
Tanzania Yaitandika Kenya 5–2 kwenye Mpira wa Goli FEASSA 2025
Na OR- TAMISEMI, Kenya
Tanzania imeichapa Kenya mabao 5–2 na kuibuka mshindi katika mchezo wa mpira wa goli (Goalball) kwa shule za msingi, mchezo ulioshirikisha timu kutoka Tanzania, Kenya na Uganda kwenye mashindano ya michezo ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (FEASSA) yanayoendelea mjini Kakamega, Kenya.
Ushindi huo umeiwezesha Tanzania kutwaa kombe la ubingwa wa mpira wa goli upande wa shule za msingi, huku ikisalia na michezo mitatu mkononi dhidi ya Kenya kwa ngazi ya sekondari wavulana, wasichana pamoja na msingi wavulana.
Mwaka jana, Tanzania pia iliibuka bingwa wa kwanza katika mchezo huo wa mpira wa goli kwenye michezo ya FEASSA iliyofanyika Bukedea, Uganda.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo huo, Mratibu wa Mpira wa Goli Tanzania, Anita Mlay, alisema mashindano hayo si tu yanaziunganisha nchi wanachama, bali pia yanatoa ujumbe muhimu kwa jamii kwamba watoto wenye mahitaji maalum wana uwezo mkubwa wa kushiriki na kushinda katika michezo mbalimbali.
Ametoa wito kwa jamii kuacha kuwaficha watoto wenye ulemavu majumbani na badala yake wawape nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kupitia michezo.
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2




