
WAKUU WA IDARA WAASWA KUSIMAMIA NA KUIMARISHA UKUSANYAJI WA MAPATO KATIKA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA
Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Bi. Beatrice Kimoleta, amewahimiza wakuu wa Idara na Vitengo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanashirikiana kwa karibu miongoni mwao katika usimamizi wa miradi na ukusanyaji wa mapato.
Akifunga mafunzo awamu ya pili ya Uongozi kwa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa yalioratibiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi (UONGOZI INSTITUTE) yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kilichopo Kibaha mkoani Pwani, Bi. Kimoleta ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, amewahimiza viongozi hao kuhakikisha wanayatumia mafunzo hayo kuboresha mikakati ya ukusanyaji wa mapato ili kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
“Hakikisheni mnashirikisha menejimenti yote katika ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa miradi pamoja na kuhakikisha Kamati za Bajeti zinatumika katika kugawana rasilimali fedha na rasilimali nyingine na zifanye kazi zao ipasavyo”, Amesema
Aidha, Bi. Kimoleta ameendelea kusisitiza kuwa Ofisi ya Rais - TAMISEMI inaendelea kuwahimiza viongozi hao wa mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha bajeti zinaandaliwa kuzingatia uhalisia wa mapato, vipaumbele vya wananchi na ushirikishwaji wa wadau.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Bi. Angelista Kihaga amesisitiza la kila mkuu wa idara kuendeleza elimu na maarifa waliyopata kwa kuwafikia watumishi wengine ndani ya Halmashauri zao na kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoathiri utendaji kazi wao.
Naye Emmanuel Tesua, Kaimu mkurugenzi wa Mafunzo kutoka Taasisi ya Uongozi amesema taasisi hiyo imetoa mafunzo hayo kwa kuzingatia mahitaji ya washiriki na wanaamini mafunzo waliyotoa yatakwenda kuimarisha utendaji kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa.
Mafunzo ya awamu ya kwanza yalianza Agosti 29 hadi 30, 2025 na awamu ya pili yalianza Septemba 02, 2025 na yamehitimishwa leo Septemba 04,2025 yakihusisha wakuu wote wa Idara na Vitengo kwa Halmashauri 12 za Majiji na wilaya
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2