
TAMISEMI, BENKI YA DUNIA WATETA KUHUSU MRADI WA MAJI SAFI NA MAJI TAKA
Timu ya Benki ya Dunia mapema leo wamekutana na baadhi ya Viongozi wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa lengo la kujadili maswala mbalimbali yanayohusu Mradi wa Uendelevu wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Sustainable Rural Water Supply and Sanitation - SRWSSP).
Mradi huo mkubwa umeshachangia ujenzi wa miundombinu mikuu ya maji, vyoo bora, na huduma za Usafi wa Mazingira (WASH) katika maeneo muhumu ya kijamii.
Hadi sasa, mradi huo umewafikia wananchi kwa kujenga miundombinu hii katika vituo vya kutolea huduma za afya 3,263 na shule za msingi 2,123 nchini.
Kikao hiki kinalenga kutathmini hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huu. Lengo kuu ni kutafakari mafanikio na changamoto zilizokabili mradi katika utekelezaji na kuboresha mikakati ya utekelezaji wake katika hatua za mbele.
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2




