengo vya Mawasiliano Serikalini (GCU) kutangaza huduma hizo kwa Wananchi” amesisitiza.

Mhe. Mchengerwa atoa Tuzo ya Samia Kalamu Awards kwa Dodoma FM
Na John Mapepele
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameshiriki hafla ya utoaji wa Tuzo za Samia Kalamu Awards 2025 kwa Waandishi wa Habari iliyofanyika katika ukumbi wa The Super Dome Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Mei, 2025.
Akiwa katika tukio hilo, Mhe. Mchengerwa ametoa tuzo kwa mtangazaji Leila Sanga wa Dodoma Fm Radio kituo ambacho kimeshinda tuzo ya kipengele cha redio za jamii.
Dodoma Fm Radio ni kituo kilichopo Dodoma, kilianzishwa mwaka 2010 kikiwa na lengo la kuchangia maendeleo ya mkoa wa Dodoma katika nyanja mbalimbali.
Makala iliyoshinda katika tuzo hizi inaitwa "Nani anaathirika na mabadiliko ya tabia nchi" ambapo iliangazia matumizi ya nishati safi yanavyoweza kuwapunguzia wanawake adha ya kufuata kuni umbali mrefu kitendo kinachowafanya kukutana na ukatili wa kijinsia ,pia matumizi ya nishati safi ya kupikia yanavyoweza kuokoa muda kwa mwanamke kufanya shughuli za kiuchumi.
"Tulifanya hivi kwa sababu ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia
Pia kuhamasisha jamii kuchukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
Kuokoa wanawake na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa jamii ya Dodoma ambapo wanawake wengi wanalazimika kufuata kuni umbali mrefu". Amefafanua Sanga
Mgeni rasmi katika tukio hilo amekuwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo alisistiza Waandishi wa Habari kuwa wazalendo kwa nchi yao wakati wanafanya kazi zao.
Aidha, amewataka kuelezea mafanikio na mageuzi yanayofanywa na Serikali.
Amevipongeza Vyombo vya Habari kwa kazi nzuri vinayofanya kwa kutangaza miradi mbalimbali ya Serikali.
"Ndugu zangu hatusemi kuwa msiikosoe Serikali bali tunasema tuwe wazalendo kwa nchi yetu kwa kuwa hatuna Tanzania nyingine" amesisitiza Mhe. Rais
Tuzo hizo ziliandaliwa na Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania na Mamlaka ya Mawasilino Tanzania ambapo tuzo katika sekta mbalimbali zilitolewa.

DAR ES SALAAM YASHAURIWA KUJENGA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA KATIKA MUUNDO WA GOROFA– DKT.MFAUME.
OR-TAMISEMI
Mkurugenzi wa Idara ya Afya Lishe na Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume amesema kutokana na uhaba wa maeneo katika Jiji la Dar es Salaam ni vyema Halmashauri zifikirie kujenga majengo ya kutolea huduma za afya kwa muundo wa gorofa.
Dkt. Mfaume amesema hayo wakati alipotembelea kituo cha afya cha Kinondoni kwenye ziara yake ya kukagua upatikanaji wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii katika Manispaa ya Kinondoni, Mkoani Dar es salaam.
“Kutokana na uhaba wa maeneo kwenye Mkoa wetu ni vyema sasa tukafikiria kujenga vituo vya kutolea huduma za afya kwa muundo wa gorofa hata kama tutajenga kwa awamu” amesisitiza.
Aidha, Dkt. Mfaume amevielekeza vituo vya afya vyenye mapato makubwa yatokanayo na wananchi kuchangia huduma kutumia mapato hayo katika kutekeleza miradi mbalimbali ili kufanikisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi ikiwemo ununuzi wa vifaa tiba.
“Niwapongeze kituo cha afya cha Bunju kwa kutumia fedha za mapato ya ndani zaidi ya Mil. 172 kununua vifaa tiba, na nivielekeze vituo vyenye mapato makubwa pia kuiga mfano huu wa kituo cha afya cha Bunju” amesisitiza.
Ameongeza kuwa, katika kuelekea utekelezaji wa huduma ya Bima ya Afya kwa wote ni lazima vituo vyote vya afya kuwa tayari kwa ajili ya kuwahudumia wanachama hao kwa huduma mbalimbali.

BARABARA KOROFI YA MABOGINI - KAHE KUJENGWA KWA LAMI- MHE MCHENGERWA
Na John Mapepele -Moshi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo amekagua uharibifu wa barabara ya Spencon- Fongagate- Mabogini- Chekereni hadi Kahe yenye urefu wa kilomita 31.25 na kuiagiza Wakala ya Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kuanza mara moja kujenga kwa kiwango cha lami.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa Mabogini na Kahe amesema Serikali inakwenda kujenga kwa kiwango cha lami Ili ipitike katika kipindi chote cha mwaka ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Aidha, amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutarahisisha huduma ya usafiri kwa wananchi kwenda kupata huduma ya afya na elimu.
" Kukamilika kwa barabara hii kutasaidia wananchi wetu kufikisha mazao yao sokoni kwa maana ya Moshi Mjini na maeneo mbalimbali nchini hivyo kukuza kilimo cha mazao ya mpunga, mahindi na miwa ambayo yameonyesha kusitawi vema kwenye eneo hili" . Amefafanua Mhe. Mchengerwa
Amesema katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa barabara hiyo utahusisha ujenzi wa mitaro mikubwa kwa pande zote mbili, madaraja na kuweka mawe na kifusi ambapo utaifanye ipitike katika misimu yote ya mwaka.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seiff amesema mradi wa ujenzi wa barabara hiyo hadi kukamilika kutagharimu takribani bilioni 45 ambapo awamu ya kwanza itagharimu jumla ya shilingi bilioni 7.
Pia Waziri Mchengerwa amezielekeza Halmashauri zote nchini kukusanya mapato ya ndani na kuanza kutenga 10% kwa ajili ya ujenzi wa barabara.
Wakati huohuo amewaagiza wakuu wote wa mikoa na Wilaya kuendelea kulinda amani na kudhibiti vitendo vyovyote vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

NMB YAKABIDHI VIFAA VYA MILIONI.42.4 KIGOMA,WADAU WAHIMIZWA KUUNGA MKONO SERIKALI
OR- TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amepokea Vifaa vyenye thamani ya shilingi Mil.42.4 kwa ajili ya huduma za Afya na Elimu kutoka Benki ya NMB ikiwa ni sehemu ya benki hiyo kurejesha kwa Jamii.
Akipokea vifaa hivyo Mhe. Katimba amesema serikali inaendelea kuhakikisha inapeleka maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya,Elimu na miundombinu hiivyo amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ili kuwaletea maendeleo wananchi.
“Tuwashukuru sana wadau wetu wakubwa wa NMB tunatambua jitihada zenu za kuunga mkono serikali kwa juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita katika sekta nyingi ikiwemo Afya na Elimu” amesema
Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa na Kaimu meneja wa NMB kanda ya Magharibi Gardiel Sawe ni vifaa vya kujifungulia, Viti vitano (05) kwa ajili ya Wagonjwa, Vitanda kumi (10) kwa ajili ya Wajawazito kujifungulia ambavyo vyote vimetolewa kwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Vitanda hamsini (50) kwa Wanafunzi wa Shule za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Hata hivyo, vifaa vya Afya vitasambazwa na kunufaisha Kituo cha Afya cha Ujiji, Kituo cha afya cha Buhanda, Kituo cha afya cha Kikunku na Zahanati ya Bangwe.

WATUMISHI KUJENGEWA UWEZO MATUMIZI YA MIFUMO YA TEHAMA.
OR-TAMISEMI
Mkurugenzi wa Idara ya Afya Lishe na Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume amezielekeza timu ya usimamizi wa afya ya Mkoa wa Dar es Salaam (RHMT) na timu ya usimamizi wa afya (CHMT) katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kuandaa mpango kazi wa kuwajengea uwezo wa matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika maeneo ya kutolea huduma za afya.
Dkt. Mfaume amesema hayo kwenye kikao cha majumuisho katika hospitali ya Mbezi mara baada ziara yake yenye lengo la kuangalia upatikanaji wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii kwenye Halmashauri hiyo.
“Imefungwa mifumo mbalimbali ya TEHAMA katika vituo vyetu vya kutolea huduma za afya lakini kufungwa tu haitoshi, tumeona kuna changamoto kubwa sana ya uwezo wa watumishi wetu kutumia mifumo hii hivyo Halmashauri iandae mpango kazi kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo” amesema Dkt.Mfaume
Amesema lazima halmashauri ziwekeze kwenye TEHEMA kwa kuwajengea uwezo watumishi kwa kuwa ni muelekeo wa Dunia kwa sasa.
Aidha, Dkt. Mfaume amesema matumizi ya mifumo mbalimbali katika sekta ya afya yamekuwa na mchango mkubwa sana katika kuboresha huduma na kuongeza mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KULETA SERIKALI KWA WANANCHI ILI KULETA MAENDELEO - MHE. MCHENGERWA
Na John Mapepele
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imedhamiria kwa dhati kuisogeza Serikali karibu zaidi na wananchi wake hasa wale walio na kipato cha chini katika maeneo ya vijijini na mijini ili kuwaletea maendeleo.
Akizungumza kwenye Kongamano la Uchumi la Arusha leo Mei 3, 2025 jijini Arusha akiwa miongoni mwa watoa mada, Mhe. Mchengerwa amefafanua kwamba lengo kuu ni kuwakomboa wananchi kutoka katika mnyororo wa ukosefu wa taarifa, huduma na fursa, kwa kuwajengea uelewa, uwezo na maarifa ya msingi, sambamba na kuwawekea miundombinu inayowawezesha kushiriki kikamilifu katika kupanga na kutekeleza mipango yao ya maendeleo.
“Tupo katika zama ambazo maendeleo hayategemei tena maamuzi ya viongozi wa kitaifa peke yao, bali yanategemea uwezo wa maeneo yetu ya mikoa na halmashauri zetu kuongoza kwa dira, maarifa na maamuzi ya kimkakati”.Amefafanua Mhe. Mchengerwa
Aidha, amesema utawala bora siyo tu matumizi ya sheria bali ni falsafa ya kuwezesha kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika ndoto ya taifa na kujenga taasisi imara, kusimamia rasilimali kwa uadilifu, na kutoa huduma kwa usawa bila upendeleo.
Amesisitiza kuwa kwa kutumia sera ya Decentralization by Devolution (D-by-D), halmashauri zimewezeshwa kupanga na kutekeleza mipango yao kulingana na vipaumbele vya wananchi wao na kwamba hiyo ndio njia ya kweli ya kukuza demokrasia ya kiuchumi.
”Kwa maana hiyo, TAMISEMI imewapa halmashauri zetu nguvu ya kufanya maamuzi kwa mujibu wa mazingira ya jamii zao. Hili linawezesha uwekezaji wa ardhi, huduma bora kwa wananchi, na kuimarisha mapato ya ndani”. Ameongeza Waziri Mchengerwa
Akifafanua zaidi amesema ustawi wa mikoa hautatokana na maazimio ya makaratasi pekee, bali na uthubutu wa viongozi wake kuondoa matabaka baina ya walionacho na wasio nacho ambapo amesisitiza mikoa ina wajibu wa kufanya tafiti za kina za fursa zilizopo, kutambua changamoto kisekta, kutafuta majawabu yanayotekelezeka na kuanzisha ubia mtambuka (multi-sectoral partnerships) kwa kuzingatia dira ya maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla.
Waziri Mchengerwa ameagiza kwamba kongamano lisiwe tu mkutano wa mijadala, bali chemchemi ya fikra mpya, dira ya uwekezaji wenye tija, na mlango wa fursa kwa kila raia wa Mkoa wa Arusha iwe ni kijijini au mijini.
Ametaka ongamano hilo liwe chachu ya kufungua milango mipya ya uwekezaji kwa kushirikisha Wizara na Taasisi zote husika za Serikali ili kuhakikisha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji yanaboreshwa kwa wepesi, uwazi na ushawishi chanya.
Maeneo yaliyotambuliwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili ya uwekezaji yaharakishwe kuhuishwa kwa kupangwa kitaalamu, kupimwa kwa usahihi, fidia zote itolewe kwa haki, na miundombinu ya msingi (barabara, maji, umeme, mawasiliano na huduma nyingine) ijengwe kwa haraka.
Amesisitiza kuwa wananchi na wadau wa sekta mbalimbali washirikishwe kwa kina, kwa uwazi, na kwa heshima pasipo ubaguzi wa hali za kiuchumi, jinsia, mila wala hadhi ya mtu.
Pia mchango wa wananchi wa kawaida unaojumuisha wakulima, wafanyabiashara wadogo, vijana na wanawake lazima uwekwe kikamilifu kwenye mpango unaotokana na Kongamano hili.
Aidha, ameelekeza sheria za nchi zisimamiwe kwa haki, weledi na uadilifu ili kulinda rasilimali za Mkoa na taifa na kwamba tusiruhusu migogoro isiyo ya lazima ififishe ndoto za mamilioni bali, tutumie maarifa ya ndani na teknolojia ya kisasa, kujifunza kutoka kwa uzoefu wa ndani na nje ya nchi, ili kubuni uwekezaji wa kisasa wenye tija na ustahimilivu wa muda mrefu.

MHE.MCHENGERWA ASHIRIKI KONGAMANO LA UCHUMI LA ARUSHA.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria jukwaa la uchumi Arusha linalofanyika katika Ukumbi wa IACC Arusha.
Kongamano hili limejumuisha zaidi ya wadau 1000 kutoka maeneo mbalimbali duniani na kushirikisha mawaziri kadhaa wa sekta za tofauti.
Mwanamajumui wa Afrika Profesa Patrick Lumumba pia amealikwa kuwa miongoni mwa watoa mada.
Jukwaa hilo limeandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa Mkoa huo kupata ujuzi wa namna ya kutumia fursa za uchumi zilizopo mkoani Arusha.

ZINGATIAENI VIWANGO NA UBORA WA HUDUMA ZA AFYA – DKT MFAUME.
OR-TAMISEMI
Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume amewataka watumishi wa afya katika ngazi ya msingi kuzingatia viwango (SOP) na ubora wa huduma za afya katika utekelezaji wa majukumu yao.
Dkt. Mfaume amesema hayo alipokuwa akikagua hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo katika ziara yake ya kikazi inayoendelea mkoani Dar es Salaam yenye lengo la kuangalia upatikanaji wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii.
“Wakati tunatoa hamasa kwa wananchi wanapokuja katika maeneo yetu kupata huduma lazima na sisi kama watendaji tuwe mfano kwa kuishi viwango vya ubora katika kutoa huduma bora na Salama” amesema Dkt.Mfaume
Amesema kwa kuzingatia viwango vya utoaji huduma katika maeneo ya kutendea kazi itasaidia kumlimda mtoa huduma za afya na kumlimda mteja anayepokea huduma.
Aidha, Dkt. Mfaume amesema watumishi wanaofanya kazi kwa kukiuka misingi na viwango vya utoaji wa huduma za afya anafanya kosa kisheria kwani viwango hivyo vimekubalika kitaifa na kimataifa kupitia vyama vya taaluma na Bodi za taaluma zinazowasimamia watumishi hao.

Mhe. Mchengerwa aweka jiwe la msingi jengo la jiji Arusha, ashuhudia utiaji saini mikataba ya miradi ya bilioni 40
Na John Mapepele
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo ameweka jiwe la msingi kwenye jengo la utawala la jiji la Arusha na kushuhudia utiaji wa saini mikataba ya mradi wa Stendi Kuu ya Mkoa wa Arusha, Soko la Mrombo na Bustani ya Mapumziko ya Themi vyote vikiwa thamani ya takriban shilingi bilioni 40.
Akikagua ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya jiji la Arusha lenye sakafu tisa ambalo litakapokamilika litagharimu bilioni 9.8 amemtaka mkandarasi kukamilisha ujenzi kwa wakati ili kuondokana na adha ya sasa ya watumishi kufanyia kazi kutokea kwenye ofisi zilizo katika maeneo tofauti hali inayochelewesha utoaji wa huduma kwa wananchi.
"Namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuridhia kutoa fedha za ujenzi wa jengo hili kwa kuwa baada ya kukamilika litakuwa mkombozi kwa watumishi" . Amefafanua Mhe. Mchengerwa
Aidha ameuelekeza uongozi wa Mkoa na Jiji la Arusha kuhakikisha jengo hilo linakamilika mara moja na endapo kutakuwa na mkwamo wowote wachukue hatua.
Amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda kwa kukwamua mgogoro wa kushindwa kukamilika kwa jengo hilo kwa zaidi ya miaka 5 kutokana na masuala ya kisiasa.
Mradi huo umefikia asilimia 62 na unafanywa na mkandarasi mzawa M/S Tribe Construction Ltd na unatarajiwa kukamilika Julai mwaka huu.
Akihutubia wananchi baada ya kushuhudia utiaji wa saini mikataba ya mradi wa ujenzi wa Stendi Kuu ya Mkoa wa Arusha na Soko la Mrombo na Bustani ya Mapumziko ya Themi, Mhe. Mchengerwa amewataka viongozi kufanya maaamuzi magumu katika kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye.
Miradi hiyo ambayo inatarajia kugharimu bilioni 30.6 itakapokamilika ametaka iwe inaweza kujiendesha yenyewe na kutoa faida.
Pia amesisitiza kuilinda, na kufanya usafi ili iwezekudumu kwa muda mrefu pindi itakapokamilika.
"Jukumu letu ni kuitunza miundombinu hii itakayojengwa kwa gharama kubwa ili iweze kudumu kwa muda uliotarajiwa. Aidha, naelekeza Halmashauri zenye Miradi yenye kujiendesha kama Masoko na Stendi zihakikishe miradi hiyo inajiendesha na kuzalisha mapato kwenye Halmashauri husika." Amesisitiza Mhe. Waziri
Amemtaka mkandarasi kufanya kazi kwa haraka na kukamillisha kulingana na mkataba na mpango kazi uliokubalika ili wananchi wa Jiji la Arusha waanze kunufaika na miundombinu hiyo ambayo Serikali ya Awamu ya Sita imewekeza katika jijini Arusha.
Aidha, amemtaka mkandarasi mshauri kuhakikisha mikataba hiyo inasimamiwa kikamilifu kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi na TARURA ili ikamilike ndani ya muda uliopangwa, lakini pia katika ubora uliokubalika ili thamani ya fedha ionekane.
Pia amewaagiza Wakurugenzi wote wa Halmashauri wasimamie kikamilifu utekelezaji wa miradi hiyo kwa kutumia rasilimali watu na vifaa vilivyopo kwenye Halmashauri husika.
Waziri Mchengerwa amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikichukua hatua mbalimbali zenye lengo la kuboresha maisha ya Wananchi. Mojawapo ya hatua zinazochukuliwa ni kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji, Masoko, pamoja utunzaji wa Mazingira katika maeneo ya mijini chini ya Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Miji ya Tanzania kwa kuhusisha Ushindani ambao kitaalam unajulikana kama Tanzania Cities Transforming Infrastructure and Competitiveness (TACTIC) Project.
"Ndugu Wananchi, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi thabiti wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inatekeleza kwa vitendo falsafa ya maendeleo jumuishi. Miradi tunayoizindua leo kupitia Mradi wa TACTIC siyo miundombinu pekee bali ni daraja kati ya leo na kesho bora zaidi kwa wananchi wetu." Amesisitiza
Amesema miradi hiyo inatekelezwa kupitia Mkopo wa Benki ya Dunia utakaogharimu kiasi cha Dola za Kimarekami Milioni 410 na inatekelezwa katika miji 45 mbalimbali nchini. Lengo kuu la mradi wa TACTIC ni kuboresha usimamizi wa ukuaji wa Miji pamoja na kuziwezesha Halmashauri za Miji na Majiji kutoa huduma bora kwa wananchi.

Mhe. Mchengerwa amshukuru Rais kwa kupandisha mishahara, awataka watumishi kuchapa kazi
Na John Mapepele
Siku moja baada ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kupandisha kima cha chini cha mshahara wa watumishi wa Serikali kwa 35% Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amemshukuru na kuwaelekeza watumishi chini ya Wizara yake kuwa wazalendo na wabunifu ili kuinua uchumi wa nchi.
Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Mei 2, 2025 wakati alipokuwa akiongea na watumishi wa Mkoa wa Arusha ambapo amesema Wizara yake inasimamia takribani asilimia 76 ya watumishi wote hivyo njia pekee ya kuunga mkono maono ya Mhe. Rais ni kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
" Ndugu zangu ili tuweze kutekeleza maelekezo ya Mhe Rais wetu ni muhimu kutembea katika ndoto zake za kutaka kuwaletea watanzania maendeleo". Amesisitiza Mhe. Mchengerwa
Amesema kufuatia Rais kutoa ongezeko hilo la mshahara wa 35% Tanzania inakuwa miongoni mwa nchi pekee ambayo imewapatia wananchi wake ongezeko kubwa barani Afrika.
Aidha, amewataka wataalam wa Serikali kwenye Halimashauri zote nchini katika mabaraza ya madiwani kusukuma ajenda za maendeleo na kuonya kwa baadhi ya watumishi wasio waadilifu kubadilika mara moja kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande wa Wakurugenzi wa Halimashauri, amewataka kuendelea kusimamia miradi iliyopo kwenye maeneo yao kwa kuzingatia miongozo na sheria huku wakisahihisha makosa yaliyoainishwa ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Amewataka waongeze mifumo ya kupata taarifa za ubadhilifu na kuchukua hatua ili kuwadhibiti watumishi hao.
Amewapongeza kwa kazi nzuri ya kuongeza makusanyo na kuendelea kuminya mianya ya upotevu huku akiwataka kubuni vyanzo vipya.
Amewapongeza Wakuu wa Mikoa wote nchini kwa kuimarisha amani na kukuza uchumi kwa kusimamia vema miradi mbalimbali kwenye maeneo yao na kuwasisitiza kuendelea kufanya hivyo na kusisitiza kuwa kamwe siasa isiwe kikwazo cha kufanya maendeleo.
Pia amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda kwa ubunifu wake na kumtaka asiyumbishwe na siasa.

WAKURUGENZI WAHIMIZWA KUTENGA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA MIRADI
OR- TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amesema serikali itaendelea kusimamia Halmashauri zote nchini ili ziweze kutimiza majukumu ya msingi ya kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya kuimarisha sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Elimu.
Mhe. Katimba amesema hayo leo bungeni jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati akijibu swali la Mhe. Mwita Waitara, Mbunge wa Tarime Vijijini aliyeitaka Ofisi ya Rais – TAMISEMI kutoa muongozo kwa Halmashauri kwa mwaka wa fedha ujao ili kila Halmashauri iweke mpango wa kumaliza tatizo la meza, viti na madawati.
Akijibu swali hilo Mhe. Katimba amesema “Nitumie nafasi hii kuendelea kutoa msisitizo kwa wakurugenzi wetu wa Halmashauri zote 184 waweze kutimiza wajibu wao wa msingi wa kutenga fedha kutoka kwenye mapato ya ndani na kuweza kuziweka kwenye mipango na bajeti kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo” amesema
Katika hatua nyingine Mhe. Katimba amesema kwa mwaka wa fedha 2025/26 serikali inatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 613 pamoja na mapato ya ndani ya Halmashauri ili kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo upatikanaji wa madawati.

TARURA KUANZA KUTANGAZA ZABUNI ZA MWAKA 2025/2026
Singida
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff amewaagiza Mameneja wa Mikoa nchi nzima kuanza kutangaza zabuni za mwaka wa fedha 2025/26.
Mhandisi Seff ameyasema hayo jana alipotembelea ofisi ya Meneja wa TARURA Mkoa wa Singida pamoja na kuzungumza na Mameneja wa TARURA wa wilaya katika mkoa huo.
Amesema katika zabuni hizo zizingatie barabara zenye kipaumbele kwa wananchi na zile zenye changamoto za kupitika
Pia Mtendaji Mkuu huyo aliwasisitiza Mameneja kufanya matengenezo ya barabara kwa wakati na kuhakikisha miradi yote ya kwenye maeneo yao inaanza mapema.
Hata hivyo amewataka Mameneja wa wilaya kuandaa mipango ya kuboresha barabara kwa kuzingatia vipaumbele.
Mhandisi Seff yupo Mkoani Singida ambapo jana tarehe 1 Mei, 2025 alishiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani na kupewa zawadi ya fedha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa Mfanyakazi hodari wa TARURA kwa mwaka 2024/25.

SALUM SIMBA BINGWA MCHEZO WA DRAFTI MICHEZO MEI MOSI 2025.
OR- TAMISEMI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amemkabidhi kombe la ushindi wa mchezo wa drafti mtumishi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Salum Simba baada ya kuibuka kinara wa mchezo huo kitaifa kwa upande wa wanaume.
Ushindi huo ameupata katika Mashindano ya Michezo ya Mei Mosi 2025 baada ya kushinda mchezo wa fainali hiyo na kupeperusha vema bendera Ofisi ya Rais-TAMISEMI katika mashindano hayo.
Rais Dkt. Samia alitoa zawadi kwa mshindi huyo leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi iliyofanyika kitaifa katika uwanja wa Bombadia mkoani Singida.
Ushindi wa Simba katika mchezo hiyo unaonesha vipaji vya mchezo walivyonavyo watumishi wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

MAHUSIANO MAZURI KATI YA SERIKALI NA TAASISI ZA DINI NI CHACHU KATIKA HUDUMA BORA ZA AFYA.
OR-TAMISEMI
Mkurugenzi wa Idara ya Afya Lishe na Ustawi wa Jamii , Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume amesema mahusiano mazuri kati ya Serikali na taasisi za dini yamekuwa chachu katika kufanikisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.
Dkt. Mfaume ameyasema hayo hivi karibuni mara baada ya kutembelea katika Hospitali ya Cardinal Rugabwa inayomilikiwa na Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam katika ziara yake inayoendelea mkoani huku yenye lengo la kuangalia upatikanaji wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii.
“Hapa tunaona mitambo kikubwa ya kutolea huduma za afya, Serikali imeiweka mazingira mazuri ya ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za dini zote ikiwa ni pamoja na uwekezaji kwenye Sekta ya afya” amesema Dkt.Mfaume
Aidha, Dkt. Mfaume amezitaka timu za usimamizi wa afya (CHMT) katika Halmashauri kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na taasisi hizo kwa kuwa zinatekeleza majukumu hayo kwa niaba ya Serikali.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Sr.Dkt. Sarah Deogratius amesema ziara ya Mkurugenzi katika Hospitali hiyo imewatia moyo wa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA MAKANDARASI WA BARABARA WANAOJENGA CHINI YA KIWANGO
OR- TAMISEMI
Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI inataendelea kuwachukulia hatua wakandarasi wanaotekeleza miradi ya ujenzi wa Barabara chini ya kiwango.
Hayo yamesemwa leo Aprili 30, 2025 Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati akijibu swali la nyongeza la Mhe. Aleksia Kamguna,mbunge wa Viti maalum aliyetaka kujua serikali inawachukulia hatua gani wakandarasi wanojenga Barabara chini ya kiwango
“Serikali inapotoa nafasi ya ujenzi wa barabara hizi kwa wakandarasi inatarajia wakandarasi waweze kuzingatia mkataba wanapokuwa wanatekeleza ujenzi wa barabara hizi za wilaya na serikali inakuwa makini kusimamia viwango” amesema Mhe.Katimba
Katika swali la msingi la Mhe. Kamguna ameuliza lini Serikali itajenga barabara za Wilaya ya Malinyi kwa kiwango cha Lami
Akijibu Swali hilo Mhe. Katimba amesema “Serikali inakusudia kujenga kwa tabaka la lami barabara za makao makuu ya wilaya zote hapa nchini ikiwemo wilaya ya Malinyi na katika mwaka 2024/25”
“Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara ya Mnadani-Bomani inayoelekea Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kwa tabaka la lami (kilomita 0.85) kwa thamani ya shilingi 759,000,000.00 Mpaka sasa ujenzi bado unaendelea na umefikia 30%”. Mhe. Zainab Katimba

ZUIENI MIANYA INAYOASHIRIA UPOTEVU WA FEDHA – DKT. MFAUME.
OR-TAMISEMI
Mkurugenzi wa Idara ya Afya Lishe na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume ameuelekeza uongozi wa kituo cha afya cha Buguruni kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha katika kituo hicho ili kuendelea kuboresha miundombinu ya kituo na kufanikisha utoaji wa huduma kwa wananchi .
Dkt. Mfaume ametoa maelekezo hayo mara baada ya kutembelea na kukagua upatikanaji wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii katika kituo cha afya cha Mnazi Mmoja na kituo cha afya cha Buguruni.
“ Tunapolenga upatikanaji wa huduma za afya kwa ubora zaidi lazima tudhibiti mianya ya upotevu wa fedha na kuongeza mapato kwa kutoa huduma bora Kwa wateja wetu” amesisitiza
Aidha, Dkt. Mfaume ametaka timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya (CHMT) katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuongeza usimamizi wa fedha katika kituo vituo mbalimbali katika Halmashauri hiyo.
Pia Dkt. Mfaume ameielekeza timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya (CHMT) kushirikishana na Viongozi wa Serikali za Mitaa ili kufanikisha utoaji wa huduma chanjo Kwa Watoto katika Halmashauri hiyo.

Mchengerwa: tuulinde muungano kwa vizazi vyetu
OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa Watanzania kuuenzi Muungano kwa ajili ya kudumisha amani, umoja na udugu huku akipendekeza kuanzishwa kwa wiki maalum ya Muungano kwa shule zote nchini ili kukuza uelewa wa wanafunzi kuhusu historia ya Muungano.
Mhe.Mchengerwa ameyasema hayo katika kijiji cha Sangambi mkoani Mbeya baada ya kukagua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maendeleo yenye thamani ya Sh.bilioni 40 huku wananchi wakimpongeza Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa.
Amehamasisha wasanii na waandishi kuendeleza simulizi za mshikamano wa kitaifa ili kudumisha Muungano huku akiwaasa wazazi kuwaelimisha vijana juu ya thamani ya Muungano.
Amesisitiza kuwa Tanzania ni mfano wa amani barani Afrika, tofauti na mataifa mengine yaliyogubikwa na migogoro na kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwa wa kweli, wa kiitikadi na kimaadili, na umeleta mafanikio makubwa kwa taifa.
Waziri Mchengerwa ampongeza Rais Samia kama alama ya mafanikio ya Muungano, akisema kuwa Tanzania imekuwa ya kwanza Afrika Mashariki kumpa mwanamke nafasi ya urais, jambo ambalo hata mataifa makubwa hayajafanikisha.

Kemikali za maabara kwenye shule za sekondari kuwa za uhakika.
OR-TAMISEMI
Serikali itaendelea kuimarisha Mipango na Bajeti kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya maabara na kemikali za maabara ili kuhakikisha vinapatikana kwa uhakika na wakati kwa ajili ya ujifunzaji na kufundishia.
Haya yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Mohamed Mchengerwa wakati wa kujibu hoja za wabunge kuhusu mpango wa Serikali wa kupeleka vifaa vya maabara kwenye shule 26 za sayansi za wasichana za mikoa, bila kuathiri mipango iliypowekwa ya upelekaji wa vifaa vya maabara katika shule nyingine za sekondari nchini.
Amesema vifaa vya maabara kwa shule 486 vimenunuliwa katika awamu mbili (2) na usambazaji wa awamu ya kwanza unahusisha shule 231, zikiwemo shule 26 za sayansi za wasichana na hadi sasa shule 8 kati 26 za wasichana zimepokea vifaa hivyo na usambazaji katika shule 18 zilizobakia unaendelea.
Amesema vifaa vya maabara na kemikali kwa awamu ya pili kwa ajili ya shule 255 zilizobaki vinaendelea kupokelewa na kusambazwa na pia Serikali imenunua na kusambaza kemikali za maabara katika shule za sekondari 231 ngazi ya kata.
Kuhusu kubuni chanzo cha kudumu cha fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya maabara kwa shule za sekondari nchini, Mchengerwa amesema Serikali imekuwa ikitoa fedha za ununuzi wa vifaa vya maabara kwa shule za sekondari nchini kupitia Ruzuku ya Uendeshaji wa Shule.
Pia ununuzi wa vifaa vya maabara hufanyika kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP), Mpango wa Lipa kulingana na Matokeo (EP4R) na michango ya wadau.
Hivyo, Mchengerwa amesema Serikali itaendelea kuimarisha Mipango na Bajeti kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya maabara na kemikali za maabara ili kuhakikisha vinapatikana kwa uhakika na wakati kwa ajili ya ujifunzaji na kufundishia.
Kuhusu hoja ya usimamizi na uendeshaji wa shule za mchepuo wa kiingereza katika halmashauri, Mchengerwa amesema Ofisi ya Rais - TAMISEMI imeipokea hoja hii na itafanya uchambuzi kwa kushirikiana na Wizara inayosimamia Sera ya Elimu ili kupata utekelezaji mzuri wahojahusika.

Wakurugenzi wa halmashauri waelekezwa kuwasilisha majina ya watumishi wanaodai malimbikizo
OR-TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amewaelekeza wakurugenzi wa Mamlaka za serikali za mitaa kutengeneza mchanganuo na kubaini watumishi wangapi wanadai malimbikizo ya mishahara na yasiyo yamishahara na kuyawasilisha Utumishi kuhakikiwa na kupekwa hazina kwaajili ya malipo.
Ameyatoa maelekezo hayo bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Bonnah Kamoli mbunge wa Segerea kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa, aliyetaka kujua serikali inampango gani wa kulipa malimbikizo ya mishahara na marupurupu ya walimu.
Akijibu hilo Mhe. Katimba amesema “Naomba nitoe msisitizo huo na jana kwenye bajeti ya wizara ya utumishi maelekezo hayo yalitolewa na wizara hiyo na mpaka itakapo fika tarehe 31 Mei wakurugenzi wote wawe wamewasilisha majina hayo ya watumishi hao ambao wanadai malipo yao” Amesema
Aidha, akijibu kuhusu mazingira bora ya walimu Mhe. Katimba amesema serikali inaendelea kujenga nyumba za walimu ili walimu wapate mazingira mazuri ya kuishi na kufanyakazi kwa ufanisi.

Serikali kudhibiti madeni mapya ya watumishi
OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Mohamed Mchengerwa amesema Serikali imeendelea kudhibiti uzalishaji wa madeni mapya ya kimshahara na yasiyo ya kimshahara.
Mchengewa ameyasema hayo wakati wa kujibu hoja kuhusu Serikali kulipa kwa wakati madeni mbalimbali ya watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini ili kuondoa malimbikizo ya madeni.
Amesema Serikali imeendelea kulipa madeni ya watumishi wa mamlaka za serikali za mitaa na katika mwaka 2023/24 Shilingi bilioni 116.08 zimetolewa kwa ajili ya kulipa madeni ya watumishi ambapo, mishahara ni Shilingi bilioni 32.22 na madeni yasiyo ya mishahara ni shilingi bilioni 83.85.
Amefafanua kuwa katika mwaka 2024/25 hadi machi, 2025 madeni yenye thamani ya Shilingi bilioni 78.75 yamelipwa, kati yake Sh bilioni 16.32 ni madeni ya mshahara na shilingi bilioni 62.43 ni madeni yasiyo ya mshahara yanayojumuisha fedha za uhamisho, likizo na stahiki za watumishi.
Mchengerwa amesema katika kuendelea kuhakikisha madeni yanaendelea kulipwa, Ofisi ya Rais-TAMISEMI kupitia Ofisi za Wakuu wa Mikoa imekamilisha zoezi la uhakiki wa madeni ya watumishi yasiyo ya mishahara kufikia juni 2024 ambapo Halmashauri 36 zimeonekana zinaweza kulipa zenyewe kutokana na mapato yao ya ndani na 145 hazina uwezo.
“Taarifa ya uhakiki imewasilishwa Wizara ya Fedha kwa ajili ya kuendelea na hatua zinazofuata.”amesema Mchengerwa
Aidha, Mchengerwa amesema Serikali imedhibiti uzalishaji wa madeni mapya ya kimshahara kwa kuingiza kwa wakati watumishi wote wanaoajiriwa kwa mara ya kwanza katika payroll ya Serikali, kuhakikisha marekebisho ya mishahara yanafanyika kabla ya mtumishi kupata barua ya kupanda daraja na kuingizwa kwenye payroll ya Serikali posho za watumishi wanaokaimu madaraka.
Pia katika kudhibiti uzalishaji wa madeni yasiyo ya kimshahara Serikali imeyadhibitiwa kwa kutoa ruzuku kwa ajili ya gharama za likizo, uhamisho na stahiki za viongozi.

Bunge lapitisha kwa kishindo bajeti ya tamisemi trilioni 11.78 kwa mwaka 2025/2026
Na Mwandishi Wetu, bungeni Dodoma
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepitisha kwa kauli moja bajeti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mwaka wa fedha 2025/26 yenye takribani Shilingi trilioni 11. 783 kwa ajili ya wizara na taasisi zilizo chini yake.
Kwa mujibu wa Waziri Mchengerwa Bajeti hiyo imeongezeka kutoka Shilingi trilioni 10.125 zilizotengwa mwaka 2024/25 hadi kufikia Shilingi trilioni 11.783 na kuwa na ongezeko la zaidi ya Sh trilioni 1.66.
Shilingi trilioni 3.95 zimepitishwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo ambapo kati ya fedha hizo Shilingi trilioni 2.5 ni fedha za ndani, ikijumuisha Shilingi bilioni 613.44 za mapato ya ndani ya halmashauri na Shilingi trilioni 1.45 ni fedha za nje.
Pia Shilingi trilioni 7.84 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida yanayojumuisha mishahara Shilingi trilioni 6.3 na matumizi mengineyo Shilingi trilioni 1.53 ikijumuisha Shilingi trilioni 1. 067 za mapato ya ndani ya halmashauri.
Akijibu hoja za wabunge Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe Mohamed Mchengerwa amesema kuwa anatambua uwepo wa changamoto za ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara katika maeneo mbalimbali nchini. Katika kushughulikia changamoto hiyo serikali imeendelea kutenga fedha kupitia TARURA kwa ajili ya ujenzi, matengenezo na ukarabati wa Barabara ambapo bajeti imeongezeka kutoka shilingi bilioni 275.00 mwaka 2020/21 hadi shilingi bilioni 772.19 mwaka 2024/25 sawa na ongezeko la asilimia 180.8 ya fedha za ndani.
Pia Waziri Mchengerwa amesema kuwa Ofisi ya Rais - TAMISEMI inatambua umuhimu wa kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia ambapo imeendelea kujenga na kukarabati miundombinu ya elimu pamoja na kuendeleza mazingira ya maeneo hayo.
Serikali imeendelea kuwekeza katika utoaji wa Elimumsingi na Sekondari ambapo Mpango wa Elimumsingi bila Ada umeongezewa bajeti yake kutoka shilingi bilioni 249.66 mwaka 2020/21 hadi shilingi bilioni 510.96 mwaka 2025/26 kwa mwaka sawa na ongezeko la shilingi bilioni 261.30 sawa na asilimia 104.66.
Waziri Mchengerwa ametoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa na Wilaya: kujikita kikamilifu katika kulinda amani, mshikamano wa kitaifa na ufanisi wa utendaji wa serikali katika maeneo yao.
”Hamtakiwi kuwa watazamaji wa migogoro—bali wazima moto wa chokochoko, na walinzi wa misingi ya haki, maendeleo na umoja wa kitaifa” Amesisitiza Waziri Mchengerwa
Na kuongeza kuwa Utulivu wa nchi unaanza pale ambapo viongozi wa chini wanatimiza wajibu wao bila kusubiri maagizo kutoka juu.

Wabunge waitaka wizara ya fedha iipe fedha wizara ya tamisemi itekeleze majukumu yake
Na Mwandishi wetu, Dodoma
WABUNGE mbalimbali wameipongeza Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ufanisi wao ambao wamekuwa wakiufanya katika kuhakikisha miundombinu, elimu, afya na mambo mengine yanafanyika kwa ustadi mkubwa.
Akichangia bungeni bajeti ya TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Mhe Timotheo Mnzava amesema kuwa anakubaliana na kazi kubwa ambayo imekuwa ikifanywa na TARURA huku akisema kuwa wanmaiomba wizara ya fedha iwapelekee TAMISEMI, Tarura fedha ili waweze kutatua changamoto zilizopo.
“Tunaipongeza serikali kwa kipindi cha miaka minne mitano tumefanya kazi kubwa sana na serikali imeleta fedha nyingi sana kuunga mkono ujengaji wa maboma ya madarasa na zahanati” Amekaririwa Mnzava
Naye Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mhe Hamis Tabasam amesema kuwa serikali za mitaa imebeba maslahi makubwa ya wananchi na kusema kuwa sengerema walikuwa wana matatizo ya shule za sekondari, shule za msingi Barabara na hata huduma za afya.
“Lakini katika kipindi hiki cha miaka minne Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa kuhakikisha huduma za kijamii katika nchi hii zinaboreshwa kwa kiwango kikubwa”amesema.
Jambo hili linatutolea hofu kwa sisi wabunge hakuna mbunge ambaye atakuwa na mashaka yakutokuchaguliwa jimboni kwake labda kama anahali mbaya damu zimechafuka tu maana kila kitu kipo vizuri kwa sasa.
Hata hivyo naye Mbunge wa jimbo la Nyamagana Mhe Stansilaus Mabula amesema kuwa kumekuwa na utulivu wa kiwango cha hali ya juu wizara ya TAMISEMI tangu alipoteuliwa Waziri Mhe Mohammed Mchengerwa .
Tunaposema hakuna kilichosimama hakika tunamaanisha kwasababu yote yanayojitokeza ni mambo ambayo yamejitokeza kwa muda mfupi na yameleta tija kwa watanzania.
“Tunapozungumzia uboreshaji wa sekta ya elimu msingi na sekondari namna ambavyo shule za msingi na sekondari zimeboreka.
Leo tunapozungumza kwenye uboreshaji wa shule za msingi zinazozingatia takwa maalum la Watoto wadogo (kindergarten) kupata eneo la kujifunzia hili nijambo kubwa sana na lenye tija katika nchi yetu.

Mchengerwa- marc, madc imsiwe watazamaji wa migogoro
OR-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa maelekezo mahususi kwa wakuu wa mikoa na wa wilaya akiwataka kutokuwa watazamaji wa migogoro na walinzi wa misingi ya haki na amani.
Mchengerwa ameyasema hayo wakati akihitimisha hoja ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI na taasisi zake, Tume ya Utumishi wa Walimu, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024/25.
“Ninapenda pia kutumia nafasi hii kutoa maelekezo mahsusi kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya, wajikite kikamilifu katika kulinda amani, mshikamano wa kitaifa na ufanisi wa utendaji wa serikali katika maeneo yao.”
“Hamtakiwi kuwa watazamaji wa migogoro bali wazima moto wa chokochoko, na walinzi wa misingi ya haki, maendeleo na umoja wa kitaifa. Utulivu wa nchi unaanza pale ambapo viongozi wa chini wanatimiza wajibu wao bila kusubiri maagizo kutoka juu.” amesema Mchengerwa
Amewataka kuwasha mwenge wa ulinzi wa jamii na kuzima cheche za migogoro midogo inayoweza kuwa moto mkubwa wa Taifa.

Bil. 66.57/- kujenga matundu ya vyoo 28,580
OR-TAMISEMI
KATIKA mwaka 2025/26, Serikali imetenga Sh.Bilioni 66.57 kwa ajili ya kujenga matundu 28,580 ya vyoo katika shule za msingi na sekondari.
Akijibu hoja ya wabunge kuhusu serikali kufanya tathimini ya kubaini ubora na ukubwa wa tatizo la upungufu wa matundu ya vyoo katika shule zote za msingi na sekondari, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema Serikali inatambua umuhimu wa kulinda afya za walimu na wanafunzi, hivyo itaendelea kukabiliana na changamoto hiyo kwa lengo la kulinda utu na afya za wanafunzi.
Amesema Sensa ya Elimumusingi ya mwaka 2024 inaonesha mahitaji ya matundu ya vyoo katika shule za msingi ni 429,599 wakati yaliyopo ni matundu 240,320, hivyo kuwa na upungufu kuwa ni matundu 189,279, hivyo kufanya wastani wa uwiano kwa wavulana ni 1:47 badala ya 1:25 unaohitajika na kwa wasichana kuwa ni 1:43 badala ya 1:20.
Kwa upande wa sekondari, mahitaji ni matundu 135,870 wakati yaliyopo ni matundu 84,608 na upungufu ni matundu 51,262, hivyo kufanya wastani wa uwiano uliopo kwa wavulana ni 1:36 badala ya 1:25 na wasichana ni 1:35 badala ya 1:20.
Aidha, Mchengerwa amesema mkakati wa Serikali ni kufanya tathmini ya ubora wa ujenzi wa matundu ya vyoo na kuendelea kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo kwa shule za msingi na sekondari na kuhakikisha kuwa kwa sasa kila darasa linalojengwa kunakuwa na ujenzi wa angalau matundu mawili ya vyoo.
“Katika mwaka 2025/26, Serikali imepanga kujenga matundu 28,580 ya vyoo yatakayogharimu shilingi bilioni 66.57 katika shule za msingi na sekondari.”
Mchengerwa ameongeza kuwa: choo cha staha ni haki ya mwanafunzi; ni chozi lisiloonekana, lakini lenye kuumiza.”
“Tuwashe mwenge wa heshima shuleni-tuzime giza la aibu ya vyoo visivyofaa...Serikali haijalala katika hili, lengo ni kuhakikisha shule zetu zinakuwa mahali salama pa fundishia na kujifunzia," amesema.

Wananchi dodoma waipa heko bajeti ya tamisemi
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Ikiwa leo ni siku ya mwisho ya kujadiliwa kwa bajeti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wananchi mkoani Dodoma wamejitokeza kutoa maoni yao kuhusu bajeti hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026 yenye kiasi cha shilingi bilioni 11.7.
Akizunguzmia bajaeti hiyo mkazi wa Dodoma Bi Maria Julias ambaye pia ni fundi cherehani amesema kuwa anatamani bajeti ya TAMISEMI ilenge zaidi kwenye TEHAMA ambapo itawarahisishia wafanyabiashara kwani dunia ipo kiganjani hivyo inawarahisishia wafanyabiashara kujitangaza kupitia mitandao ya kijamii.
“Mfano mimi nikishona nguo zangu huwa naweka kwenye mitandao ya kijamii kwahiyo natumai tamisemi itatusaidia kwa upande huo”amesema Maria
Kwa upande wake Emmanuel Mabalwe amesema kuwa amefuatilia Bunge na kuona bajeti ya Tamisemi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 iliyowasilishwa na Waziri wa TAMISEMI Mhe Mohammed Mchengerwa.
Amesema kuwa bajeti ya mwaka huu ya Tamisemi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 imekuwa na ongezeko kwa kiasi kikubwa kutoka bajeti ya mwaka jana 2024/2025 ambayo ilikuwa ya tril.10.1 hadi kiasi cha tril 11.7
“Kwahiyo ongezeko ni kubwa ambapo Trilioni 1.66 ndiyo ambayo imeongezeka kwa mwaka huu na hiki ni kiwango kikubwa ambacho kitaenda kuhudumia watanzania” Amesema.
Naye Manoa Samweli amesema bajeti ya TAMISEMI ijikite kwenye masuala ya michezo kwani mpaka sasa michezo imekuwa ajira kwa vijana wengi ambao wana kipaji.
Amesema mchezo wa mpira wa miguu lunazidi kukua hivyo inatakiwa kuwepo na maboresho zaidi hasa kwenye miundombinu ya michezo kama vile viwanja jambo litakalosaidia kuweka ajira na kupata ajira kwa vijana ambao wana vipaji vya mpira.

Wazee rufiji wamuombea dua waziri mchengerwa
OR-TAMISEMI
Wazee Wilayani Rufiji wamefanya Dua ya kumuombea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa ya kumtakia heri katika utekelezaji wa majukumu yake ya kitaifa pamoja na jukumu la kuijenga Rufiji kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo
Dua hiyo imefanyika katika Msikiti Mkuu wa Jumuiya ya Ikwiriri na Mitaa mbalimbali ya Ikwiriri, ambapo wananchi wa Rufiji wamepata fursa ya kuwaombea waliotangulia mbele za haki, kuliombea Taifa liendelee kuwa na amani na utulivu, pamoja na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na viongozi aliwateua ili waendelee kulitumia taifa kwa uzalendo.
Wakizungumza katika Mahojiano Maalumu Wazee hao, akiwemo Daruesh Rwanda Mkazi wa Ikwiriri amesema Dua imelenga kumuombea Mhe. Mchengerwa kwasababu ameleta maendeleo, amani na utulivu ndani ya Rufiji.
"Ametuletea maendeleo na ametutengenezea amani, sasa hivi wafugaji wapo sehemu yao na sisi tupo sehemu yetu hivyo maisha mazuri yanaendelea" amesema Rwanda.
Kiongozi wa Al Qadiri ya Wilaya ya Rufiji, Yusufu Kinjogo amempongeza Waziri Mchengerwa kwa namna alivyoiletea Rufiji maendeleo ambayo yameleta mabadiliko ya kifikra kwa wananchi.
"Tunamshukuru kwa kuibadilisha Rufiji, Rufiji ya leo imebadilika kwani mitaa yote imewekwa lami, Mungu ampe afya njema ili aendelee kuwatumikia wananchi," amesema Kinjojo.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amewashukuru wote waliandaa Dua hiyo ya kumuombea, kuwaombea Viongozi waliotangulia mbele za haki, kuliombea Taifa pamoja na viongozi wa Serikali ambao wanaongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"Nawashukuru sana wazee wa Rufiji, leo tumewakumbuka wazee wetu waliotangulia mbele za haki, tumemkumbuka Mtume wetu Mohamed (S.A.W), tumemuombea Mhe. Rais na viongozi aliowateua katika nafasi mbalimbali na tumeiombea Rufiji ili iendelee kupata maendeleo," Amesema Mhe. Mchengerwa.

Tamisemi yazielekeza halmashauri zenye uwezo kuajiri watumishi wa mikataba
Na. James K. Mwanamyoto OR-TAMISEMI
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Festo Dugange, amezitaka halmashauri zenye uwezo wa kiuchumi kuajiri watumishi wa mikataba ili kutatua changamoto ya upungufu wa watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa
Dkt. Dugange ametoa maelekezo hayo kwa wakurugenzi wa halmashauri nchini, wakati akifunga mkutano wa 15 wa Taasisi ya Maboresho ya Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) uliofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliopo kwenye Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
“Ofisi ya Rais-TAMISEMI ilitoa mwongozo maalum wa namna ya kuajiri watumishi wa mikataba na hususani wa sekta ya elimu na afya, hivyo Makatibu Tawala wa Mikoa kawasimamieni Wakurugenzi wa Halmashauri kutekeleza mwongozo huo,” Dkt. Dugange amesisitiza.
Dkt. Dugange amesema, Serikali imeleta fedha nyingi katika halmashauri ambazo zimejenga zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya na shule na inaendelea kuajiri kwa awamu, hivyo halmashauri zinazokusanya mapato ya kutosha zinapaswa kuajiri watumishi wa mikataba ili waweze kutoa huduma kwa wananchi kupitia mbiundombinu hiyo iliyojengwa na Serikali.
Aidha, Dkt. Dugange amehimiza kuwa, siku zote Ofisi ya Rais-TAMISEMI inaamini watumishi wote waliochini ya TAMISEMI wakifanya kazi kwa bidii na ufanisi, ni dhahiri kwamba kiwango cha utendaji kazi wa Serikali kitakuwa ni zaidi ya asilimia tisini kwani majukumu yanayotekezlezwa na TAMISEMI yanawagusa wa Tanzania wengi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bi. Beatrice Kimoleta amesema kuwa, TAMISEMI itaendelea kushirikiana na Taasisi ya Maboresho ya Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) ili iweze kuwa imara na kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Tamisemi yakusanya tril.1.11/-
OR-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema hadi Machi, 2025 Sh.Trilioni 1.11 zimekusanywa sawa na asilimia 93.15 ya lengo la kukusanya Sh.Trilioni 1.60 kwa Mwaka 2024/25.
Akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka 2025/26, Waziri Mchengerwa amesema kati ya fedha hizo Sh.Tilioni 61.21 ni kodi ya majengo, Sh. Trilioni 1.04 ni mapato ya ndani ya mamlaka za serikali za mitaa.
Pia, amesema Sh.Bilioni 16.23 ni mapato ya ndani ya taasisi na Sh.Milioni 201.60 ni maduhuli ya mikoa.
Amefafanua kuwa makusanyo hayo yalitokana na ada za wanachuo, tozo, ukusanyaji wa madeni, mauzo ya bidhaa mbalimbali na ushuru unaotozwa na mamlaka za serikali za mitaa kulingana na Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura 290.
Mh.Mchengerwa amesema kwa kipindi hicho TAMISEMI ilipanga kutumia Sh.Bilioni 541.27 za mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya kuchangia utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Hadi Machi, 2025 Sh.Bilioni 312.30 sawa na asilimia 57.70 zimetolewa.
Ameeleza kuwa baadhi ya miradi iliyotekelezwa kwa kipindi hicho ni ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya, ujenzi wa barabara, machinjio, minada nyumba za walimu na watumishi wa afya, hospitali, vituo vya afya, zahanati, vituo vya polisi, ununuzi wa magreda

Mhe. mchengerwa atoa maagizo mahususi kwa marc na maded
OR TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tamisemi Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa amewaelekeza Wakuu wote wa mikoa kuwasimiamia Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuzingatia vipaumbele vya mwaka 2025/26 kikamilifu.
Waziri Mchengerwa ametoa maelekezo hayo leo Aprili 16, 2025 wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara na taasisi zake kwa mwaka 2025/26.
Amesema vipaombele vya kuzingatia ni kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unafikia malengo na kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya afya ya msingi, elimu ya msingi na sekondari kulingana na mipango iliyowekwa.
Mhe. Mchengerwa amewaataka kuzingatia kusimamia utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Uchumi wa Kidigitali ikiwemo uwekaji na matumizi ya mifumo na miundombinu ya TEHAMA katika mikoa na mamlaka za serikali za mitaa ikiwa ni pamoja na vituo vya huduma za afya na elimu.
Vilevile amewaagiza kuhakikisha mapato katika mikoa na mamlaka za serikali za mitaa yanakusanywa kupitia mifumo ya TEHAMA ya Serikali pamoja na kufanya ufuatiliaji wa karibu wa mifumo hiyo ili kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.
Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema Mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha inatekeleza Mikakati ya Uchumi wa Buluu, nishati safi ya kupikia na mabadiliko ya tabianchi na utunzaji wa mazingira.
Ameiagiza mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kuendelea kuimarisha mifumo stahimilivu na endelevu ya utoaji wa huduma bora za afya, ustawi wa jamii na lishe ili kuboresha huduma ambayo ni nguzo muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote
Pia, amewataka wakuu wa mikoa na wakurugenzi kuhakikisha watoto walio chini ya miaka mitano wanajiunga kwenye vituo vya jamii vya kulelea watoto wadogo mchana.
“Kila halmashauri itapimwa utekelezaji wa vipaumbele hivi kwa kuzingatia miradi iliyotengewa bajeti kwa Mwaka 2025/26.

Tamisemi yaomba trilioni 11.78 bajeti 2025/2026
OR-TAMISEMI
OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imewasilisha bungeni makadirio ya mapato kwa mwaka 2025/26 yenye takribani Shilingi trilioni 11. 783 kwa ajili ya wizara na taasisi zilizo chini yake.
Bajeti hiyo imeongezeka kutoka Shilingi trilioni 10.125 zilizotengwa mwaka 2024/25 hadi kufikia Shilingi trilioni 11.783 na kuwa na ongezeko la zaidi ya Sh trilioni 1.66.
Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa iamesema Shilingi trilioni 3.95 zinaombwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo ambapo kati ya fedha hizo Shilingi trilioni 2.5 ni fedha za ndani, ikijumuisha Shilingi bilioni 613.44 za mapato ya ndani ya halmashauri na Shilingi trilioni 1.45 ni fedha za nje.
Pia amesema Shilingi trilioni 7.84 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida yanayojumuisha mishahara Shilingi trilioni 6.3 na matumizi mengineyo Shilingi trilioni 1.53 ikijumuisha Shilingi trilioni 1. 067 za mapato ya ndani ya halmashauri.
“Tumewasilisha si tu makadirio ya mapato na matumizi, bali tumeweka mbele yetu dira ya matumaini, ramani ya maendeleo na ahadi ya uongozi unaowajibika. TAMISEMI haitafuti sifa ya kisiasa, tunatafuta suluhisho sahihi kwa maisha ya mtanzania wa kawaida.”
Aidha, Mchengerwa ametoa wito kwa mikoa, mamlaka za serikali za mitaa na wananchi wote kushirikiana, kusonga mbele kwa mshikamano.
“Kwa dhamira hii, na kwa imani kubwa katika maono ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunawasilisha bajeti hii kama zana ya kazi, dira ya matumaini na silaha ya mapinduzi ya kiutawala, kiuchumi na kijamii.”
“Kwa hiyo, tunasema kwa ujasiri mkubwa, TAMISEMI, ndiyo msingi wa maendeleo endelevu. Kila Shilingi ina Jukumu, Kila Kiongozi ana Wajibu na Kila Mwananchi ana Nafasi!”

Tamisemi yapongezwa na benki ya dunia kwa utekelezaji mzuri ujenzi wa miundombinu kupitia mradi wa sequip
Na OR TAMISEMI
Benki ya Dunia imeipongeza Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa ujenzi wa shule mpya zilizojengwa kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari SEQUIP ambao umepunguza umbali kwa wanafunzi kufuata elimu suala ambalo lilikuwa likiwakatisha masomo yao hasa jinsia ya kike.
Pongezi hizo zimetolewa na Huma Kidwai Mtaalamu wa Elimu kutoka Benki ya Dunia ambaye ni Mtaratibu wa Mradi wa SEQUIP kwa niaba ya Benki ya Dunia baada ya kutembelea shule ya Sekondari ya Amali ya Katerero iliyoko katika Halmashauri ya Bukoba ambayo imejengwa kupitia mradi huo katika Mkoa wa Kagera.
Akisistiza umahiri wa wanafunzi katika shule hizo mpya, Kidwai amewashauri Wakuu wa shule hizo kujifunza mbinu mpya kwa shule Kongwe na kuwa wabunifu ili kuzalisha wanafunzi bora na mahiri.
Akizungumza kwa niaba ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mratibu wa Mradi wa SEQUIP Richard Makota amesema shule hizo zilizojengwa zinalenga kuwasaidia wanafunzi kupata elimu kwa vitendo na nadharia kutokana na miundombinu iliyowekwa hasa kwa masomo ya Sayansi.
Aidha, Ferdinand Eladius Mkuu wa shule ya Sekondari ya Amali ya Katerero akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake amesema uwepo wa shule hiyo umewasaidia wanafunzi kupenda masomo kutokana na upekee wa miundombinu iliyopo

Majaliwa: toa iwe sehemu ya mabadiliko chanya kwenye serikali za mitaa
OR - TAMISEMI
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ameeleza uimarishaji wa Taasisi ya Maboresho ya Mamlaka za Serikali za Mitaa(TOA) ili iwe na nguvu na iweze kuishauri Serikali ipasavyo.
Majaliwa ametoa maagizo hayo leo Aprili 14, 2025 wakati akifungua mkutano wa 15 wa TOA unafanyika katika Ukumbi wa Jiji mkoani Dodoma.
Amesema viongozi wa Kitaifa wanaitaka taasisi hiyo kuwa sehemu ya mabadiliko chanya ya mwelekeo wa utendaji ili ichagize maboresho katika Serikali za Mitaa.
”Endeleeni kuhimiza wanachama kufanya kazi kwa weledi na uzalendo ili kuleta matokeo yanayotarajiwa na wananchi.”
“Kwa kuzingatia ukaribu na ushirikiano wenu na wananchi, naamini mnazitambua changamoto zinazowakabili na mnaelewa afua ambazo zikitekelezwa zitawaletea maendeleo. "
Aidha, Mhe. Majaliwa amesema Serikali imesimamia matumizi ya mifumo ya kieletroniki ili kuimarisha ufanisi, uwazi na uwajibikaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Mifumo hiyo ni pamoja na Mifumo ya Uhasibu, Mifumo ya ukusanyaji wa mapato, Manunuzi na Malipo.
"Matumizi ya Mifumo yamesaidia kupunguza urasimu, kurahisisha ulipaji wa malipo na kodi mbalimbali za Serikali na kuboresha ukusanyaji wa mapato hadi kufikia ukusanyaji wa zaidi ya shilingi bilioni 900."
Pia ametumia fursa hiyo kuagiza uongozi wa TOA uwajibike kuhamasisha Mamlaka za Serikali za Mitaa kutanua wigo wa mapato ili kuongeza uwezo wa kujitegemea kimapato na kugharamia shughuli mbalimbali za uendeshaji na utoaji wa huduma.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amewataka viongozi wote wa Mikoa na watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini, waendelee kusimamia maadili na uzalendo, mifumo ya ukusanyaji wa mapato pamoja na mifumo mingine yote iliyoanzishwa na Serikali kwenye ngazi zao.
Pia amewahimiza kusimamia kikamilifu matumizi ya fedha za umma pamoja na utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kusisitiza kuwa Serikali chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan umekuwa na ufanisi zaidi katika Serikali za Mitaa.
Awali, Mwenyekiti wa Taifa wa Taasisi ya Maboresho ya Serikali za Mitaa Tanzania, Albert Msovela alisema wataendelea kusimamia taasisi hiyo na kuhakikisha wanatekeleza shughuli zote za Serikali kwa weledi na ufanisi mkubwa.

Serikali ya kuendelea kujenga miundombinu ya maji shuleni.
Naibu Waziri ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange amesema Serikali ina mikakati ya kuendelea kujenga miundombinu ya maji shuleni katika kila bajeti ya fedha ili kuepuka milipuko ya magonjwa na pamoja na kuhakikisha kuwa Ujenzi wa miundombinu ya vyoo unaojumuisha wa miundombinu ya maji tiririka.
Mhe. Dkt Dugange ameyasema hayo wakati wa akijibu swali Mbunge wa Viiti Maalum Mhe Minza Simon Mjika katika kipindi cha maswali na majibu aliyeuliza “Je, Serikali ina mpango gani kujenga miundombinu ya maji shuleni ili kuepuka milipuko ya magonjwa?” katika Bunge la bajeti linaloendelea Jijini Dodoma.
“shule 5,311 za Sekondari zina vyanzo vya maji vya uhakika ambapo shule zenye maji ya bomba ni 2,960, visima shule 1,217 na wanaovuna maji ya mvua ni shule 1,134. Aidha, shule 20,509 za msingi zina vyanzo vya maji ya uhakika ambapo shule zenye maji ya bomba ni 10,965, visima shule 4,966 na shule zinazovuna maji ya mvua ni 4,578.” Amesisitiza.
Amesema pia, Serikali imetoa maelekezo kwa miradi yote ya ujenzi ya vitio vya afya na ujenzi wa shule mpya utajumuisha miundombinu ya maji inayohusisha kuvuna maji ya mvua, kuunganisha na mifumo ya Mamlaka za Maji na kuchimba visima.

Mchengerwa: zoezi la upandaji miti kuwapima wakuu wa wilaya na wakurugenzi
OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema utekelezaji wa agizo la upandaji wa miti lililotolewa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, ni sehemu kipimo cha utendaji kazi wa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya.
Waziri Mchengerwa amesema hayo, wakati wa hafla ya kutoa tuzo kwa washindi wa shindano la upandaji miti shuleni ilioyofanyika katika shule ya Sekondari Mwambisi Forest iliyopo wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Mhe. Mchengerwa amesistiza kuwa, maelekezo ya Makamu wa Rais ni amri hivyo yatakuwa ni sehemu ya kipimo cha utekelezaji wa majukumu ya Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala wa Wilaya pamoja na wasaidizi wao.
“Kaimu Katibu Mkuu peleka maelekezo yangu haya mahususi kwenye sekretarieti zote za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa ili agizo la kupanda miti litekelezwe,” Waziri Mchengerwa amesisitiza.
Aidha, Mhe. Mchengerwa amewapongeza walimu pamoja na wanafunzi wa shule zote tatu ambazo zimeibuka washindi katika shindano la upandaji miti lililoratibiwa na benki ya NMB.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Benki ya NMB ambaye ni Afisa Mkuu wa Fedha Bw. Juma Kimori, ametangaza washindi katika kampeni hiyo ya upandaji wa miti ambapo Shule ya Sekondari Mwambesi Forest imeibuka mshindi wa kwanza, Shule ya Msingi Ibondo imekuwa ya pili na ya tatu ni Shule ya Sekondari Itimbo.
Benki ya NMB imetoa zawadi ya shilingi milioni 50 kwa mshindi wa kwaza, milioni 30 kwa mshindi wa pili na milioni 20 kwa mshindi wa tatu.

Wakandarasi 457 wa ujenzi wa barabara walipwa, wengine 322 kulipwa hivi karibuni
OR-TAMISEMI
Serikali imelipa madeni ya wakandarasi 457 wa ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara waliokuwa wakidai baada ya kutekeleza mikataba yao kwa kiwango kinachostahili malipo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa ameyasema hayo jijini Dodoma akifungua semina ya mafunzo elekezi kwa wakandarasi wazawa kuhusu matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa 'Samia Infrastructure Portal' unaolenga kuwawezesha kuomba fedha kwa ajili ya kuimarisha mitaji yao katika miradi ya barabara chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA).
Waziri Mchengerwa amesema hadi kufikia Aprili 9, 2025, wakandarasi hao walikuwa tayari wamelipwa, huku malipo ya wakandarasi wengine 322 yakiwa mbioni kukamilika.
“Hadi kufikia Aprili 11, 2025, Wakandarasi hawa 322 watakuwa wamelipwa na TARURA, maelekezo yangu kwenu TARURA ni kuhakikisha fedha ambazo tayari mmepokea zinagawiwa kwa haraka, kwa usawa na bila upendeleo, watu wapewe haki zao."
“Wakandarasi waliopo katika kanda zote nchini wafikirieni kwa usawa kutokana na kiasi tulichokipokea kutoka Wizara ya Fedha. Keshokutwa mnipe taarifa ya mgawanyo wa fedha hizo kama tulivyokubaliana,”amesema.
Kuhusu semina hiyo maalum ya elimu ya bidhaa ya kifedha iliyoandaliwa kwa ajili ya wakandarasi wazawa, watumishi wa TARURA, na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Waziri Mchengerwa amesema ni fursa muhimu kwa pande zote kupata uelewa wa kina juu ya utaratibu wa bidhaa lengwa, majukumu ya kila upande, na namna ya kusimamia mchakato huo kwa uwazi na ufanisi.
Awali, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba amesema kuanzishwa kwa hatifungani ya miundombinu ya Samia ni utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mchengerwa na ni moja ya alama muhimu atakazoziacha katika ofisi hiyo, ikionesha namna alivyotekeleza kwa vitendo dira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwekeza katika miundombinu na kuwawezesha wakandarasi wazawa.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Idara ya Mikopo wa Benki ya CRDB, Xavery Makwi, amesema hatifungani hiyo ya Samia imewezesha kukusanywa zaidi ya Sh. bilioni 300 ambazo zitawasaidia wakandarasi wazawa kutekeleza kandarasi zao kwa uhakika, tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali.

Mchengerwa: Wakurugenzi, msiwaondoe Waganga Wafawidhi kwa matakwa yenu
OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa, amewaelekeza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha kuwa hawaondoi Waganga Wafawidhi wa vituo vya afya ngazi ya msingi kwa maamuzi ya hiari au kwa utashi binafsi. Badala yake wazingatie taratibu rasmi za kiutumishi na kinidhamu kwa mujibu wa miongozo iliyowekwa.
Mhe. Mchengerwa ametoa agizo hilo alipokuwa akihitimisha mkutano wa mwaka wa Waganga Wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi, uliofanyika jijini Dodoma kwa muda wa siku mbili ambao umewakutanisha wataalamu wa afya kutoka ngazi mbalimbali kwa ajili ya kujadili fursa, changamoto na masuala ya kitaaluma yenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma katika ngazi ya msingi.
Katika hotuba yake, Waziri Mchengerwa amesisitiza:
“Ninawataka Wakurugenzi watumie vigezo vya kupima utendaji au ubora wa kazi za Waganga Wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya msingi—yaani Key Performance Indicators (KPI)—na si maamuzi ya mtu mmoja mmoja, nadhani nimeeleweka vizuri,”amesema.
Agizo hilo la Waziri limekuja kufuatia malalamiko kutoka kwa baadhi ya Waganga Wafawidhi waliodai kuwa wamekuwa wakiondolewa kwenye nafasi zao kwa hila, kinyume na sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma.

Mkoa wa Iringa washika mkia matumizi ya Mfumo wa GoTHOMIS.
Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume, amewataka Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya Msingi kuweka mikakati yenye tija kukabiliana na dosari mbalimbali zinazokwamisha vituo vyao katika matumizi ya mifumo inayobuniwa na OR – TAMISEMI kwa lengo la kurahisisha na kuboresha utolewaji wa huduma za afya kwa wananchi.
Dkt. Mfaume ametoa agizo hilo wakati akihoji sababu za baadhi ya mikoa kushika nafasi ya mwisho kwenye matumizi ya mfumo ulioboreshwa wa usimamizi na uendeshaji wa vituo vya kutolea huduma za afya ya ngazi ya msingi wa ukusanyaji wa taarifa na mapato wa GOTHOMIS wakati wa mkutano wa mwaka wa waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi, unaonedelea katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa Dkt. Mfaume, licha ya mkutano huo kuwa fursa ya kujadiliana juu ya changamoto, mafanikio na masuala kadha ya kitaaluma juu ya kada hiyo lakini pia mkutano huo unatumika kupima utendaji kazi wa waganga wafawidhi ili kuboresha utendaji kazi wao na kuondoa dosari mbalimbali zinazotatiza utolewaji wa huduma bora kwa wananchi.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Mkurugenzi wa idara ya TEHAMA OR – TAMISEMI Bw. Erick Kitali juu ya utendaji kazi wa mikoa kupitia mfumo wa GOTHOMIS mpaka kufikia mwezi Aprili mwaka 2025, mkoa wa Ruvuma, umeibuka kinara ukifuatiwa na Songwe, Mbeya, Kigoma na Singida huku mikoa mitano ya mwisho ikiwa ni Tabora,Pwani, Shinyanga, Njombe na Iringa ikishika Mkia.

TRIL.1.29/- ZIMEWEKEZWA NGAZI YA AFYA YA MSINGI– Mhe. Dkt. Dugange
Na OR - TAMISEMI, Dodoma
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Dkt. Festo Dugange, amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali imewekeza Sh.Trilioni 1.29 kwenye ngazi ya afya ya msingi pekee.
Ametoa kauli hiyo jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Nchi-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwenye kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Afya ambayo yamefanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mwaka huu kwa lengo la kutambua mchango wa sekta ya afya, kuimarisha uelewa wa jamii, na kutathmini maendeleo yaliyopatikana, yakiwa na kauli mbiu “Tulipotoka, Tulipo, Tunapoelekea; Tunajenga Taifa Imara na lenye Afya.”
Dkt. Dugange ameeleza kuwa fedha hizo zimetumika kuboresha miundombinu na vifaa tiba katika vituo vya afya, ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mashine za mionzi za kawaida na za kidigitali (Digital X-ray), pamoja na vifaa vya upasuaji vilivyoongezwa katika vituo 21 vya afya nchini.
Vilevile, amesema Serikali imeimarisha mawasiliano na mshikamano kati ya ngazi ya afya ya msingi na rufaa ili kuondoa usumbufu kwa wananchi waliokuwa wakihitaji huduma za kibingwa.
Katika hatua nyingine, Dkt. Dugange ameeleza kuwa katika kipindi hicho hospitali 129 za Halmashauri zimejengwa, pamoja na vituo vya afya 367, majengo ya huduma za dharura 87, ICU 30, mitambo ya hewa tiba (oxygen plant) 21, na nyumba za watumishi 270. Aidha, hospitali kongwe 50 zimekarabatiwa, maboma ya zahanati 980 yamekamilishwa, na magari 560 yamenunuliwa, yakiwemo magari ya wagonjwa 382 na magari ya usimamizi shirikishi 212.
Ameongeza kuwa jitihada hizo zimechangia kupungua kwa vifo vya akinamama wakati wa kujifungua kutoka 556 kwa kila vizazi hai 100,000 miaka mitano iliyopita hadi kufikia 104 mwaka 2024 na kwamba hilo ni zao la uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya ya msingi nchini.

Mchengerwa: Rufiji ina ndoto ya kuwa na majengo ya ghorofa hospitali ya Utete
Na OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema wananchi wa Rufiji wana ndoto ya kuwa na majengo ya ghorofa yatakayoinua viwango vya utoaji huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Utete.
Kauli hiyo ameitoa akiwa katika Hospitali hiyo kabla ya kumkaribisha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa, Ismail Ussi, kuzungumza na wananchi mara baada ya Mwenge wa Uhuru kukagua ukarabati uliofanyika katika hospitali hiyo muhimu kwa wakazi wa Rufiji.
“Kutokana na kasi ya maendeleo inayosukumwa na Mheshimiwa Rais kwa wananchi wa Rufiji, tuna ndoto ya kupata majengo ya ghorofa katika hospitali yetu ya wilaya, na tunayo ardhi ya kutosha kwa ajili ya ujenzi huo,” amesema Mhe. Mchengerwa.
Aidha, amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kutolewa sh. milioni 850 kwa ajili ya kuongeza majengo katika Hospitali hiyo ya Wilaya, hatua itakayoboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na fedha hizo zinatarajiwa kupokelewa ndani ya mwezi huu wa Aprili.
Mhe. Mchengerwa amesisitiza kuwa wananchi wa Rufiji wana matarajio makubwa ya maendeleo, na kwa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, anaamini maendeleo hayo yataendelea kushamiri katika maeneo yote ya wilaya hiyo.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa, Ismail Ussi, amesema kuwa maendeleo yaliyofanywa Rufiji, hususan ukarabati wa Hospitali ya Wilaya Utete, ni kielelezo tosha cha mafanikio ya Mwenge wa Uhuru ambao unahimiza utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.
“Sisi wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa tumeridhishwa na ukarabati na maboresho yaliyofanyika hapa Hospitali ya Wilaya ya Utete, na tunasisitiza huduma ziendelee kutolewa kwa wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa jitihada hizi,” amesema Ussi.

Viongozi wa Mikoa na Wilaya waagizwa kuhamasisha wananchi kushiriki Mbio za Mwenge
Na OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika Mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka 2025, ambazo zinalenga kuchochea utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuleta maendeleo nchini.
Ametoa agizo hilo akiwa katika Shule ya Msingi Ukombozi, Ikwiriri, kabla ya kumkaribisha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa, Ismail Ussi, kuzungumza na wananchi waliokusanyika kushuhudia uraghabishaji wa falsafa ya Mwenge wa Uhuru uliofanywa na wanafunzi wa shule hiyo.
Mhe. Mchengerwa amesisitiza kuwa atahakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu kwenye maeneo yote ambayo Mwenge wa Uhuru utapita kukagua miradi ya maendeleo na kuwaelekeza Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanahamasisha wananchi kwa nguvu zote kushiriki shughuli hizo muhimu.
“Mbio za Mwenge zinahamasisha maendeleo, na ndio maana zinaambatana na uzinduzi wa miradi ya kimkakati ya maendeleo. Ushiriki wa wananchi ni fursa muhimu ya kuwajengea uelewa katika usimamizi na utekelezaji wa miradi hiyo,” amesema Waziri Mchengerwa.
Aidha, Waziri Mchengerwa amemweleza Kiongozi wa Mbio za Mwenge Taifa, kuwa Wilaya ya Rufiji imepiga hatua kubwa katika miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule, barabara, masoko, vituo vya afya na zahanati, miradi ambayo baadhi yake itakaguliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu.
Kwa upande wake, Ismail Ussi amesema kila Mtanzania anapaswa kuienzi falsafa ya Baba wa Taifa, akisisitiza kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendeleza falsafa hiyo kwa kumkabidhi jukumu la kuongoza Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, ambapo miradi ya maendeleo itakaguliwa na kuzinduliwa pale itakapobainika kutekelezwa kwa viwango stahiki.

Serikali yatoa mwezi mmoja kwa wanafunzi wa kidato cha nne 2024 kubadilisha machaguo ya Tahasusi za Kidato cha Tano
Na OR TAMISEMI, Dodoma
SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais-TAMISEMI inatoa fursa ya mwezi mmoja kwa wanafunzi waliohitimu Kidato cha Nne mwaka 2024 kubadili tahasusi au kozi itakayomwandaa kuwa na utaalamu stahiki katika maisha yao ya baadaye.
Utaratibu huo umeanza Machi 31 hadi Aprili 30 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo tarehe 02.04.2025 Jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa alisema hatua hiyo inatoa fursa kwa wanafunzi kubadilisha machaguo ya Tahasusi za Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati na Elimu ya Ufundi kwenye mfumo wa kielektroniki wa uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na Kidato cha Tano na Vyuo.
“Hatua hii ni maandalizi ya awali ya uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga Kidato cha Tano na Vyuo vya Serikali kwa mwaka 2025.”
Serikali imekuwa ikitoa fursa kwa wahitimu wa Kidato cha Nne kufanya mabadiliko ya machaguo ya Tahasusi (combination) na Kozi mbalimbali walizozichagua kupitia Fomu ya Uchaguzi (Selform.).
Fursa hii huwawezesha wanafunzi kurekebisha machaguo yao kulingana na ufaulu waliopata kwenye matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).
Mchengerwa alisema Serikali kupitia Ofisi ya Rais-TAMISEMI imekamilisha utaratibu wa awali wa kuingiza kwenye kanzidata taarifa zilizo kwenye fomu za uchaguzi za wanafunzi kama zilivyojazwa na wanafunzi wakiwa shuleni.
“Baada ya wanafunzi kufanya marekebisho yao, kanzidata hiyo ndiyo itakayotumika kuwachagua na kuwapangia nafasi za Kidato cha Tano na Kozi mbalimbali katika Vyuo vya Kati na vya Elimu ya Ufundi kwa kuzingatia sifa za ufaulu na machaguo yao.”
“Ofisi ya Rais – TAMISEMI inatoa fursa kwa wahitimu wa elimu ya sekondari Kidato cha Nne, mwaka 2024 kubadili machaguo yao ili kutoa nafasi zaidi kwa mwanafunzi kusoma tahasusi au kozi itakayomwandaa kuwa na utaalamu stahiki katika maisha yake ya baadaye.”
Mhe. Mchengerwa alisema hatua hiyo pia itatoa fursa zaidi ya wanafunzi kuongeza machaguo na kufanya machaguo mapya ya Tahasusi na Kozi.
“Napenda kuwasihi wazazi na walezi kushauriana kikamilifu na watoto wao na kupata ushauri wa kitaalamu na kabla ya kufanya machaguo sahihi ya tahasusi na kozi kulingana na ufaulu wao.”
Wanafunzi, wazazi na walezi wanakumbushwa kushauriana kikamilifu ikiwa ni pamoja na kupata ushauri wa kitaalam na kitaaluma kabla ya kufanya mabadiliko ya tahasusi au Kozi.
Mchengerwa amewahimiza wahitimu wote wanahimizwa kufanya marekebisho ya machaguo ya tahasusi na kozi kulingana na ufaulu wao, kwa kuingia kwenye Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi unaopatikana kupitia kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz.
Akielekeza namna ya wahitimu kuingia kwenye mfumo, Mchengerwa alisema mhitimu anapaswa kuandika jina lake la mwisho, mwaka wa kuzaliwa na alama za ufaulu alioupata kwenye somo atakaloulizwa na mfumo au swali lolote atakaloulizwa.
“Ni matumaini yangu kuwa wahitimu wote watatumia kwa ukamilifu fursa waliyopewa ya kubadilisha tahasusi na kozi kulingana na ufaulu waliopata. Pia wataweza kusoma tahasusi au kozi ambazo wamefaulu vizuri ama wana malengo nazo zaidi.”
Mhe. Mchengerwa alisema baada ya kukamilika kwa utaratibu huo na wanafunzi kupangiwa shule na vyuo, hakutakuwa na fursa ya wazazi na wanafunzi kubadili tahasusi na kozi zao.
“Ninawasisitiza wanafunzi, wazazi na walezi kutumia muda huo vyema ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza mara baada ya matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo kutangazwa.”
“Baada ya matokeo ya kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo kutangazwa, Ofisi haitashughulikhuduma ya kubadilisha tahasusi na zoezi hili ni bure.”

Ukaguzi maalum ufanyike shule ya wasichana ya Mkoa wa Morogoro.
Na OR TAMISEMI Pwani
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Mhe. Halima Mdee imeielekeza Ofisi ya mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum katika mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa mkoa wa Morogoro.
Mhe. Mdee ameyasema hayo mara baada ya ziara ya kukagua miradi miwili ambayo
ni ujenzi wa nyumba za Wakuu wa Idara na mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Wasichana ya Mkoa wa Morogoro katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro vijijini.
“wote tumetembelea ujenzi wa shule tumeshuhudia Kazi nyingi sana hazijakamilika Kwa kiwango ambacho fedha zimetolewa, Kamati ya Bunge inafanya kazi na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kama jicho letu uje ufanye ukaguzi Maalum katika mradi huu” amesisitiza.
Amesema hali ya miundombinu iliyojengwa katika mradi huo hauendani na thamani ya fedha ambayo Serikali imekwishatoa katika mradi huo.
Aidha, Kamati imemuelekeza Afisa Masuuli kuwasilisha Kwa Mkaguzi Mkuu wa Serikali Taarifa ya kina inayohusu matumizi ya fedha zote za mradi huo.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Atupele Mwambene amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI imechukua maelekezo yote yaliyotolewa na Kamati hiyo na kwenda kuyasimamia katika utekelezaji.

Mchengerwa: sitaki kusikia changamoto ya dawa hospitali ya utete
Na OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema hataki kusikia tena kuhusu changamoto ya upatikanaji wa dawa katika Hospitali ya Utete na kumtaka Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Hamis Abdallah, kuhakikisha anashughulikia tatizo hilo ili wananchi waendelee kupata huduma bora.
Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji katika Hospitali ya Wilaya ya Rufiji, iliyopo Utete.
"Mganga Mkuu, umepata nafasi ya kuja Rufiji, hivyo unapaswa kushirikiana na wasaidizi wako kutatua changamoto ya kutopatikana kwa dawa katika eneo hili, ambalo mimi ni Waziri wa TAMISEMI," Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Waziri Mchengerwa ameeleza kuwa, Rufiji haijawahi kukutana na changamoto hiyo ya ukosefu wa dawa na kutolea mfano kipindi alichokuwepo Dkt. Makenge, ambaye aliwahi kuwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rufiji.
"Mganga Mkuu, suala hili halifurahishi. Sitaki wananchi walalamike tena kuhusu kukosa dawa. Jipange kuhakikisha kuwa dawa hazipungui, na nitafanya uchunguzi ili kubaini tatizo ni nini, kwani Serikali haina tatizo la fedha za madawa," ameongeza Mhe. Mchengerwa.
Aidha, Mhe. Mchengerwa amewapongeza Waganga Wakuu na watumishi wa kada ya afya kwa juhudi zao katika kupunguza vifo vya mama na mtoto na kudhibiti vitendo vya rushwa, hususan dhidi ya akina mama wanaofuata huduma ya afya ya uzazi katika hospitali na vituo vya afya nchini.
Naye, Mmoja wa wananchi wa Wilaya ya Rufiji, Mwema Said, ametoa shukrani kwa Waziri Mchengerwa kwa kuboresha miundombinu katika Hospitali hiyo ambayo kwasasa wananchi kufurahiya wodi zilizojengwa, vifaa tiba vilivyonunuliwa, pamoja na huduma bora zinazotolewa.

Mchengerwa: Serikali imedhamiria kuboresha maisha ya Walimu nchini
Na OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imejidhatiti katika kuboresha maisha ya walimu nchini, hususan katika maeneo ya maslahi na mazingira ya kazi.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Wilaya ya Rufiji, mara baada ya walimu hao kufanya uchaguzi wa viongozi katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo Ikwiriri.
"Tumedhamiria kuboresha maisha yenu. Binafsi, tangu nikiwa Waziri wa UTUMISHI hadi sasa nikiwa Waziri wa TAMISEMI, nimekuwa mstari wa mbele kupigania madaraja yenu na maslahi ya walimu kwa ujumla," amesisitiza.
Aidha, Waziri Mchengerwa amebainisha kuwa Taifa lina bahati ya kuwa na Rais anayewajali na kuwathamini walimu na kwamba baada ya kupokea ombi la kuwapandisha madaraja walimu, Rais hakusita kulitekeleza, licha ya ukweli kuwa hatua hiyo ilisababisha ongezeko katika bajeti ya mishahara.
Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Walimu Mkoa wa Pwani, Susan Shesha, amemshukuru Waziri Mchengerwa kwa juhudi zake za kupigania maslahi ya walimu tangu akiwa Waziri wa UTUMISHI na kueleza kuwa katika nafasi yake ya sasa kama Waziri wa TAMISEMI, ameendelea kutoa kipaumbele kwa walimu kwa kusimamia miradi ya elimu kwa uadilifu, ili kuhakikisha kuwa inawanufaisha wananchi kwa ujumla.

Laac yaagiza ujenzi wa hospitali ya mji ifakara ukamilike
Na OR-TAMISEMI, Ifakara
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imeielekeza Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara kuhakikisha ujenzi wa hospitali ya mji huo unakamilika kwa wakati ili wananchi wapate huduma bora za afya.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Halima Mdee, ametoa maelekezo hayo baada ya kutembelea na kukagua miradi miwili ya maendeleo ambayo ni ujenzi wa jengo la utawala na ujenzi wa hospitali ya Mji wa Ifakara.
"Afisa Masuuli aondoe dosari zote zilizobainishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili mradi huu ukamilike na kutoa huduma kamili kwa wananchi. Aidha, taarifa ya kila robo mwaka ya maendeleo ya ujenzi huu iwasilishwe kwa CAG kwa ajili ya uhakiki," amesisitiza Mhe. Mdee.
Pia, amemtaka Afisa Masuuli kuhakikisha kuwa zaidi ya Sh. milioni 133, ambazo zilichukuliwa kutoka kwenye fedha zilizotolewa na Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo, zinarudishwa ili kuendeleza mradi huo.
Vilevile, Mhe. Mdee ameelekeza kuwa utekelezaji wa miradi katika halmashauri hiyo uzingatie sheria, kanuni, na miongozo inayotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Atupele Mwambene, amesema kuwa ofisi yake imepokea maelekezo hayo na itahakikisha yanatekelezwa kikamilifu kwa usimamizi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara.

LAAC yataka Utekelezaji wa miradi uzingatie Miongozo na Kanuni
OR-TAMISEMI
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imeielekeza Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kuhakikisha inazingatia miongozo na kanuni katika utekelezaji wa miradi.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Halima Mdee ametoa maelekezo hayo baada ya ukaguzi wa miradi miwili ambayo ni nyumba ya Mkurugenzi wa Halmashauri na kukagua mradi wa wodi tatu (wanaume, wanawake, na watoto) katika hospitali ya Halmashauri.
“Ofisa Masuhuri ahakikishe miradi yote inayotekelezwa inafuata miongozo, sheria, na kanuni zinazotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI,” amesisitiza.
Amesema kamati imeongeza kuwa matumizi sahihi ya miongozo, sheria, na kanuni ni muhimu katika kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia thamani ya fedha na kuepusha matumizi mabaya ya rasilimali.
Naye, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Dkt. Festo Dugange, amesema kuwa ofisi yake imepokea maelekezo hayo na tayari imeanza kuyafanyia kazi kwa utekelezaji.

Wauguzi imarisheni Usimamizi wa utoaji wa huduma bora za afya nchini - Dkt Dugange
Na OR-TAMISEMI, Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Dkt. Festo Dugange amewaelekeza Wauguzi Viongozi wa ngazi zote za afya nchini kuhakikisha wanaimarisha usimamizi wa utoaji wa huduma bora ili wananchi wote wapate huduma bora na kwa usawa
Dkt. Dugange ameyasema hayo leo Machi 27, 2025 wakati akifungua mkutano Mkuu wa Mwaka wa wauguzi viongozi uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa PSSSF Jijini Dodoma wenye kauli mbiu ya inayosema HUDUMA BORA WAJIBU WANGU.
Amefafanua kuwa Serikali ya Awamu ya sita imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya hivyo bila ya kuwepo kwa huduma nzuri na bora kutoka kwa watoa huduma za afya, na hasa Wauguzi, uwekezaji huu hautakua na manufaa.
“Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya afya ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya afya, ununuzi wa vifaa na vifaa tiba, uboreshaji wa mazingira ya kazi, hivyo mapaswa kuwasimamia waliopo chini yenu ili wafanye kazi kwa weledi na uadilifu,” Dkt. Dungange amesisitiza.
Dkt. Dugange amewataka wauguzi wote nchini kuhakikisha wanafanyakazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu, Miongozo na Miiko ya taaluma ili kuepuka malalamiko yasiyokuwa ya lazima katika eneo la utoaji wa huduma za afya msingi nchini.
“Tunatambua kuwa wauguzi wanafanya kazi nzuri sana japo kuna baadhi yenu wachache wanaharibu sifa nzuri ya wauguzi kwa kufanya makosa mbalimbali yanayoweza kuepukwa hivyo msisite kuchukua hatua za kisheria na kinidhamu dhidi ya wote watakaobainika kwenda kinyume, kukiuka maadili ya kitaaluma na kufanya ubadhirifu wa mali za umma, amesisitiza Dkt.Dugange
Aidha, amewataka wauguzi hao kujiendeleza ili kupata wauguzi wenye ujuzi na maarifa zaidi ikiwa ni pamoja na Wauguzi Bingwa watakaosaidia kuimarisha upatikaji wa huduma za kibingwa katika hospitali zetu nchini.

Mchengerwa: daraja la muhoro ni mkombozi kwa wananchi rufiji
Na OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema ujenzi wa Daraja la Muhoro utaleta ukombozi kwa wananchi wa Kata ya Muhoro, ambao kwa muda mrefu wamekumbwa na changamoto za usafiri na hata kupoteza maisha wanapovuka Mto Rufiji.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo, Mhe. Mchengerwa amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha mradi huo wa kisasa wenye thamani ya zaidi ya Sh.Bilioni 17.
“Nimeridhishwa na kasi ya ujenzi, lakini nataka mkandarasi aongeze juhudi ili daraja likamilike ifikapo Julai 2025,” amesisitiza Waziri Mchengerwa.
Kwa mujibu wa Meneja wa Wakala qa Barabara Mijini na Vijijiji (TARURA) Mkoa wa Pwani, Mhandisi Leopold Runji, ujenzi umefikia asilimia 40, tayari nguzo nne kati ya sita zimekamilika na lina urefu wa mita tisa, hivyo litasaidia kuzuia mafuriko.
Nao, Wakazi wa Muhoro, Pili Lwambo na Mikidadi Omary, wameeleza furaha yao, wakisema daraja hilo litaepusha vifo vinavyosababishwa na mamba, kusaidia kina mama kujifungua hospitalini, na kurahisisha usafiri wa watoto kwenda shule.

Mchengerwa atoa miezi miwili barabara za TARURA Ikwiriri zikamilike
Na OR-TAMISEMI, Pwani
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amemtaka Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Pwani, Mhandisi Leopold Runji, kuhakikisha wakandarasi wanakamilisha ujenzi wa barabara za lami Ikwiriri ndani ya miezi miwili ili wananchi wanufaike na maboresho ya miundombinu hiyo yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita.
Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hizo wilayani Rufiji.
"Natoa miezi miwili tu, barabara ziwe zimekamilika ifikapo Mei 30, 2025, ikiwa ni pamoja na mitaro na taa za barabarani. Hakutakuwa na nyongeza ya muda," amesisitiza Waziri Mchengerwa.
Ameagiza Meneja wa TARURA kuwasimamia wakandarasi wafanye kazi usiku na mchana, akibainisha kuwa barabara hizo zilipaswa kukamilika Desemba 2024 na iwapo hazitakamilika kwa muda uliopangwa, atamuwajibisha meneja huyo.
Nao, Baadhi ya wananchi, akiwamo Dereva wa bodaboda Ramadhan Mwipi na Mama Lishe Mariam Hamza, wamemshukuru Waziri Mchengerwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha barabara hiyo, wakieleza kuwa imeleta ahueni kubwa kwa usafiri na biashara zao.

LAAC yataka hatua dhidi ya watumishi wazembe Mbeya zichukuliwe
Na OR-TAMISEMI, Mbeya
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Halima Mdee, imeielekeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaokwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Maelekezo hayo yametolewa katika kikao cha majumuisho baada ya ziara ya siku tatu ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa mkoani humo.
"Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ichukue hatua za kinidhamu kwa watumishi wote watakaobainika kukwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo," amesisitiza
Aidha, Kamati imeitaka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa miradi yote ya maendeleo, ikiwemo kubaini changamoto zinapojitokeza mapema ili kuepusha athari katika utekelezaji wake.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Atupele Mwambene, amesema kuwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI imechukua maelekezo hayo na itayafanyia kazi kwa kuhakikisha utekelezaji wake unafuatiliwa ipasavyo.
Kamati hiyo imetembelea na kukagua miradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, na Halmashauri ya Wilaya ya Mbalizi, mkoani Mbeya.

“Marufuku malori kupita barabara za Mwendokasi” Mhe. Mchengerwa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Machi 21, 2025 amekemea uharibifu wa barabara unaofanywa na Magari Makubwa (Malori) kupita Mwendokasi huku akizitaka Halmashauri na Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kufikiri namna bora ya kumaliza foleni ndani ya Dar es Salaam.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya Utiaji Saini wa Zabuni 9 zilizobeba thamani ya Shilingi Bilioni 221.8 zinazojumuisha Barabara zenye urefu wa Kilomita 84.4 zinazotarajiwa kwenda kuboreshwa katika Halmashauri za Dar es Salaam chini ya Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP TWO).
Akizungumza wakati wa Hotuba yake Mhe. Mchengerwa amesema Mhe. Rais hatamani kuona foleni, Halmashauri kaeni fikirini namna ya kumaliza foleni ndani ya Jiji hili, mmetoa Kibali Magari kupita Mwendokasi afadhali kwa Magari madogo lakini sasa yanapita mpaka malori, barabara zimeanza kuharibika. Malori kuanzia sasa nisisikie yamekatisha ndani ya barabara za Mwendokasi.
Lakini pia tutakwenda kufanya mapitio hii asilimia ya makusanyo ya mapato ya ndani inayopaswa kwenda kwenye barabara isiwe 10% ili muifanye TARURA iwe na uwezo wa kufanya kazi masaa 24 kusimamia ujenzi wa barabara katika maeneo yetu.
Nendeni mkafungue barabara ambazo watu wanapaswa kupita kumaliza foleni, TARURA mkoa nendeni mkafikiri nini kifanyike ili mtengeneze barabara za kimkakati zinazoweza kupunguza foleni".
Mhe. Mchengerwa ameshuhudia Utiaji Saini wa Mikataba ya Ujenzi wa Barabara kupitia DMDP zenye urefu wa Km. 84.4.

Mhe. Mchengerwa Utiaji saini wa Mikataba ya ujenzi wa barabara km. 84 za Dar es salaam
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Machi 21, 2025 ameshuhudia Utiaji Saini wa Zabuni 9 zilizobeba thamani ya Shilingi Bilioni 221.8 zinazojumuisha Barabara zenye urefu wa Kilomita 84.4 zinazotarajiwa kujengwa katika Halmashauri za Dar es Salaam chini ya Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II).
Miongoni mwa zabuni Hizo, Zabuni 2 zenye Jumla ya thamani ya Sh.Bil 47.1 ni kwa ajili ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ambapo Bilioni 25.9 zitakwenda kutengeneza Barabara za Masuliza, Kilimahewa na Tuangoma zenye jumla ya kilomita 10.21 huku Bilioni 21.1 zikielekezwa kwa ajili ya Barabara za Konisaga 1, Konisaga 3, Kurasini, Taningira uhasibu, Kizota, Lushoto, Pendamoyo, Mandera, Mkumba Miburani, Kipati pamoja na Vivuko 6 vya Mdeda, Mpeta, Baajun, Msalaka Mashine ya maji, Shehe muckhi, na Azimio Msalaka.
Akizungumza katika Hafla hiyo Mhe. Mchengerwa amesema Matarajio ya Rais wetu ni kulifanya Jiji la Dsm kuwa Miongoni mwa Majiji ya Kisasa, Jiji shindani (Metropolitan city) na fedha hizi ni za Watanzania, Wakandarasi wanapokabidhiwa Mikataba hii waende kuitendea haki, na Wakandarasi walioshindwa kutimiza Makubaliano naelekeza kutengua Mikataba, taratibu zote zifuatwe bila kuingiza hasara Serikali maana yake ni lazima walipe fedha zote walizopewa na Serikali. Taratibu hizi zianze na ntaanza kuzifatilia kwa katibu mkuu"
"Na Kampuni hizi tulizozipa Kazi leo hii kusaini Mikataba wasipotekeleza makubaliano na kushindwa kutekeleza kwa muda tuliokubaliana taratibu za kuvunja Mkataba zifuatwe na wawe blacklisted wasiruhusiwe kupata Mkataba wowote ndani ya Nchi hii. Kwenye Mikataba hii tuliyosaini leo hatutakuwa na nyongeza hata siku moja". Alisema Mhe. Mchengerwa.
Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Mradi (Millenium Tower) na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali.

Mhe. Mdee: Wajibu wenu ni kuhudumia wananchi kwa ufasaha
Na OR-TAMISEMI, Mbeya
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mhe. Halima Mdee, amewataka Watumishi wa Umma na Viongozi kutekeleza wajibu wao kwa ufasaha ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mhe. Mdee akizungumza katika ziara ya Kamati hiyo kukagua miradi mbalimbali ya afya na elimu inayotekelezwa Halmashauri ya Kyela, mkoani Mbeya, amesema "Kila mmoja atekeleze wajibu wake kwa wakati na kwa ufasaha, viongozi hawatakuwa na haja ya kuja kukagua."
Ameeleza kuwa kutokana na ukubwa wa nchi, haiwezekani kwa kiongozi mmoja kutembelea kila mahali kutoa huduma, hivyo majukumu hayo yamekabidhiwa kwa Watumishi wa Umma ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki.
Aidha, amewataka Watumishi wa Umma kutekeleza maelekezo yanayotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge na kuhakikisha wanazitatua dosari zinazobainishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa kutoa taarifa sahihi.
Naye, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Dkt. Festo Dugange, amesema Ofisi yake imechukua maelekezo yote yaliyotolewa na Kamati na itayasimamia kikamilifu katika utekelezaji wake.
Pia, Mhe. Dkt. Dugange amewataka Watumishi wa Umma kuhakikisha fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo zinatumika ipasavyo ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na kuzingatia thamani ya fedha.

Mchengerwa: bil.82.84/- zimekopeshwa kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu
Na OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema katika mwaka wa fedha 2024/25, serikali imetoa mikopo yenye thamani ya Sh. bilioni 82.84 kwa vikundi 8,275 vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu kupitia mpango wa asilimia 10 ya mapato ya halmashauri.
Waziri Mchengerwa ameeleza hayo wakati akiwasilisha mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2025/26 katika vikao vya kamati za kudumu za Bunge linaloendelea jijini Dodoma.
Ameeleza kuwa kati ya fedha hizo Sh. Bilioni 40.71 zimetolewa kwa vikundi 4,557 vya wanawake, Sh.Bilioni 36.64 kwa vikundi 2,827 vya vijana na Sh.Bilioni 5.48 kwa vikundi 891 vya watu wenye ulemavu.
Waziri Mchengerwa amefafanua kuwa
Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeandaa mwongozo wa ukomo wa mkopo ambao utawezesha halmashauri kusimamia utoaji wa mikopo yenye tija kwa jamii na kulingana na mwongozo huo kiwango cha juu cha mkopo kwa kikundi ni sh. milioni 150 na kiwango cha chini cha mkopo ni sh.500,000.
Aidha, Waziri Mchengerwa amebainisha kuwa hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya kwenye vituo vya kutolea huduma imeimarika ambapo upatikanaji wa dawa umeongezeka kutoka asilimia 63.00 mwaka 2023/24 hadi asilimia 79.30 Januari 2025, ikiwa ni ongezeko la asilimia 16.30.

Kamati ya Bunge yaitaka TAMISEMI kumchunguza Mkandarasi wa mradi wa TACTIC Kahama
Na OR-TAMISEMI, Shinyanga
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI imeielekeza Ofisi ya Rais - TAMISEMI kupitia upya mkataba wa mkandarasi wa kigeni, Sichuan Road and Bridge Group Corporation, na kuchukua hatua za haraka kutokana na kushindwa kutekeleza kwa wakati mradi wa TACTIC awamu ya kwanza katika Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Justin Nyamoga, ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kukagua utekelezaji wa mradi huo wa ujenzi wa barabara za katikati ya mji na mifereji ya maji ya mvua wenye thamani ya sh. bilioni 20.864.
Kwa mujibu wa mkataba, mradi huu ulianza kutekelezwa Novemba 20, 2023, na ulipaswa kukamilika Februari 19, 2025. Hata hivyo, hadi sasa utekelezaji wake uko katika asilimia 48%, hali iliyosababisha kuongezewa muda wa ziada wa miezi mitatu hadi Mei 19, 2025.
Mhe. Nyamoga amesema "Kamati haitatoa maelekezo nini kifanyike, lakini ninyi nendeni mkasome mkataba wake, kaangalieni changamoto anazozisababisha, ikiwemo kuwafilisi Watanzania ambao yeye amechukua vitu kwao na hajawalipa."
Naye, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema serikali itasubiri kwa miezi mitatu kuona kama mkandarasi huyo atakamilisha kazi na iwapo atashindwa, serikali itavunja mkataba na mkandarasi huyo hatakuwa na sifa ya kupata kazi nchini.
Kwa upande wake, Mhandisi Rogatus Mativila, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, amesema moja ya changamoto zinazokwamisha miradi mingi ni kuhamisha pesa za miradi kwenda kwenye shughuli nyingine baada ya kuzipokea.
Mradi huu wa Kupendezesha Miji (TACTIC) unatekelezwa katika Halmashauri 45 nchini, ikiwemo Kahama, ambapo awamu ya kwanza inahusisha, Ujenzi wa barabara za katikati ya mji – Kilomita 12.03, Barabara za eneo la viwanda Zongomela – Kilomita 3.06, Ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua – Chelsea – Lyazungu na Shunu Magobeko (Kilomita 4.9)

Mchengerwa amtaka Mkandarasi wa daraja la Mbambe kuongeza kasi ya ujenzi
Na. OR-TAMISEMI, Rufiji Pwani
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amemtaka mkandarasi wa Kampuni ya Nyanza Road Works kuongeza kasi ya ujenzi wa Daraja la Mbambe lenye urefu wa mita 81 ili likamilike kwa wakati na kuondoa adha inayowakabili wananchi wa Wilaya ya Rufiji.
Mhe. Mchengerwa akitoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kijiji cha Mbambe ya kufuatilia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, amesema; "Mkandarasi ongeza kasi ya ujenzi wa daraja hili kwani asilimia 22 iliyofikiwa bado ni ndogo sana. Kwa mwendo huu, mvua zikiongezeka zitaleta changamoto itakayokwamisha ujenzi."
Aidha, amewataka wananchi wa Kijiji cha Mbambe kushirikiana na uongozi wa wilaya kwa kutoa taarifa pale wanapoona hali ya kusuasua katika ujenzi wa daraja hilo na kuwahakikishia kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari ametoa fedha kwa ajili ya fidia kwa wote waliopitiwa na mradi huo, ambao unahusisha pia ujenzi wa barabara za maingilio zenye urefu wa kilomita 3.
"Mkuu wa Wilaya, naelekeza Meneja wa TANROADS wa mkoa kuhakikisha kuanzia wiki ijayo fidia inalipwa kwa wale wote waliokwishahakikiwa madai yao. Rais Samia ameshatoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya fidia," ameagiza Mhe. Mchengerwa.
Hata hivyo, Waziri Mchengerwa amewataka wananchi wa Mbambe na Rufiji kwa ujumla kupuuza taarifa potofu kwamba mradi wa daraja hilo umesimama, akisisitiza kuwa ujenzi unaendelea.
Awali, Msimamizi wa Mradi kutoka Kampuni ya Nyanza Road Works, Mhandisi Emmanurel Owoya, amesema kuwa ujenzi huo umefikia asilimia 22, ambapo tayari nguzo za msingi 64 kati ya 107 zimejengwa na Sh.Bilioni 24.16 zitatumika kukamilisha ujenzi wa Daraja la Mbambe, likijumuisha barabara za maingilio za kilomita 3 kwa pande zote mbili za daraja.

LAAC yaielekeza iringa kukamilisha ujenzi wa uzio wa madarasa ya Awali
Na OR-TAMISEMI, Iringa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imeielekeza Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mjini kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa uzio katika madarasa ya awali ya Shule ya Msingi Uyole.
Maelekezo hayo yametolewa katika kikao cha majumuisho baada ya Kamati hiyo kufanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo na Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye Mbunge wa Kilindi, Mhe. Omary Kigua kwa niaba ya Mwenyekiti wa LAAC, Halima Mdee.
Amesema “Afisa Masuhuri hakikisha uzio katika madarasa ya awali uwe umejengwa kabla ya kukamilika kwa mwaka wa fedha 2025/26, na taarifa ya ujenzi huo iwasilishwe kwa CAG kwa ajili ya mapitio.”
Pia, Amesema Kamati imeelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa ujenzi wa jengo la kufulia katika Kituo cha Afya Itamba unakamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu wa fedha.
Naye, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Dkt. Festo Dugange, amesema kuwa serikali kupitia TAMISEMI itafanyia kazi mapungufu yote yaliyoainishwa na Kamati ili kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa viwango vinavyokubalika kwa manufaa ya wananchi.
Miradi iliyokaguliwa na kamati hiyo ni pamoja na Ujenzi wa machinjio ya kisasa Ngelewala, Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Mkondo Mmoja Uyole na Ujenzi wa Kituo cha Afya Itamba ambapo kamati imesisitiza ikamilike kwa wakati ili kuboresha huduma kwa wananchi wa Iringa.

LAAC yataka dosari zilizobainishwa na CAG Halmashauri ya Wilaya Kilolo zitatuliwe
Na OR-TAMISEMI, Kilolo
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imeielekeza Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kuhakikisha inaziondoa dosari zote zilizobainishwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ujenzi wa Shule ya Wasichana ya Lugalo, mkoani Iringa.
Maelekezo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa kamati, Halima Mdee baada ya kamati kutembelea na kukagua ujenzi wa shule hiyo.
"Dosari zote zilizobainishwa na CAG katika utekelezaji wa mradi huu zinaondolewa na kuhakikisha miundombinu muhimu inakamilika," amesema Mhe. Mdee.
Kamati pia imeelekeza Afisa Masuuli wa Halmashauri kuandaa taarifa yenye maelezo ya kina na mchanganuo wa matumizi ya fedha zote za mradi huo na kuiwasilisha kwa CAG kwa ajili ya uhakiki.
Aidha, kamati imeitaka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kufanya tathmini ya kina na kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo, huku ikichukua hatua za haraka iwapo kutabainika ukiukwaji wa sheria na taratibu.

Serikali kujenga na kukarabati shule ya msingi Kakoyoyo
Na OR-TAMISEMI, Geita
Serikali imeahidi kuanza ukarabati na ujenzi wa majengo ya Shule ya Msingi Kakoyoyo, ambayo ilifungwa baada ya baadhi ya majengo yake kutitia, kupata nyufa, na kuanguka kufuatia mvua kubwa zilizonyesha mapema 2024 katika Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita.
Shule hiyo, iliyojengwa kwa nguvu za wananchi mwaka 1999, ilihudumia wanafunzi 934 ambao kwa sasa wamelazimika kusoma katika Shule ya Msingi Igwamanoni kwa kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 13.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba, ametembelea shule hiyo na kuthibitisha kuwa serikali itaanza ukarabati mara baada ya tathmini ya wataalamu kukamilika.
“Tumeona uhitaji mkubwa wa kurejesha shule hii, na kupitia mapato ya ndani, serikali kuu, pamoja na wadau wa maendeleo, tutahakikisha ukarabati unafanyika ili wanafunzi waendelee kusoma katika mazingira bora,” amesema.
Naye, Diwani wa Kata ya Bulega, Mhe. Erick Kagoma, ameipongeza serikali kwa hatua hiyo, akieleza kuwa kurejeshwa kwa shule hiyo kutapunguza adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu.
Ziara hiyo imefanyika kufuatia ombi la Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko, ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, ili kuwapa wananchi taarifa kuhusu hatua za serikali katika kuboresha shule hiyo.

Kamati ya Bunge yaelekeza ujenzi wa shule mpya za Muleba zikamilike ifikapo Aprili, 2025
Na OR-TAMISEMI
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI imeuagiza uongozi wa Wilaya ya Muleba, Mkoa wa Kagera, kuhakikisha ujenzi wa Shule ya Sekondari Biija na Shule ya Sekondari ya Amali (Ufundi) Mubunda unakamilika ifikapo Aprili 2025 ili wanafunzi waanze masomo.
Miradi hiyo inafadhiliwa na Serikali kwa asilimia 100 kupitia mradi wa SEQUIP, ambapo kila shule imepokea Sh.Milioni 584.2 na ujenzi wake unafanyika kwa njia ya 'Force Account'.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Justin Nyamoga, akizungumza katika ziara ya kamati ya kukagua ujenzi huo, amesema Shule ya Biija imejengwa ili kupunguza umbali wa wanafunzi wanaosafiri kutoka maeneo ya mbali na kuagiza pindi ujenzi utakapokamilika, walimu waletwe haraka na wanafunzi waanze masomo bila kuchelewa.
Pia, amesisitiza kuwa wanafunzi wanaotembea mwendo mrefu wahamishiwe katika shule hiyo ili kurahisisha upatikanaji wa elimu.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amehimiza viongozi wa Halmashauri kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na miundombinu ya shule inatunzwa ili iweze kuwanufaisha vizazi vingi na kwamba ucheleweshaji wa miradi haukubaliki.
Aidha, Mhe. Katimba amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kuimarisha matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa manunuzi ya umma (NEST) ili kuepusha ucheleweshaji wa miradi.

Mchengerwa atoa maelekezo nane mahsusi kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa maelekezo mahsusi nane kwa viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwamo kufanya tathmini ya kina na kuchukua hatua za haraka kwa watumishi wanaoshiriki kuhujumu mfumo wa mapato kwenye maeneo yao.
Akifunga Machi 12, 2025 Mkutano Mkuu wa 39 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri Mchengerwa, Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. DFesto Dugange, amewataka wafanye tathmini hiyo ili kuhakikisha hakuna upotevu au uvujaji wa mapato mikononi mwa watumishi.
Aidha, ameelekeza kupatiwa taarifa ya namna kila Halmashauri zilivyokusanya katika vyanzo kodi ya majengo, ushuru wa mabango na kodi ya Ardhi ili ili kupima ufanisi.
Pia, ameagiza Halmashauri zisimamie kikamilifu utoaji wa huduma bora za afya ili kuondoa malalamiko ya wananchi kwa serikali na ziweke mikakati madhubuti ya kudhibiti upotevu wa fedha za uchangiaji wa huduma za afya.
Kuhusu elimu, ameelekeza wahakikishe wanasimamia uandikishaji wa madarasa ya awali, darasa la kwanza na makundi mengine kutokana na hali kutoridhisha kwa baadhi ya mikoa sambamba na kuthibiti mdondoko wa wanafunzi.
Mhe. Waziri Pia ameelekeza Halmashauri zinazotekeleza miradi ya TACTIC ambayo Wakurugenzi wamesaini mikataba, hakikisheni wanasimamia utekelezaji kwa viwango, ukubwa wa kazi, muda unaotakiwa na fedha itumike kama ilivyokusudiwa.
Pamoja na hayo, ameagiza Wakurugenzi kusimamia mikopo ya asilimia 10 na kuondoa changamoto zinazolalamikiwa kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyoandaliwa kusimamia mikopo hiyo.

Kamati ya Bunge yahimiza maslahi ya watumishi wapya yazingatiwe
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI imeiomba serikali kuendelea kuboresha maslahi ya watumishi na kuwalipa stahiki zao, hususan kwa watumishi wapya, ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Justin Lazaro Nyamoga ametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya kukagua mradi wa Hospitali Mpya ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza ambayo ni miongoni mwa hospitali mpya 129 zilizojengwa na serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
"Suala la watumishi katika baadhi ya mikoa, ikiwemo Kigoma, ni changamoto. Kamati inasisitiza mambo mawili: kuongeza watumishi hasa pale fursa zinapojitokeza, na kuhakikisha malipo stahiki yanatolewa kwa watumishi wapya na wanaohama ili kuwapa moyo wa kufanya kazi kwa bidii," amesema Mhe. Nyamoga.
Aidha,Kamati hiyo imetoa maelekezo kwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuhakikisha jenereta kubwa linapelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Uvinza, kwani lililopo sasa halina uwezo wa kusambaza umeme kwa hospitali nzima.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Mhe. Mohamed Mchengerwa, ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo ya kamati huku akiwataka watumishi wa umma kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Mchengerwa: Rais Samia ametoa kipaumbele kwa Serikali za Mitaa kuchochea maendeleo
Na OR-TAMISEMI, Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuweka mkazo katika kuimarisha serikali za mitaa kama chachu ya maendeleo ya wananchi kwa kuongeza rasilimali, kuboresha mifumo ya utendaji, na kuimarisha uwajibikaji wa viongozi wa halmashauri.
Waziri Mchengerwa amesema hayo Machi 11, 2025 kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 39 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika jijini Dodoma.
“Maendeleo siyo ahadi, bali ni hatua zinazochukuliwa kila siku kwa vitendo. Tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha serikali za mitaa zinakuwa msingi wa maendeleo ya wananchi. Serikali yake imeonesha kuwa maendeleo yanaanzia chini kwenda juu, na kwa kuimarisha serikali za mitaa, tumewawezesha wananchi kushiriki moja kwa moja katika mchakato wa maendeleo,” amesema Mhe. Mchengerwa.
Ameeleza kuwa uwekezaji mkubwa umefanyika katika sekta ya elimu, afya, na miundombinu, hatua inayowezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi.
Aidha, Waziri Mchengerwa amewahimiza viongozi wa serikali za mitaa kuwa wabunifu, kuzingatia uadilifu katika utendaji wao, na kushirikiana na serikali kuu ili kuhakikisha maendeleo ya taifa yanapiga hatua kwa kasi zaid

Kamati ya Bunge yavutiwa na ubunifu wa TARURA ujenzi wa daraja la kamba za chuma Mbulu
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI imepongeza ubunifu wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) katika ujenzi wa daraja la kamba za chuma kwenye barabara ya Tipri, Halmashauri ya Mji wa Mbulu, Mkoa wa Manyara ambalo limeondoa kikwazo kikubwa cha shughuli za kiuchumi na kijamii wakati wa msimu wa mvua.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Justin Nyamoga, ametoa pongezi hizo katika ziara ya kukagua mradi huo katika mto Mtunguli ambao umegharimu Sh. milioni 158.9 kutoka kwenye tozo ya mafuta.
Mhe. Nyamoga ameshauri TARURA kujenga kingo za daraja hilo ili kuimarisha usalama wa watembea kwa miguu na waendesha pikipiki wanaoweza kuteleza na kuanguka mtoni.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema daraja hilo la watembea kwa miguu lina uwezo wa kubeba tani 1.5 na litadumu kwa zaidi ya miaka 70 na kutoa wito kwa wananchi kulinda miundombinu hiyo muhimu.
Daraja la Tipri, lililojengwa kwenye bonde la mto Mtunguli, litasaidia zaidi ya wananchi 3,900 waliokuwa wakikwama na kupoteza mawasiliano wakati wa mvua

Maafisa Elimu wahimizwa kuimarisha usimamizi wa elimu nchini
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Elimu, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Emmanuel Shindika, amewataka Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri kuhakikisha wanaimarisha ufuatiliaji na usimamizi wa elimu katika maeneo yao ili kuleta mabadiliko chanya kwenye Sekta ya Elimu nchini.
Dkt. Shindika ametoa wito huo leo Machi 7, 2025 alipokuwa akifunga Mkutano Mkuu wa Umoja wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri (REDEOA), uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambao unatathmini utekelezaji wa shughuli za elimu kwa kipindo cha kuanzia mwezi Julai hadi Desemba, 2024.
Amesema ni muhimu kuimarisha usimamizi wa elimu kwa kuhakikisha uandikishaji wa wanafunzi wa shule za awali na msingi unasimamiwa kwa ukaribu ili kufanikisha malengo ya serikali katika Sekta ya Elimu.
"Uandikishaji wa wanafunzi wa awali na msingi bado ni changamoto katika maeneo yenu. Hakikisheni mnasimamia kwa karibu suala hili ili kutimiza malengo yaliyowekwa na Serikali," amesisitiza.
Pia amewataka Maafisa Elimu kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili walimu ili kuongeza tija na ufanisi katika ufundishaji na kuimarisha mahusiano mazuri kazini, kuwalipa walimu stahiki zao kwa wakati, na kuhakikisha malipo ya likizo hayacheleweshwi.
Aidha, amewaelekeza Viongozi hao kusimamia kwa weledi utekelezaji wa miradi ya elimu katika maeneo yao, ili ikamilike kwa wakati na kuendana na thamani ya fedha iliyotengwa huku akisisitiza ushirikiano wa karibu kati ya Maafisa Elimu na Wadau mbalimbali wa elimu ili kuimarisha ubora wa elimu nchini.

Kamati ya Bunge ya TAMISEMI yataka ulinzi wa daraja la mawe Garkawe
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, imewataka wananchi kuacha shughuli za kilimo kando ya mto ulipojengwa Daraja la Mawe la Garkawe katika barabara ya Maretadu - Garkawe, Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara ili kulinda miundombinu ya daraja hilo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Justin Nyamoga ametoa wito huo katika ziara ya kukagua mradi wa daraja hilo, ambalo limejengwa kwa fedha za tozo ya Mafuta kiasi cha Sh.Milioni 470.95.
Aliutaka uongozi wa Wilaya ya Mbulu kufuatilia na kuzungumza na wananchi ili kuhakikisha shughuli za kilimo haziendelei karibu na daraja hilo.
"Madaraja haya yanajengwa kwa gharama kubwa, na tunatambua kuwa wananchi wanahitaji kulima. Hata hivyo, ni muhimu kuacha nafasi ili mto huu usiendelee kupanuka, kwani inaweza kusababisha madhara kwenye daraja," amesema Mhe. Nyamoga.
Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema kuwa ujenzi wa madaraja ya mawe, ikiwamo la Garkawe, umesaidia kupunguza gharama za ujenzi kutokana na wepesi wa upatikanaji wa malighafi.
"Madaraja haya yaliyotumia teknolojia ya mawe yamejengwa 238 kwa gharama ya jumla ya Sh.Bilioni 12.52 nchini kote. Ni hatua kubwa katika kupunguza gharama za ujenzi na kuongeza ufanisi," amesema Mhe. Katimba.

Ubora wa miundombinu uendane na ubora wa huduma – Dkt. Mfaume
Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume, amewataka watumishi wa sekta ya afya kutoa huduma bora zinazoendana na ubora wa miundombinu ambayo serikali imewekeza katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Dkt. Mfaume ametoa maelekezo hayo alipofanya ziara katika Hospitali ya Wilaya ya Bahi, ikiwa ni sehemu ya ziara shirikishi ya usimamizi wa upatikanaji wa huduma mbalimbali za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii katika Mkoa wa Dodoma.
"Tuna majengo mazuri na vifaa vyote vya msingi ambavyo vimetolewa na serikali. Hivyo, ubora wa majengo uendane na huduma zinazotolewa kwa kuzingatia miongozo ya afya," amesema Dkt. Mfaume.
Aidha, amesisitiza kuwa kuna miongozo mbalimbali kutoka Wizara ya Afya na Shirika la Afya Duniani (WHO) inayopaswa kuzingatiwa katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa.
Vilevile, amewakumbusha wasimamizi wa miradi ya afya inayoendelea kutekelezwa nchini kuhakikisha kuwa miradi hiyo inazingatia thamani ya fedha ili ikidhi malengo ya serikali ya kuboresha huduma kwa wananchi.

Prof.Mkenda asisitiza umuhimu wa Elimu ya Amali kukuza ujuzi
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, amesisitiza umuhimu wa elimu ya amali kama njia ya kukuza ujuzi wa kiutendaji katika sekta mbalimbali kama vile ufundi, kilimo, uvuvi, muziki na michezo.
Aidha, ametoa wito kwa wazazi na wawekezaji kuunga mkono elimu hiyo kwa kuwa ni suluhisho muhimu kwa changamoto ya ukosefu wa ajira na inahitajika kwa ufanisi wa sekta ya uwekezaji.
Prof. Mkenda ameyasema hayo , katika Mkutano wa Umoja wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Ameeleza kuwa shule za amali zitakazokuwa na rasilimali na vitendea kazi vya kutosha zitapata kibali cha kufundisha na kutoa mafunzo ya vitendo.
Pia, amesisitiza kuwa elimu ya amali inapaswa kuimarishwa ili kukabiliana na upungufu wa wafanyakazi wenye ujuzi katika sekta mbalimbali za uchumi.
"Wazazi kumsihofie kupeleka watoto wenu katika shule za amali, elimu hii ni fursa muhimu ya kuwajengea watoto maisha bora na mustakabali mzuri wa ajira,"amesema.

Halmashauri zatakiwa kupima maeneo ya huduma za afya na kupata hati miliki
Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume, amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha zinapima ardhi za Zahanati, Vituo vya Afya, na Hospitali zote nchini ili kupata hati miliki za maeneo hayo.
Dkt. Mfaume ametoa ushauri huo alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa huduma za afya, lishe, na ustawi wa jamii katika Mkoa wa Dodoma, ambapo alitembelea Kituo cha Afya Kibakwe kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
“Ni lazima tupime maeneo yetu, tuweke mipaka rasmi na kuhakikisha yanakuwa na hati miliki ili kuzuia uvamizi na kuimarisha utoaji wa huduma za afya,” amesema Dkt. Mfaume.
Ameongeza kuwa kasi ya ukuaji wa miji inasababisha watu kuhamia karibu na vituo vya huduma, hivyo upimaji wa maeneo hayo utasaidia kulinda miundombinu ya afya dhidi ya uingiliaji usio rasmi.

Dkt. Mfaume: TAMISEMI tumejipanga vyema utekelezaji wa sheria ya Bima ya Afya kwa Wote
Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume, amesema kuwa katika kuelekea utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote, TAMISEMI imejipanga vyema kuhakikisha kunakuwa na usimamizi bora huduma za afya katika ngazi ya msingi.
Dkt. Mfaume ametoa kauli hiyo alipokuwa katika ziara yake ya kukagua utoaji wa huduma za afya, lishe, na ustawi wa jamii mkoani Dodoma, ambapo alitembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
Amesema TAMISEMI itahakikisha katika ngazi ya afya ya msingi bidhaa zote muhimu za afya zinapatikana.
"Tunawahakikishia Watanzania kuwa katika ngazi ya huduma za afya ya msingi, Ofisi ya Rais TAMISEMI imejipanga kuhakikisha wananchi wote wanaojiunga na Bima ya Afya kwa Wote wanapata huduma zote stahiki kama inavyotakiwa," amesema Dkt. Mfaume.
Aidha, amebainisha kuwa hapo awali kulikuwapo na changamoto ya baadhi ya wanachama wa bima ya afya kukosa dawa katika vituo vya kutolea huduma na kulazimika kununua dawa hizo wenyewe.
Hata hivyo, kwa sasa TAMISEMI imechukua hatua kuhakikisha vituo vya afya vinakuwa na akiba ya kutosha ya dawa na vifaa tiba ili kuboresha huduma kwa wananchi

Wagonjwa 6,847 watibiwa hospitali ya wilaya Handeni
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema wagonjwa wapatao 6,846 wamepata huduma za Afya Katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni tangu ilipokamilika na kuanza kutoa huduma.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Hospitali hiyo iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Tanga.
Amesema ujenzi wa hospitali hiyo umegharimu jumla ya shilingi Bilioni 7.3 ambapo Serikali imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 4.3 na wadau wa Islamic Help wametoa kiasi cha shilingi Bilioni 3.
Amesem mpaka sasa jumla ya majengo yaliyokamilika ni 15 amesema Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga hadi sasa imeshapokea wajawazito 900 na kati yao 300 walijifungua kwa njia ya upasuaji ndani ya miaka mitatu(3).
Rais Samia amefanya uzinduzi wa hospitali hiyo akiwa katika ziara mkoani Tanga ambayo ameanza leo Februari 23, 2025 hadi Machi 1, 2025 kwa lengo la kukagua na kuzindua miradi mbaliambali iliyotolewa fedha na Serikali.

Katimba: Serikali imeendelea kuchukua hatua kupunguza uhaba wa walimu
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba, amesema serikali inaendelea kuchukua hatua za kukabiliana na upungufu wa walimu kwa kuajiri kila mwaka kulingana na upatikanaji wa fedha, huku kwa sasa ikiwa katika majaribio ya matumizi ya teknolojia ya madarasa janja.
Mhe. Katimba ameyasema hayo leo, Februari 22, 2025, alipokuwa akizungumza na Maofisa Elimu Kata waliokuwa wakipatiwa mafunzo ya matumizi ya Madarasa Janja katika Taasisi ya Elimu Kibaha, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuajiri walimu kila mwaka kwa kutoa vibali vya ajira, huku ikiimarisha utaratibu wa kuwatumia walimu wa kujitolea.
"Watanzania wamehamasika kupeleka watoto shule, na udahili wa wanafunzi umeongezeka maradufu, hali iliyosababisha upungufu wa walimu. Hivyo, serikali, pamoja na kuajiri, imebuni teknolojia ya kutumia madarasa janja, na kwa sasa ipo katika hatua za majaribio," amesema.
Pia, Mhe. Katimba amebainisha kuwa pamoja na jitihada hizo, serikali inaendelea kupandisha madaraja ya walimu kama sehemu ya motisha ya kiutendaji.

Wadau wahimizwa kuzingatia usawa wa kijinsia kwenye miradi ya maendeleo
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ustawi wa Jamii katika Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Subisya Kabuje, ametoa wito kwa wadau wanaotoa misaada kwa wanawake na vijana wa kike kuhakikisha wanawahusisha pia vijana wa kiume na wanaume katika vikundi vya maendeleo ili kuimarisha ustawi wa familia na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Kabuje ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kukagua shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Shirika la Brac Maendeleo katika Wilaya ya Singida Vijijini, mkoani humo.
Ameeleza kuwa vikundi hivyo vimekuwa vikipatiwa elimu na misaada mbalimbali, ikiwemo mafunzo ya ujasiriamali, ufugaji na usimamizi wa fedha, ili kusaidia familia zenye kipato cha chini kujikwamua kiuchumi.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa wataalamu wa maendeleo ngazi ya mkoa, halmashauri na vijiji kushiriki kikamilifu katika kusimamia uwekezaji wa miradi hiyo, kwani inasaidia jamii kupambana na umaskini.
Vilevile, Kabuje amewahimiza wazazi kuanzisha vituo vya kijamii vya kulelea watoto wadogo walio chini ya miaka mitano ili kuwasaidia wakati wanapokuwa kwenye shughuli za biashara au kilimo. Vituo hivyo vitatoa huduma muhimu za lishe, afya, ulinzi na ujifunzaji wa awali kwa watoto.
Kwa upande wake, Meneja wa Mradi huo, Rachel Mbwiliza, amesema mradi huo unalenga kusaidia watu wa rika mbalimbali, huku hatua ya awali ikitekelezwa katika Halmashauri za Wilaya ya Manyoni, Chamwino, na Singida Vijijin

Katimba:Serikali itawafikia vijana wapate elimu ya kudhibiti maambukizi ya VVU
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amesema Ofisi hiyo itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na wadau wa maendeleo kuhakikisha inawafikia vijana na kutoa Elimu ya tahadhari na Udhibiti wa maambukuzi ya Virusi vya UKIMWI katika jamii.
Mhe. Katimba ametoa kauli hiyo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa katika hafla ya uzinduzi wa awamu ya tatu ya mradi wa Timiza Malengo ambao ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni ya Tunasonga na Samia kutokomeza UKIMWI, katika uwanja wa Madini wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi.
Amesema mradi huo unalenga kumuelimisha kijana katika kujitambua na kuweza kujilinda na changamoto zinazochochea katika kujihusisha na tabia hatarishi zinazopelekea kupata maambukizi hasa ya virusi vya UKIMWI.
Aidha, Mhe. Katimba amewapongeza watendaji wote kwenye mradi huo hasa watumishi wa OR – TAMISEMI walioko kwenye Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kutoka Mikoa 10 na halamshauri 32 kusimamia mradi huo ili uendelea kuleta tija kwa maendeleo ya vijana wa Tanzania.
Kwa upande wake, mgeni Rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, amesema kiwango cha ushamiri wa maambukizi ya UKIMWI kwa umri wa miaka 15-49 kimepungua kutoka asilimia 4.7 kwa mwaka 2017 hadi asilimia 4.4 kwa mwaka 2023.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya, Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Godwin Mollel amesema gharama za matibabu kwa waathirika wa UKIMWI ni kubwa hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari ili kuepuka maambukizi

TAMISEMI yakusudia kuboresha zaidi huduma za macho Sekta ya Afya ya Msingi
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI, imesema itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za macho katika sekta ya afya ya msingi, kwa kuhakikisha miongozo na sera zinazoongoza utoaji wa huduma hizo zinaendelea kuboreshwa kwa manufaa ya wananchi.
Hayo yameelezwa leo Februari 20, 2025 jijini Dodoma na katibu Mkuu OR – TAMISEMI Adolf Ndunguru kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Idara ya Afya,Ustawi wa jamii,na Lishe Dkt. Rashidi Mfaume katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa macho imara, utakaotekelezwa katika mikoa minne ya Arusha, Singida, Tabora na Manyara.
Dkt. Mfaume amesema kutokana na eneo la afya ya macho kupewa kipaumbele cha chini, OR – TAMISEMI kwa kushirikiana na wizara ya Afya, na wadau mbalimbali imejipanga kuhakikisha huduma za macho zinajumuishwa katika mfumo wa afya ya msingi ili kuwafikia watoto wengi zaidi katika jamii.
Naye, Mkurugenzi wa huduma za uuguzi na ukunga Dkt. Ziada Sellah akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama, amesema inakadiriwa kuwa wastani wa watoto nane kati ya kila watoto 10,000 wenye umri wa miaka 0 -15, wana ulemavu wa kutokuona na idadi kubwa zaidi wana upungufu wa kuona.
“Serikali itaendelea kuboresha huduma za Uzazi, Mama na Mtoto ikiwemo za uchunguzi wa macho na kutoa afua sahihi kwa watoto tangu wakiwa tumboni mwa mama zao hadi wanapofika umri wa miaka mitano, kipindi hiki ni muhimu sana kwani ndio matatizo mengi yasababishayo ulemavu wa kutokuona hutokea,” amesema Dkt. Sellah
Awali, akitoa taarifa ya mpango huo, Daktari Bingwa wa macho kutoka Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Prof. Milka Mafwiri amesema lengo la mpango huo ni kupunguza ulemavu wa kutokuona unaozuilika kwa Watoto hapa nchini kwa kujumuisha afua za afya ya macho kwa watoto katika afya ya msingi hususani kwenye huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto.
Kwa mujibu wa Prof. Mafwiri mpango huo unaogharimu Sh.Bilioni 4.9 na utatekelezwa kwa muda wa miaka mitano katika halmashauri 16 za mikoa ya Arusha, Singida, Tabor ana Manyara.
Mpango huo uliopewa kaulimbiu ya uoni bora, Maisha bora, unakuja wakati ambao watoto milioni 1.4 duniani, wanakabiliwa na tatizo la kutoona huku nusu ya idadi hiyo wakiwa ni Watoto wanaoishi katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania.

Trilioni 1.3/- zatumika kuboresha afya ya msingi nchini
KATIKA kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kiasi cha Sh.Trilioni 1.3 kimetumika kufanya maboresho makubwa kwenye miundombinu ya kutolea huduma za afya, vifaa na vifaa tiba, dawa na ubora wa utoaji wa huduma za afya ya msingi nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume ameyasema hayo leo Februari 19, 2025 alipokuwa akizungumzia mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita katika utoaji wa huduma za afya ngazi ya msingi nchini.
Amesema fedha hizo zimetumika kufanya uwekezaji katika afya msingi na kuchangia ongezeko la miundombinu ambapo hadi sasa kuna zahanati 6163, vituo vya afya 932 na hospitali za Wilaya 188.
“Mpaka sasa kuna hospitali mpya za Wilaya 129 ambazo zimejengwa kwenye maeneo ya pembezoni, hospitali kongwe 48 zimeboreshwa, vituo vya kutolea huduma za afya 367 vyenye uwezo wa kufanya upasuaji, kuongeza, damu,” amesema.
Dkt. Mfaume amesema uwekezaji huo umesaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto kutoka vizazi hai 556 hadi 104 katika kila vizazi hai 1000.
Pia, amesema katika maeneo ya vijijini kulikuwa na changamoto kubwa ya kupeleka watumishi wa afya na ilitokana na kutokuwa na nyumba za kuishi lakini mpaka sasa Serikali imejenga nyumba 270 kwa ajili yao.
Pamoja na hayo, amesema Serikali imejenga majengo ya kutolea huduma za dharura 86, magari ya kubebea wagonjwa 382 yamesambazwa kwenye halmashauri zote huku kwa kipindi hicho watumishi 25,936 wameajiriwa.

Katimba atoa maelekezo kwa chuo cha hombolo kuwajengea uwezo viongozi wa mitaa na vijiji
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba ametoa maelekezo kwa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo kuwasiliana na Wakurugenzi Halmashauri zote nchini ambazo hazijatimiza maelekezo ya serikali ya kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa serikali za mitaa na vijiji ili wawezeshe kupata mafunzo hayo.
Mhe. Katimba ametoa maelekezo hayo baada ya kutembelea chuo hicho kilichopo Hombolo jijini Dodoma ikiwa ni ziara ya kikazi ya kutembelea taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na viongozi na watumishi wa taasisi hizo ili kupata mwelekeo wa kiutendaji wa Taasisi hizo.
"Mafunzo haya ni ya lazima sio ya hiari mfanye mawasiliano ili waweze kuhakikisha mafunzo haya yanaweza kufanyika kwa wenyeviti wetu hawa na mafunzo haya mnayotoa yana lengo zuri la kuwajengea uwezo wale watendaji wote waliopo huko kwenye mamlaka za serikali za mitaa waweze kutimiza majukumu yao kwa ufanisi," amesema
Amesisitiza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi yanatakiwa kuendana na mabadiliko ya kifikra ili mamlaka za serikali za mitaa zielewe kuwa pamoja na utoaji wa huduma kwa jamii bali ni chombo cha kuwezesha shughuli za kiuchumi.
"Mamlaka zetu za serikali za mitaa ziwe ni chombo cha kuchochea na kuwezesha wananchi katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali katika sekta mbalimbali najua mna'component' nyingi lakini katika eneo hili natoa msisitizo,"amesema Mhe. Katimba.

Samia bond yaorodheshwa dse
Samia Infastructure Bond hati fungani Mahususi inayotolewa na Benki ya CRDB, kwa ajili ya kufadhili miradi muhimu ya miundombinu nchini Tanzania, hasa ujenzi wa barabara chini ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), leo imeorodheshwa kwenye soko la hisa la Dar es Salaam, hatua hiyo imejiri baada ya kukusanywa kiasi cha bilioni 323 kutoka Taasisi mbalimbali na wawekezaji binafsi.
Zoezi hilo limeongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa kupiga kengele ikiwa ni ishara ya kuorodhesha Samia Infastructure Bond kwenye soko la hisa la Dar es Salaam.
Samia Infastructure Bond inatazamiwa kutatua changamoto ya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya malipo ya wakandarasi wanaotekeleza miradi ya barabara hivyo kuharakisha maendeleo ya miundombinu muhimu kwa usafirishaji wa abiria, mizigo na huduma na bidhaa

Waziri mchengerwa akutana na kampuni iliyoonesha nia kulifanya jiji la dar kuwa la kisasa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amekutana na wawakilishi wa Kampuni ya Straling Holding ya Abu Dhabi na kujadili namna bora ya ujenzi wa mji mpya wa kisasa katika Jiji la Dar es Salaam.
Waziri Mchengerwa amekutana na Kampuni ya Straling Holding leo tarehe 14.02.2025 kwenye ukumbi TAMISEMI jijini Dodoma ambao wameonesha nia ya kuwekeza kwenye ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja, elimu, afya, bandari, umeme wa maji, reli, mifumo ya umwagiliaji, madini na viwanda nchini.
Mhe. Mchengerwa amefanya kikao kazi na wawekezaji hao ili kuwa na uelewa wa pamoja juu ya shughuli wanazozifanya, ili kuona kama kuna haja ya kushirikiana nao katika ujenzi wa mji mpya wa kisasa katika jiji la Dar es Salaam kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa

Mchengerwa awaweka kikaangoni wakurugenzi watoto kusomea chini ya mti
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, ameagiza tathmini ifanyike kubaini maeneo ambapo wanafunzi wanalazimika kusoma chini au kukaa chini ya miti.
Pia, amewataka wakurugenzi wa halmashauri na wataalamu wao kuandikiwa barua za kujieleza juu ya hali hiyo.
Agizo hilo limetolewa leo, Februari 13, 2025, jijini Dodoma, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kukabiliana na msongo wa mawazo kazini kwa watumishi wa TAMISEMI.
Mchengerwa amesisitiza kuwa haiwezekani katika karne hii wanafunzi wakakosa madarasa au madawati, ilhali serikali imetumia matrilioni ya shilingi kuboresha sekta ya elimu.
"Miaka yote tumekuwa tukipata usumbufu ikifika Desemba na Januari, lazima zitafutwe sh. bilioni 250 au 300 kwa madarasa na madawati. Lakini sasa miaka miwili imepita hatujamuomba Rais fedha za kujenga madarasa au kununua madawati. Msisubiri msukumwe, fanyeni kazi," amesisitiza Mhe. Mchengerwa.
Ameagiza Idara ya Usimamizi wa Elimu ya TAMISEMI kufanya tathmini ya shule zote za msingi na sekondari zilizo chakavu ili kuweka mpango wa ukarabati.
Aidha, amewapongeza watumishi wa TAMISEMI kwa kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ufanisi na kuwataka kuendelea kutoa huduma bora zinazokidhi matarajio ya wananchi.
Kuhusu sekta ya afya, Mchengerwa ameeleza kuwa juhudi za TAMISEMI zimechangia kupunguza vifo vya mama na mtoto, huku akihimiza ufuatiliaji wa karibu kwa waganga wakuu wa mikoa na wilaya ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Aidha, amewahimiza watumishi hao kufuatiliwa kwa karibu Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya na kwenye vituo vya afya ili waongeze kasi ya kuwahudumia wananchi kwa weledi

Tamisemi yaweka wazi viwango vipya ujenzi wa madarasa na zahanati
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imefanya mapitio ya bajeti kwa kuzingatia muundo wa kanda na gharama za maisha ili kuhakikisha fedha zinazotengwa kwa miradi ya ujenzi zinatosheleza kukamilisha miundombinu muhimu.
Hivyo, kuanzia bajeti ya mwaka 2024/25, madarasa yatagharimu kati ya Sh.Milioni 22 hadi 25, huku ujenzi wa zahanati ukigharimu kati ya Sh.Milioni 284 hadi 358.
Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba, ameliambia Bunge leo Februari 13, 2025 alipokuwa akichangia taarifa ya mwaka ya utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).
Amesema hatua hiyo imetokana na serikali kubaini tofauti kubwa ya gharama za vifaa vya ujenzi kati ya kanda mbalimbali, hali iliyokuwa ikikwamisha utekelezaji wa miradi muhimu kama shule, zahanati na majengo ya utawala.
“Tumefanya maboresho ya bajeti ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa viwango sahihi. Kuanzia bajeti ya mwaka 2024/2025, madarasa yatagharimu kati ya shilingi milioni 22 hadi 25, huku ujenzi wa zahanati ukigharimu kati ya shilingi milioni 284 hadi 358,” amesema Mhe. Katimba.
Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya LAAC, Mhe. Halima Mdee, amesisitiza kuwa kuanzia mwaka wa fedha 2025/2026, taasisi zote za umma zinazotoa huduma katika Serikali za Mitaa zinapaswa kushirikiana katika kuandaa miundombinu muhimu kama barabara, umeme, na maji kabla ya kuanza miradi yoyote ya ujenzi.

Mchengerwa: Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kipaumbele kwa Serikali za Mitaa kuchochea maendeleo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuweka mkazo katika kuimarisha serikali za mitaa kama chachu ya maendeleo ya wananchi kwa kuongeza rasilimali, kuboresha mifumo ya utendaji, na kuimarisha uwajibikaji wa viongozi wa halmashauri.
Waziri Mchengerwa amesema hayo Machi 11, 2025 kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 39 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika jijini Dodoma.
“Maendeleo siyo ahadi, bali ni hatua zinazochukuliwa kila siku kwa vitendo. Tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha serikali za mitaa zinakuwa msingi wa maendeleo ya wananchi. Serikali yake imeonesha kuwa maendeleo yanaanzia chini kwenda juu, na kwa kuimarisha serikali za mitaa, tumewawezesha wananchi kushiriki moja kwa moja katika mchakato wa maendeleo,” amesema Mhe. Mchengerwa.
Ameeleza kuwa uwekezaji mkubwa umefanyika katika sekta ya elimu, afya, na miundombinu, hatua inayowezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi.
Aidha, Waziri Mchengerwa amewahimiza viongozi wa serikali za mitaa kuwa wabunifu, kuzingatia uadilifu katika utendaji wao, na kushirikiana na serikali kuu ili kuhakikisha maendeleo ya taifa yanapiga hatua kwa kasi zaidi.

TAMISEMI yakemea Wanasheria wa Halmashauri wasiowajibika
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba, amewataka wakuu wa Idara na Vitengo vya Sheria katika Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanazingatia weledi, uadilifu, na uwajibikaji katika majukumu yao ili kuepusha uzembe unaoigharimu serikali.
Akizungumza Februari 12, 2025 kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha siku mbili cha wakuu wa idara hizo jijini Dodoma, Mhe. Katimba amesema kuna uzembe wa hali ya juu katika usimamizi wa mashauri ya madai.
"Katika baadhi ya maeneo, mashauri ya madai yameendeshwa upande mmoja kwa zaidi ya miaka mitano na maamuzi kufikiwa dhidi ya serikali bila mwanasheria wa halmashauri husika kuhudhuria hata mara moja mahakamani," amesema.
Ameongeza kuwa serikali haiwezi kuvumilia uzembe huu, hasa pale ambapo halmashauri hulazimika kulipa mabilioni ya shilingi baada ya kushindwa kesi kwa sababu ya kutohudhuria mahakamani au kusimamia vibaya mashauri.
Mhe. Katimba pia amebainisha changamoto katika usimamizi wa mikataba, ambapo baadhi ya mikataba hufikia ukomo bila mamlaka husika kuchukua hatua mapema za kuongeza muda wake, hali inayosababisha utekelezaji wa majukumu nje ya utaratibu wa kisheria.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wakili Richard Odongo, amesema kikao kazi hicho kinalenga kujadili changamoto hizi na kuweka mikakati madhubuti ya kuongeza uwajibikaji na uadilifu katika sekta ya sheria ndani ya halmashauri.

Meneja tarura kilimanjaro aagizwa ukarabati barabara ya sonu-sawe
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange, amemuelekeza Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Kilimanjaro kuwasilisha maombi maalumu ya fedha kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Sonu kwenda Sawe ambayo imeharibika kutokana na mvua.
Dkt. Dugange ametoa maelekezo hayo Februari 10, 2025 alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Hai, Mhe. Saashisha Mafuwe aliyetaka kujua ni lini serikali itakarabati barabara hiyo ili iweze kupitika wakati wote.
Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, Dkt. Dugange alisema: "Namuelekeza Meneja wa TARURA mkoa wa Kilimanjaro na Meneja wa TARURA Wilaya ya Hai, kama hawajawasilisha maombi maalumu na tathmini ya mahitaji ya fedha, wafanye hivyo mara moja ili serikali ipeleke fedha kwa ajili ya kuirekebisha barabara hiyo."
Katika swali la msingi, Mbunge wa Kishapu, Mhe. Boniphace Butondo, amehoji lini serikali itapeleka fedha za dharura wilayani Kishapu kwa ajili ya matengenezo ya barabara zilizoathiriwa na mvua za El Nino mwaka 2023/24.
Dkt. Dugange akijibu swali hilo, amefafanua kuwa serikali tayari imepeleka sh. milioni 190 katika mwaka wa fedha 2023/24 kwa ajili ya matengenezo ya dharura kwenye baadhi ya maeneo, ikiwemo barabara ya Mwamakanga – Mwanghiri yenye urefu wa kilomita 4.5 pamoja na ujenzi wa makalavati saba.
Aidha, ameeleza kuwa TARURA Wilaya ya Kishapu inasimamia mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 1,024.66, ambapo kilomita 2 ni za lami, kilomita 405.64 ni za changarawe, na kilomita 617.02 ni za udongo. Katika tathmini ya mwaka 2023/24, serikali ilibaini kuwa Sh.Bilioni 2.55 zinahitajika kwa ajili ya ukarabati wa barabara hizo.
Dkt. Dugange amesisitiza kuwa serikali itaendelea kutekeleza matengenezo ya barabara zote zilizoathiriwa na mvua, kulingana na upatikanaji wa fedha.

Mkandarasi anayejenga barabara za tactic morogoro atakiwa kukamilisha kazi ndani ya miezi mitatu
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila amemtaka Mkandarasi M/s Jiangxi GEO Engineering Group anayejenga barabara ya Kihonda - VETA yenye urefu wa Km 12.85 kwa kiwango cha lami Manispaa ya Morogoro mkoani Morogoro kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa ubora unaotakiwa ndani ya miezi mitatu hadi kufikia mwezi Mei 2025.
Mhandisi Mativila ametoa agizo hilo kwa mkandarasi pamoja na Mhandisi Mshauri wa mradi huo katika ziara ya ukaguzi wa mradi huo unaotekelezwa kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Miji Tanzania (TACTIC) chini ya mkopo nafuu toka Benki ya Dunia.
“Nimekuja kutembelea moja ya miradi mikubwa ambayo serikali ya awamu ya sita inatekeleza kwa ajili ya kuleta maendeleo na ushindani katika miji 45 ya Tanzania iliyochanguliwa iwe na ushindani wa kuwa na miundombinu bora ikiwemo ya barabara kwa kiwango cha lami inayowezesha kukua kwa uchumi’’, alisema.
Alisema kati ya miji hiyo ni pamoja na Manispaa ya Morogoro ambayo inanufaika na utekelezaji wa mradi huo mkubwa ambapo kwa mkoa huo mradi unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 19.6.
“Mradi huu umechelewa na upo nyuma kwa asilimia 18 na kwamba umetekelezwa kwa asilimia 82 tu na kuna sababu kadhaa ambazo zimeelezwa, baada ya kuweka mambo sawa tunataka mradi huu ukamilike ndani ya muda wa miezi mitatu endapo kukiwa na mvua kubwa basi mradi uwe umekamilika Mwezi Augosti mwaka huu“, alisema .
Naye, Meneja wa TARURA Wilaya ya Morogoro, Mhandisi Mohamed Muanda alisema ujenzi wa mradi huo ulianza Oktoba 23, 2024 na kutakiwa kukamilika Februari 2025 ambapo awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa mifereji mikubwa ya maji ya mvua kuelekea mto Kikundi yenye urefu wa jumla ya Km 4.4, ujenzi wa ofisi ya Mhandisi Mshauri na ofisi ya wasimamizi wa miradi.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mhandisi Mshauri kutoka nchini pamoja na Mhandisi Mshauri kutoka Ethiopia (JV Core consultancy), Mhandisi Dargie Dilbedi alimhakikishia Naibu Katibu kwamba kazi hiyo ipo katika hatua ya mwisho na kwamba anatumaini ndani ya miezi mitatu ya nyongeza itakamilika.

Kamati ya bunge yaelekeza halmashauri zenye mapato makubwa kujenga uzio maeneo ya huduma za afya
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, imeielekeza Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuhakikisha Halmashauri zote nchini zenye mapato makubwa ya ndani zinajenga uzio katika maeneo ya kutolea huduma za afya kwa ajili ya usalama wa wananchi na mali za umma.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Justin Nyamoga ametoa maelekezo hayo wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya elimu na afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Mkoa wa Pwani.
“Tukipita kwenye maeneo mengi tunaona hospitali hazina uzio. Kutokana na maeneo mengi kuwa karibu na makazi ya watu, Kamati inashauri Halmashauri zenye mapato ya ndani ya kutosha zianze kujenga uzio kwenye maeneo ya huduma za jamii kama haya,” amesema Mhe. Nyamoga.
Ameongeza kuwa ni muhimu maeneo yanayotoa huduma za afya kuwa salama na kuhakikisha faragha kwa wagonjwa na wateja wanaoingia na kutoka.
Pamoja na hilo, Mhe. Nyamoga amezitaka Halmashauri zote nchini kufuata miongozo na taratibu katika matumizi ya fedha za miradi ya BOOST na SEQUIP, ili Watanzania waendelee kunufaika na juhudi za Serikali katika kuimarisha sekta ya elimu.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba, amepokea maelekezo hayo huku akisisitiza umuhimu wa Halmashauri kuendeleza miundombinu katika sekta nyeti, ikiwamo sekta ya afya.
Kamati hiyo imemaliza ziara yake ya siku mbili katika Mkoa wa Pwani, ambapo imetembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji wa Rufiji na Manispaa ya Kibaha.

Kamati ya bunge yapongeza rufiji kwa utekelezaji bora wa miradi
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, imeridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Rufiji, hususan ukarabati wa Hospitali ya Wilaya pamoja na miradi mingine ya afya, elimu, miundombinu na masoko.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Justin Nyamoga ameyasema hayo atika ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya afya, elimu, soko, jengo la utawala na miundominu ya barabara za TARURA inayotekelezwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI.
Mhe. Nyamoga amepongeza usimamizi mzuri wa miradi hiyo, akibainisha kuwa Rufiji imeonyesha mfano bora wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
"Mhe. Waziri, tumejionea kazi nzuri ya ukarabati wa hospitali ya Wilaya ya Rufiji. Tumefurahishwa na ubora wa mradi huu, hivyo tunakupongeza kwa usimamizi mzuri. Rufiji ni mfano wa kuigwa," amesema Mhe. Nyamoga.
Aidha, Mjumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Salome Makamba, ameeleza kuwa licha ya hospitali hiyo kujengwa mwaka 1963, ukarabati wake umefanyika kwa kiwango cha hali ya juu, jambo linaloonyesha utekelezaji mzuri wa miradi ya serikali.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu), Mhe. Zainab Katimba, ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, serikali imewekeza zaidi ya Sh.Trilioni 1.2 katika sekta ya afya, huku Rufiji pekee ikinufaika na uwekezaji wa Sh.Bilioni 8.3.
Mbunge wa Jimbo la Rufiji, ambaye pia ni Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, ameeleza kuwa pamoja na maboresho ya huduma za afya, Rufiji inaendelea kuwekeza katika miradi mikubwa ya maendeleo, ikiwamo ujenzi wa kiwanda kikubwa cha sukari, kiwanda cha ndizi kinachotarajiwa kutoa ajira zaidi ya 8,000, pamoja na ujenzi wa bandari ndogo ya Muhoro kwa ajili ya kusafirisha bidhaa za kilimo.
Ziara ya Kamati hiyo wilayani Rufiji ilihitimishwa kwa ukaguzi wa miradi mbalimbali, ikiwamo soko la Umwe, jengo la Halmashauri ya Mji, barabara za TARURA, na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Pwani – Bibi Titi Mohamed.

Anwani za makazi zaboresha usafirishaji wa dawa na vifaa vya shule nchini
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Dkt. Festo Dugange, amesema kuwa mfumo wa anwani za makazi umeleta mapinduzi makubwa katika usambazaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ya msingi nchini, kwani hakuna tena changamoto ya kutafuta au kuuliza eneo la zahanati au kituo cha afya kilipo.
Akizungumza leo Februari 8, 2025 kwenye kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Anwani za Makazi jijini Dodoma, Dkt. Dugange ameeleza kuwa pamoja na dawa, mfumo huu pia umewezesha vifaa na mahitaji muhimu ya shule kufikishwa katika maeneo husika kwa ufanisi mkubwa zaidi kuliko ilivyokuwa kabla ya utekelezaji wa mfumo huo.
Aidha, amebainisha kuwa Bohari ya Dawa ya Taifa (MSD) sasa inasambaza dawa moja kwa moja hadi kwenye zahanati katika maeneo yote ya Tanzania kwa kutumia anwani za makazi, jambo ambalo limeimarisha usambazaji wa dawa na huduma za afya kwa wananchi wa mijini na vijijini kwa kiwango kikubwa.
Dkt. Dugange amesisitiza kuwa mfumo wa anwani za makazi umewezesha maeneo yote nchini kufikika kwa urahisi zaidi, na Ofisi ya Rais - TAMISEMI itaendelea kusimamia na kuhakikisha utekelezaji wake unazidi kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mkandarasi anayejenga barabara za tactic jijini dodoma atakiwa kukamilisha ujenzi kwa wakati
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila amemuagiza Mkandarasi M/s China Geo-Engineering Corporation kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa barabara kiwango cha lami Km 10.21, mtaro wa maji ya mvua Ilazo Km 2.1, uboreshaji wa mabwawa ya kuhifadhi maji ya mvua (3), mitaro ya kutiririsha maji Km 2.81 pamoja na ujenzi wa jengo la usimamizi na uratibu wa miradi kwa wakati na ubora.
Mhandisi Mativila ametoa agizo hilo alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo jijini Dodoma ambayo inatekelezwa kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Miji Tanzania (TACTIC) chini ya mkopo nafuu toka Benki ya Dunia.
Naibu Katibu Mkuu ameeleza kuwa baada ya ukaguzi wa mradi huo amebaini kuwa ujenzi wa barabara, mifereji ya maji ya mvua pamoja na jengo la usimamizi na uratibu wa miradi upo nyuma ya muda kutokana na nguvu kazi hafifu, ukosefu wa vitendea kazi na kupelekea mradi huo ambao unapaswa kukamilika Februari 2025 kuonyesha ishara za kutofikia malengo ya kukamilika kwa muda na kuwanyima wananchi fursa ya kupata huduma ya barabara.
“Mradi upo asilimia 45% tu bado zimebaki 55% kazi kukamilika, mpaka leo zimebaki siku 13 tu ili mkataba ukamilike. Tumeongea na mkandarasi lakini tumeona sehemu kubwa ya ucheleweshaji wa kazi umesababishwa na mkandarasi mwenyewe kwa kushindwa kuweka nguvu kazi na vifaa vya kutosha, ametueleza anahitaji mwaka mwingine ili akamilishe kazi kiukweli ataongezewa muda lakini atapata adhabu ya kukatwa fedha kulingana na mkataba na pia atatakiwa afanye kazi usiku na mchana ili akamilishe kazi ndani ya muda mfupi na kwa ubora ule ule”. amesema

Waziri mchengerwa: muswada wa makao makuu dodoma uingie bungeni haraka
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohammed Mchengerwa, amemuelekeza Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo kuhakikisha Muswada wa Sheria ya Usimamizi na Uendelezaji wa Makao Makuu Dodoma unawasilishwa bungeni kabla ya kuvunjwa kwa Bunge la 12 mwaka huu.
Mhe. Mchengerwa ametoa agizo hilo leo, Februari 6, 2025 katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Soko Kuu la Majengo na vituo vya daladala jijini Dodoma kupitia mradi wa uboreshaji miundombinu ya Miji (TACTIC) awamu ya pili unaotekelezwa chini ya Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA).
Amesema Dodoma haiwezi kuwa Makao Makuu kwa matamko pekee, bali ni lazima kuwe na sheria rasmi itakayohakikisha hadhi yake inalindwa kwa vizazi vijavyo.
Amesema "Sheria hii iharakishwe kama zinavyoharakishwa sheria nyingine. Hatuwezi kusubiri tena. Tutamuomba Mheshimiwa Rais kwa hati ya dharura ili iwasilishwe bungeni kabla ya kuvunjwa kwa Bunge hili."

Majaribio ya utoaji wa barua za utambulisho kupitia napa yaonesha mafanikio
Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI imesema majaribio ya utoaji wa barua za utambulisho kwa njia ya kidijitali kwa kutumia mfumo wa anuani za makazi (NAPA) yameonesha mafanikio katika kurahisisha utoaji na upokeaji wa huduma za utambuzi.
Hayo yameelezwa leo Februari 6, 2025 na Naibu Waziri OR – TAMISEMI Dkt. Festo Dugange wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma katika uzinduzi wa wiki ya anuani za makazi kwa mwaka 2025 inayoenda sambamba na maonesho ya huduma mbalimbali zinazotolewa kupitia huduma ya mtandao kwa kutumia anuani za makazi.
Kwa mujibu wa Dkt. Dugange mbali na mafanikio makubwa yaliyo onekana katika hatua za awali za majaribio, mfumo huo wa NAPA umesaidi katika utekelezaji wa jukumu la kutoa majina ya mitaa na kugeuka nyenzo muhimu zaidi inayorahisisha utambuzi wa makazi, utoaji na upokeaji wa huduma mbalimbali.
Kutokana na ufanisi huo, Dkt. Dugange amewaelekeza Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kuwaruhusu, kuwahamasisha na kuwahimiza waratibu wa mfumo huo katika maeneo yao kushiriki mafunzo ya mara kwa mara yanayolenga kuboresha utoaji wa huduma kupitia mfumo wa NAPA, ili wawe msaada wa kuwawezesha wananchi kutambua anuani zao.
Kadhalika ameeleza kuwa OR – TAMISEMI itaweka mazingira ya kutoa msaada wa kiufundi pale inapohitajika wakati wote, ikiwa ni hatua ya kudhibiti changamoto zinazo weza kujitokeza.
Kwa upande wake waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa amepongeza ushirikiano uliopo baina ya wizara hizo mbili akieleza namna unavyorahisha utekelezaji wa mfumo huo wa anuani za makazi.
Maadhimisho ya wiki ya anuani za makazi kwa mwaka 2025 yamebebwa na kauli mbiu ya “Tambua na tumia anwani za makazi kurahisisha utoaji na upokeaji wa huduma”.

Uandikishaji wa wanafunzi ufanyike bila kujali tofauti zao’ mhe mchengerwa
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaagiza Viongozi wa Mikoa na Halmashauri zote nchini kuhakikisha uandikishaji wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari unafanyika bila kujali tofauti zao za kiafya na kimaumbile.
Mhe. Mchengerwa ametoa maagizo hayo leo Januari 6, 2025 wakati wa hafla ya kukabidhi vyumba 18 vya madarasa vilivyogharimu Shilingi milioni 300 katika Halmashauri ya Wiaya ya Bahi ambapo pia ametoa tuzo kwa waandishi 15 wa habari za Mradi wa Shule Bora.
'Nawaagiza mkasimamie kwa dhati zoezi la uandikishaji wa wanafunzi wote bila kujali tofauti zao za kiafya na kimaumbile wenye umri lengwa kwa ajili ya kuanza darasa la awali, msingi na MEMKWA' amesisitiza.
Mchengerwa amewataka Viongozi hao kutoa takwimu sahihi za uandikishaji na jinsi wanavyoripoti wanafunzi katika ngazi ya elimu ya awali, msingi na sekondari kama ilivyoelekezwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Kila siku ya Ijumaa katika wiki).
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amempongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Elimu ambayo yameleta matokeo makubwa ikiwemo kuongeza ufaulu Dodoma kwa shule za msingi na sekondari na kupunguza utoro kutoka wanafunzi 24,000 hadi 6,000 (2024).
Akitoa taarifa kuhusu umalizaji wa ujenzi wa madarasa hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi, Zaina Mlawa alisema ujenzi wa madarasa 10 umefanyika kwa kufuata mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji ambao unalengo la kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.
Naye Mwakilishi wa Balozi kutoka ubalozi wa Uingereza, Sally Hedley alisema elimu ni kipaumbele kwa serikali hiyo hivyo nchi hiyo itaendelea kuwekeza katika sekta hiyo kwa kuweka miradi rafiki ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa wanafunzi.
Mradi wa Shule Bora umejikita katika kuboresha elimu ya awali na msingi kwa katika maeneo manne ya ujifunzaji, ufundishaji, ujumuishi na uimarishaji wa mifumo na ulizinduliwa rasmi na Vicky Ford (Parliamentary Under Secretary State-UK) Aprili 4, 2022 katika shule za Msingi Mkoani iliyopo Kibaha- Pwani. Mikoa unapotekelezwa Mradi ni Dodoma, Singida, Pwani, Tanga, Simiyu, Kigoma, Katavi na Rukwa ambapo uchaguzi wa mikoa hii ulizingatia mambo mbalimbali ikiwemo ufaulu usioridhisha wa wanafunzi katika mitihani ya kuhitimu darasa la saba na ile ya upimaji wa darasa la Nne, utoro na mimba za utotoni.

Simamieni miradi kikamilifu na kwa ubora – mhandisi mativila
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila, amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi wa Sekta ya Miundombinu katika Sekretarieti za Mikoa kusimamia miradi kikamilifu kwa mujibu wa mikataba ili kuhakikisha zinakuwa na ubora.
Mhandisi Mativila ametoa maelekezo hayo leo Februari 5, 2025 kwenye kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma, kilicholenga kujadili utekelezaji wa miradi ya ujenzi, ukarabati, na matengenezo ya miundombinu katika Mikoa 26, Wilaya 139, na Halmashauri 184 nchini.
"Ubora wa kazi ni jambo la msingi. Kama ni jengo, lijengwe kwa viwango vinavyostahili. Kuna baadhi ya majengo yanapotembelewa na waheshimiwa wabunge, hubainika kuwa hayana ubora," amesisitiza Mhandisi Mativila.
Aidha, amewataka viongozi hao kuwa na mipango thabiti ya muda mfupi, muda wa kati, na muda mrefu ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, kama ilivyokusudiwa na serikali.
Mhandisi Mativila amewasihi kuboresha utendaji wao kwa lengo la kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa watanzania wa mijini na vijijini.
Naye, Katibu Tawala Msaidizi wa Miundombinu wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Ezron Kilamhama, ameahidi kushirikiana na wahandisi wa halmashauri kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa mujibu wa mikataba na kwa viwango vinavyostahili.
Msanifu Majengo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Chabu Nghoma, amesema wataandaa mpango kazi wa utekelezaji wa miradi kwa ufanisi na kuuwasilisha kwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI ndani ya mwezi wa pili kwa ajili ya tathmini.
Ofisi ya Rais – TAMISEMI ina jukumu la kuratibu matengenezo, ukarabati, na ujenzi wa miundombinu ya barabara, majengo, na miundombinu mingine katika ngazi za mikoa, wilaya, na mamlaka za serikali za mitaa.

Miradi yote ngazi ya msingi itangazwe kupitia nest
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na wakuu wa vitengo vya manunuzi kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa kwenye ngazi ya msingi inatangazwa kupitia mfumo wa Nest.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati akizungumza na Wabunge,Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala Wasaidizi Miundombinu na wakuu wa vitengo vya manunuzi kutoka kwenye Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wakati wa kikao kazi kuhusu mfumo wa Nest kilichofanyika kwenye ukumbi wa wa Mabeyo jijini Dodoma leo tarehe 04.02.2024.
Amesema baada kupata mafunzo haya leo hii nendeni mkabadilike, fuateni Sheria ya Manunuzi, onyesheni mabadiliko hayo kwenye utekelezaji wa miradi na kuanzia sasa miradi yote itangazwe kupitia mfumo wa Nest na si vinginevyo alisisitiza.
Miradi hiyo ikishatangazwa kupitia Nest hakikisheni mnaisimamia kwa Weledi wa hali ya juu na kwa uaminifu ili itekelezwe kwa viwango vinavyotakiwa na thamani ya fedha iweze kuonekana’ amesema!
Aidha Mhe. Mchengerwa aliwataka PPRA kuhakikisha inawajengewa uwezo watumiaji wa mfumo wa Nest katika ngazi za msingi ili kupunguza changamoto zinazojitokeza wakati wa kuomba zabuni mbalimbali.