
Mradi wa Barabara ya Kyema - Katerelo wafikia Asilimia 80
Bukoba - Kagera
Mradi wa Barabara inayowaunganisha wananchi wa kata ya Katerelo na Kata za Bujugo na Kasharu Maarufu kama Kyema-Katerelo unaotekelezwa na Wakala ya Barabara za mjini na vijijini (TARURA) kwa kiwango Cha Lami kilometa 0.55 chini ya mkandarasi wa ndani Kashico LTD umefikia asilimia 80
Meneja wa TARURA wilaya ya Bukoba Mhandisi Emmanuel Yahana amesema mradi huo umetekeleza kigezo namba 2.2 cha Mwenge wa Uhuru na sera ya barabara na mradi ulianza kutekelezwa Agosti 16 mwaka 2024 ukitarajiwa kukamilika Octoba 2025.
Amesema mradi huo unazisaidia kata hizo kufuata huduma katika Halmashauri ya Bukoba huku akitaja uwepo wa ongezeko la majengo ya kibiashara katika eneo hilo na kupunguza changamoto ya wananchi kuzunguka kuzifikia kata hizo huku wengine wakitumia gharama nyingi Kufika katika Ofisi za Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Bukoba
"Mradi huo umetekelezwa kwa awamu 4 na sasa tunaendelea vizuri ambapo sasa katika hatua zote za utekelezaji ni kumrahisishia mwananchi kupata huduma na katika maeneo haya tumeanza kushuhudia ujenzi wa maduka na ongezeko la wakazi wakati zamani hata barabara ilikuwa haipitiki"alisema Yohana
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Katerero Halmashari ya Bukoba Mkoani Kagera wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwajengea mradi barabara hiyo kwani kwa sasa hawana hofu na vyombo vyao vya Usafiri
Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 imeweka jiwe la Msingi katika mradi huo ambao unaendelea kutekelezwa kwa viwango huku watumishi wa jengo jipya La Halmashauri mpya Ya wilaya ya Bukoba wakishuhudia lami hadi mlangoni kwao
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa ndugu Ismail Ussi ameipongeza TARURA kwa usimamizi na utekekezaji barabara na kuwataka wananchi waendelee kutunza miundombinu ya barabara na kufanya uwekezaji kwani uwepo wa barabara unarahisisha Mawasiliano.
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2