
WALIMU MAHIRI WANOLEWA KUTENGENEZA ZANA BORA ZA KUFUNDISHIA KIGOMA
Mafunzo ya uandaaji na utengenezaji wa zana za kufundishia na kujifunzia kwa Walimu mahiri wa darasa la kwanza yaliyoanza jana Oktoba 08, 2025 katika Shule ya Msingi Kigoma tayari yameanza kuonyesha mafanikio.
Mafunzo hayo yanafanyika kwa Walimu wa Shule za Msingi za Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma chini ya Mradi wa Shule Bora.
moja ya washiriki wa mafunzo hayo ni Mwalimu Jetta Ndororo na Mwalimu Metus Steven wanasema mafunzo hayo yanawajengea uwezo wa uandaaji wa zana za kufundishia na kujifunzia zinazorahisisha na kukuza viwango vya ujifunzaji wa Kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) kwa wanafunzi wa darasa la kwanza.
Shule Bora ni programu ya elimu inayofadhiliwa na Serikali ya Uingereza chini ya Idara ya maendeleo ya Kimataifa (FCDO) na inashirikiana na ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia huku ikilenga kuboresha elimu katika shule za Serikali kwa ngazi ya Elimu ya Awali na msingi nchini Tanzania.
Comments
Please sign in to leave a comment.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2