
MTWALE AHIMIZA LUGHA ZA STAHA KWA WATUMISHI WA SERIKALI ZA MITAA.
Na OR- TAMISEMI, Pwani
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Serikali za Mitaa, Sospeter Mtwale amewahimiza Wakuu wa Idara na Vitengo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutotumia lugha zisizo na staha kwa wananchi na watumishi wanaowasimamia.
Mtwale amesema hayo wakati wa kufungua mafunzo ya Uongozi kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa yalioratibiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na UONGOZI INSTITUTE, ambayo yameanza leo tarehe 29 Agosti, 2025 katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kilichopo ya Kibaha mkoani Pwani ambapo amehimiza kupunguza malalamiko yanayotolewa na watumishi wa ngazi za chini na wananchi.
“Tumezoea kupata mafunzo mara nyingi yanayohusu kada zetu tunazozisimamia katika kila idara, lakini mafunzo haya yamebuniwa kuwawezesha Wakuu wa Idara na Vitengo kuwa na uwezo wa kiuongozi ili kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi na uadilifu,” amefafanua Mtwale.
Katika kusisitiza umuhimu wa uadilifu katika uongozi, Mtwale amesema mafunzo yanayotolewa yanalenga kuongeza uhodari na ujuzi katika utendaji wa kazi katika kutatua changamoto zilizobainika katika utekelezaji wa majukumu.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani, Pili Mnyema amesema mafunzo haya yatasaidia kubadilika kifikra na utendaji wa watumishi na amewasihi viongozi wanaopata mafunzo hayo kuwa kielelezo cha uongozi kwa wengine
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2
Habari na Matukio
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.




