
USHIRIKIANO WA SERIKALI NA HELEN KELLER INTERNATIONAL WAENDELEA KULETA MATOKEO YA KISERA KWENYE AFYA NA LISHE
Na OR-TAMISEMI
Mkuu wa Kitengo cha Uboreshaji wa Miundo ya kimenejimenti kutoka Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Peter Mhimba, amepokea ugeni kutoka Shirika la Kimataifa la Helen Keller International ukiongozwa na Rais wa shirika hilo, katika ziara iliyolenga kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Adolf Ndunguru katika kikao hicho, Bw. Mhimba amesema ujio wa viongozi hao wa juu ni uthibitisho wa uhusiano wa muda mrefu na wa mafanikio kati ya Serikali ya Tanzania na shirika hilo, ambalo limekuwa mshirika wa maendeleo kwa zaidi ya miaka 40 katika sekta ya afya, lishe, na mapambano dhidi ya magonjwa yaliyopuuzwa.
Amebainisha kuwa shirika la Helen Keller International limechangia pakubwa kuboresha huduma za afya ya macho, lishe na kutokomeza ugonjwa wa trakoma. Zaidi ya watoto 480,000 wamepatiwa dozi ya vitamini A, huku watu 12,000 wakipata huduma za upasuaji wa macho — wakiwemo watoto 35 waliorejeshewa uwezo wa kuona.
"Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, shirika hilo limewajengea uwezo wataalam wa afya 2,160 katika mikoa sita, na kutoa vifaa tiba vya kisasa katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Mbeya. Kwa upande wa lishe, zaidi ya wahudumu wa afya 900 na wafanyakazi wa kijamii 1,400 wamepewa mafunzo ya kutoa huduma bora za lishe kwa jamii za vijijini".amesema Mhimba
Bw. Mhimba ameongeza kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI itaendelea kushirikiana kwa karibu na Helen Keller International katika kuimarisha huduma za msingi za afya na lishe, hasa katika ngazi ya jamii kupitia vituo vya kutolea huduma vya msingi.
Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Mhimba ametoa shukrani kwa shirika hilo kwa mchango wake mkubwa, akieleza kuwa mafanikio yaliyopatikana ni ushahidi wa mshikamano wa kweli katika kuwatumikia wananchi.
Aidha, amesisitiza kuwa umoja ni nguvu, kama alivyonena Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akieleza kuwa kauli hiyo inabeba ujumbe mkubwa wa kisera na maendeleo.
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2




