
WARATIBU WA HUDUMA ZA MACHO WAASWA KUJUMUISHA HUDUMA ZA MACHO KWENYE BAJETI ZA HALMASHAURI
Waratibu wa huduma za macho kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa wameaswa kuendelea kujumuisha huduma za macho katika Mipango na Bajeti za Halmashauri ili kuhakikisha urahisi wa upatikanaji wa huduma bora za afya ya macho kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Dkt. Ernest Kisandu, ambaye alizungumza kwa niaba ya mratibu wa macho kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, katika kambi ya matibabu ya mtoto wa jicho inayoendelea katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe.
Dkt. Kisandu alisisitiza kwamba kuendelea kwa mipango ya huduma za macho kwenye bajeti za Halmashauri kutasaidia kupunguza changamoto zinazohusiana na matatizo ya macho, hasa kwa watoto kwani itahakikisha huduma hizi kupatikana kwa watu wengi na kuifanya afya ya macho kuwa sehemu ya huduma muhimu za afya za jamii.
Naye Afisa wa Programu kutoka Hellen Keller International, Bw. Allen Lemilia, amesema kambi hiyo ya siku sita, imekuwa na mwitikio mkubwa kutoka kwa wananchi wa Halmashauri ya Mbozi na maeneo jirani na imepata ushiriki mkubwa kutoka kwa jamii na inatarajiwa kutoa huduma kwa watu wengi zaidi.
Kambi hiyo ya matibabu inaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Afya, na wadau wa Helen Keller International, ina lengo la kufikia watu 720 wenye matatizo ya mtoto wa jicho, ambapo hadi sasa jumla ya watu 412 wamepatiwa huduma.
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2
Habari na Matukio
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.




