
Prof. Nagu apokea ujumbe kutoka Big WIN Philanthropy
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI (AFYA) Prof. Tumain Nagu amepokea ujumbe kutoka Shirika la Big Win Philanthropy wakiongozwa na Dkt. Taye Balcha, Mkurugenzi Mkuu wa Programu, mapema leo walipomtembelea ofisini kwake katika jengo la Sokoine Jijini Dodoma.
Mbali na mazungumzo yao, Prof. Nagu amelishukuru Shirika hilo kwa jitihada zake katika kupambana na changamoto mbalimbali kwenye Sekta ya Afya kama vile udumavu.
Amesema, kwa kufanya hivyo wanaunga mkono moja kwa moja jitihada za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa kinara katika kupambana na changamoto za lishe nchini.
Ameongeza kuwa, Ofisi ya Rais – TAMISEMI itaendelea kishirikiana kwa ukaribu na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini kufanikisha malengo yao ya kuwasaidia wananchi kwa niaba ya Serikali katika maeneo husika.
Kwa upande wake, Dkt. Taye Balcha, Mkurugenzi Mkuu wa Programu kutoka Big Win Philanthropy amesema Big Win itaendelea kushirikina na Serikali ya Tanzania katika Sekta mbalimbali kwa kuunga mkono jitihada zinazofanya na Serikali ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
Comments
Please sign in to leave a comment.