
TAMISEMI, BIG WIN PHILANTHROPY WAANDAA MPANGO JUMUISHI KUKABILIANA NA UDUMAVU NA KUBORESHA LISHE
Ofisi ya Rais TAMISEMI, kwa kushirikiana na Shirika la Big Win Philanthropy, wamefanya kikao kazi cha kuandaa Mpango Jumuishi wa utekelezaji wa Afua za Lishe kwa Mikoa ya Iringa, Tabora na Geita. Mikoa hiyo imechaguliwa kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto walio na udumavu na waliochini ya umri wa miaka mitano huku lengo likiwa ni kuboresha hali yao ya lishe.
Kikao hicho kimeongozwa na Bw. Mwita Waibe, ambaye ni Mratibu wa Mradi huo kutoka OR - TAMISEMI, Huku kikihudhuliwa na Dkt. Taye Balcha, Mkurugenzi Mkuu wa Programu kutoka Shirika la Big Win Philanthropy, Bw. Vikram Mand Meneja uendeshaji kutoka Big Win philanthropy, pamoja na Maafisa na washauri wa lishe kutoka Mikoa husika, wakiwa na lengo la kuweka misingi thabiti ya mpango huo muhimu.
Kwa pamoja, washiriki walijadili mikakati ya kuhakikisha kuwa programu inafikiwa kikamilifu na kuwafikia watu wanaolengwa. Hii inaendezeleza jitihada za Serikali za kukabiliana na changamoto za lishe na udumavu kwa kutumia mbinu za ushirikiano imara.
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2
Habari na Matukio
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.




