
TANZANIA YABEBA KOMBE LA KWANZA LA KRICKETI FEASSA 2025
Na OR TAMISEMI, Kakamega, Kenya
Tanzania imeandika ukurasa mpya wa historia katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Shule za Msingi na Sekondari Afrika Mashariki (FEASSA 2025) baada ya timu ya wasichana kutwaa ubingwa wa kwanza kabisa wa Kriketi, mchezo ambao umejumuishwa kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa mashindano haya.
Katika mchezo wa fainali uliopigwa mjini Kakamega, Kenya ilimaliza kwa Runs 80, Wickets 8, Overs 20, lakini Tanzania iliwapiku kwa kishindo kwa kufunga Runs 81, Wickets 5, Overs 17, na kuandika historia ya kuwa mabingwa wa kwanza wa Kriketi wa FEASSA.
Kwa upande wa wavulana, Tanzania ilipambana vikali dhidi ya Uganda kwenye fainali yenye mvuto mkubwa. Tanzania ilimaliza kwa Runs 84, Wickets 9, Overs 20, lakini Uganda iliibuka na ushindi baada ya kufunga Runs 85, Wickets 9, Overs 18, hivyo kuibuka mabingwa wa kwanza wa Kriketi upande wa wavulana.
Kujumuishwa kwa mchezo wa Kriketi katika mashindano haya kumetoa fursa mpya ya kukuza vipaji na kuendeleza michezo mbalimbali miongoni mwa vijana wa Afrika Mashariki. Kwa Tanzania, ushindi wa wasichana ni kumbukumbu ya kipekee itakayokumbukwa katika historia ya michezo ya shule za msingi na sekondari.
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2




