
TAMISEMI YAWAHUDUMIA WANANCHI ZAIDI YA 9000 KWENYE MAONESHO YA NANE NANE DODOMA
Na Angela Msimbira OR-TAMISEMI
Wananchi zaidi ya 9000 waliotembelea banda la Ofisi ya Rais -TAMISEMI wakati wa Maonesho ya Wakulima (Nane Nane) yanayoendelea jijini Dodoma, wamehudumiwa moja kwa moja kwa kupewa elimu, huduma na ufafanuzi wa utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya serikali kupitia Ofisi ya Rais -TAMISEMI.
Ofisi ya Rais - TAMISEMI inayowahudumia wananchi kupitia mikoa na halmashauri imetumia jukwaa hilo muhimu kuwasogezea wananchi huduma ya elimu kuhusu mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Sanjari na hilo, imetoa elimu ya matumizi ya Mfumo wa TAUSI, mwongozo wa ununuzi wa viwanja ikiwa ni pamoja na masuala mengine yanayosimamiwa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI.
Akizungumza katika maonesho hayo, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia TAMISEMI, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Bw. Sospeter Mtwale, aliwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kupata huduma, akibainisha kwamba ofisi hiyo itaendelea kuwa kiunganishi muhimu kati ya serikali kuu na wizara mbalimbali ili kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi kwa wakati.
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2