
TANZANIA NA BURUNDI ZAZINDUA UJENZI WA RELI YA SGR UVINZA - MSONGATI KM.300
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana Jamhuri ya Burundi leo Agosti 16, 2025 zimeshiriki hafla ya uwekaji jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa kipande cha Uvinza mkoa wa Kigoma hadi Musongati nchini Burundi.
Mradi wa SGR Uvinza–Musongati wenye urefu wa kilomita 300 umezinduliwa na Rais wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye na Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimuwakilisha Rqis Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika kipande hicho cha reli kilomita 240 ni njia kuu na kilomita 60 ni njia za kupishania pamoja na stesheni za mizigo na abiria.
Viongozi mbalimbali kutoka Tanzania na Burundi wameshiriki hafla hiyo akiwemo Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba akimwakilisha Mhe. Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI.
Mradi huu kwa upande wa Tanzania kitakuwa na urefu wa kilomita 190 wakati kipande cha Musongati (Burundi) kitakuwa na urefu wa kilomita 110 na unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa gharama ya dola za Marekani bilioni 2.54.
Comments
Please sign in to leave a comment.