
WAKUU WA IDARA NA VITENGO WAASWA KUSHIRIKIANA KIUTENDAJI
Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Bi. Angelista Kihaga amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanyakazi kwa ushirikiano ili kutimiza lengo la Serikali la kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi walioko katika halmashauri zote nchini.
Bi. Kihaga ametoa wito huo kwa viongozi hao leo Agosti 30, 2025 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo ya uongozi ya kuwajengea uwezo kiutendaji ambayo yanatolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Taasisi Uongozi katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kilichopo Kibaha, mkoani Pwani.
Aidha, Bi. Kihaga amefafanua kuwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI inatoa mafunzo hayo kwa viongozi hao ili kuwapatia fikra mpya za uongozi, ujuzi na maarifa ambayo yataboresha utendaji kazi wao na kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji miongoni mwao.
Katika mafunzo hayo mada mbalimbali zinaendelea kuwasilishwa na wataalamu wabobezi katika sekta ya umma, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara na Vitengo hao utakaowawezesha kusimamia utoaji wa huduma bora kwa wananchi katika maeneo yao ya utawala.
Comments
Please sign in to leave a comment.