
Mhe Katimba, Mtwale, washiriki Maadhimisho ya Siku ya Watoa Huduma za Misaada ya Kibinadamu Duniani
Na OR- TAMISEMI, Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Serikali za Mitaa Sospeter Mtwale ni miongoni mwa viongozi walioshiriki leo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Watoa Huduma za Misaada ya Kibinadamu Duniani jijini Dodoma.
Katika maadhimisho hayo Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Willium Lukuvi amewasisitiza watoa huduma za kibinadamu kutia mkazo suala la kuelimisha wananchi kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu ili kupunguza athari za majanga pindi yanapotokea.
Mhe. Lukuvi ametoa msisitizo huo kwa niaba mgeni rasmi wa tukio hilo Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa
“Ninatoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali, sekta binafsi na taasisi za dini kuimairisha ushirikiano na Serikali na kujiunga katika mtandao wa kitaifa wa usimamizi wa huduma za kibinadamu, kwa kufanya hivyo kutaongeza uratibu, uwajibikaji na ufanisi katika kushughulikia majanga” ameeleza.
Mbali na hayo Mhe. Lukuvi amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mikakati na kampeni zote za uhifadhi na utunzaji wa mazingira kwani kwa kufanya hivyo kutawezesha katika kukabiliana na majanga hususani yale ya asilia.
“Suala na utunzaji wa mazingira ni muhimu sana katika kukabiliana na majanga hususan yale ya asilia, nitoe wito kwa wananchi wote kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mikakati na kampeni zote za uhifadhi na utunzaji wa mazingira. Hatua mojawapo muhimu ni kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi hivyo niwakumbushe Watanzania wote kushiriki kikamilifu katika kampeni hizo muhimu za Kitaifa” amesisitiza.
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2




