
Mwambene Awapokea Mabingwa wa Taifa wa Netiboli, TAMISEMI Queens
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI (ELIMU) Bw. Atupele Mwambene ameipokea timu ya TAMISEMI Queens ambayo ilikuwa ikishiriki Ligi ya Netiboli Daraja la Kwanza Tanzania Bara na kufanikiwa kutwaa ubingwa huo.
Mashindano hayo yalihusisha timu 13 huku TAMISEMI Queens ikiibuka na ubingwa kwa kushinda jumla ya michezo 12 huku ikitoa mfungaji bora na mchezaji bora wa mashindano hayo lakini pia kuchangia wachezaji saba watakaojiunga na Timu ya Taifa Queens kwa ajili ya michezo ijayo ya Netiboli Kimataifa.
Mashindano ya Netiboli Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, yalifanyika mkoani Tabora kuanzia tarehe 26 Septemba hadi tarehe 6 Oktoba, 2025 na kufikia tamati hapo jana.
Comments
Please sign in to leave a comment.