
TANZANIA YAANZA KUNG’ARA MASHINDANO YA FEASSA NCHINI KENYA
Tanzania inaendelea kuonesha uwezo mkubwa katika mashindano ya Federation of East Africa Schools Sports Association (FEASSA) yanayoendelea mjini Kakamega, Kenya.
Katika michezo ya soka, Benjamin Mkapa Sekondari, imeanza kwa kishindo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya E.P.M Mpanda kutoka Burundi, ushindi unaoipa nafasi nzuri kwenye kundi lake.
Mchezo mwingine wa kundi A ulimalizika kwa sare ya 0-0 kati ya Butere Wavulana HS (Kenya) na Kizuka Sekondari (Tanzania), huku pande zote zikionesha ushindani mkubwa.
Kwa upande wa soka la wasichana, Fountain Gate kutoka Tanzania ililazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Kabala Sekondari ya Kenya katika mchezo wa kundi B, wakati timu ya Nasokol Wasichana ikitoshana nguvu na Alliance Sekondari kwa sare ya 0-0 katika kundi A.
Mashindano ya FEASSA 2025 yamekusanya timu kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki, zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, na Burundi, yakiwa ni jukwaa la kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo kwa vijana wa shule za msingi na sekondari katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2