
MIKOA NA HALMASHAURI ZAHIMIZWA KUJIPANGA KUPAMBANA NA MABADILIKO TABIANCHI
Serikali imezitaka Mikoa na Halmashauri zote nchini kujiandaa ipasavyo kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia Nchi, kwa kuhakikisha ajenda ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi inajumuishwa katika vipaumbele vya mipango ya maendeleo.
Wito huo umetolewa leo Jumanne, Septemba 23, 2025 na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Tawala za Mikoa kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhandisi Enock Nyanda, wakati wa kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Uhimili na Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabia Nchi (LoCAL), kilichofanyika jijini Dodoma.
Mhandisi Nyanda amesema sasa ni wakati wa kila mkoa na halmashauri kuandaa mipango mkakati ya maendeleo yenye kulenga mazingira na tabia Nchi kwa kipindi cha miaka 5 hadi 10, ili kupima mafanikio ya utekelezaji kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Ameeleza kuwa Serikali itaendelea kushirikisha wadau wote muhimu katika maandalizi ya mipango ya muda wa kati na mrefu ili kuhakikisha ajenda ya mazingira na mabadiliko ya tabia Nchi inatekelezwa kwa ufanisi.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa UNCDF–LoCAL nchini, Bi. Aine Mushi, ameishukuru Serikali kwa ushirikiano mkubwa unaotolewa, hususan kupitia Halmashauri zinazotekeleza mradi huo, ambao tayari umeleta manufaa kwa wananchi.
Tanzania inatekeleza Mpango wa UNCDF wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia Nchi (LoCAL), unaotumia ruzuku maalum za ustahimilivu wa tabianchi zenye masharti ya utendaji (PBCRGs), ambazo hupitishwa kupitia mifumo ya kitaifa ya uhamasishaji, ili kufanikisha utekelezaji wake katika ngazi za Serikali za mitaa.
Comments
Please sign in to leave a comment.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2