
TAMISEMI YASHIRIKI WARSHA YA ESP KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI
Warsha ya siku tatu ya kuwajengea uwezo washauri wa programu ya Empowerment through Skills Program (ESP) imeanza leo Jijini Mwanza.
Warsha hiyo inalenga kuwaandaa washauri watakaowaongoza wanawake na wasichana waweze kuhitimu kozi fupi za Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC), kwa kuzingatia usawa wa kijinsia, haki za binadamu na maadili ya kazi.
Washauri wanaoshiriki wanatoka Mikoa ya Kigoma, Mara, Kagera, Tanga na Dodoma, wakiwa na utaalamu katika fani kama ufugaji, ushonaji, umeme na biashara ndogo ndogo.
Aidha, Kupitia warsha hiyo iliyoanza tarehe 30, Septemba hadi tarehe 02, Octoba, 2025 inalenga kuwajengea uwezo washauri hao kuwasaidia wahitimu kuelewa soko la ajira na kujipanga kwa ajili ya ajira au kujiajiri.
Utekelezaji wa ESP kwa sasa umefika hatua ya ushauri kwa wanafunzi, hatua muhimu katika kuwajengea uwezo wa kujitegemea.
Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeshiriki kikamilifu kama mdau mkuu wa uwezeshaji wa kiuchumi kupitia mikopo ya asilimia 10 ambayo hutolewa na Halmashauri inayolenga kuwakwamua kiuchumi wahitimu wa kozi za muda mfupi wanaofadhiliwa na Programu ya ESP ambao ni kundi la vijana lengwa wa mikopo hiyo.
Ushirikiano wa wizara mbalimbali zikiwemo Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum zimeonesha dhamira ya Serikali katika kuhakikisha wanawake na wasichana wanashiriki kikamilifu kwenye maendeleo ya Taifa kupitia elimu na ujuzi wa vitendo.
Comments
Please sign in to leave a comment.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2