
MHANDISI MATIVILA AKAGUA MIRADI YA BARABARA MWANZA, AWATAKA WANANCHI KUITUNZA
Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila amewataka wananchi kutunza barabara kwa kuzifanyia usafi ili zidumu kwa muda mrefu.
Mhandisi Mativila ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miundombinu ya barabara zinazosimamiwa na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza.
Katika ziara hiyo ametembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya RTC-Sungura yenye urefu wa Km 0.321 pamoja na barabara ya Pump House Km 0.299 katika mji wa Nansio.
Aidha, amesema dhamira ya Serikali ni kuendelea kuimarisha mtandao wa barabara nchini kwa kujenga barabara mpya na kuzifanyia matengenezo zilizopo.
Amefafanua kuwa barabara hizo zikitunzwa vizuri zitachochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi, pamoja na kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali huku akisisitiza kuwa kuboreka kwa barabara kutaongeza ajira kutokana na kupitika katika kipindi chote cha mwaka.
Amemshukuru na kumpongeza Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya mapinduzi makubwa katika ujenzi wa barabara nyingi za kiwango cha lami kote nchini ikiwa ni pamoja na miundombinu yake.
“Nichukue fursa hii kutoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais kwa kutoa mabilioni ya fedha kwenye ujezi wa barabara na miundombinu yake, ambapo tumeshuhudia ujenzi ukiendelea kila sehemu ya nchi yetu hali ambayo itasaidia sana kukua kwa uchumi wa nchi yetu kwa kuwa kuboreka kwa barabara na miundombinu yake ni kitovu na kichocheo cha uchumi.” Amesisitiza Mhandisi Mativila.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Christopher Ngubiagai akitoa taarifa kwa Naibu Katibu Mkuu amepongeza kazi inayofanywa na Serikali huku akimpongeza Naibu Katibu Mkuu Mativila kutembelea Wilaya ya Ukerewe kwa kukagua na kujionea hali ya miundombinu ilivyoleta matumaini makubwa kwa wananchi na wadau wa vyombo vya usafirishaji.
Mradi wa barabara za RTC - Sungura na Pump House umetekelezwa na Mkandarasi Deep Construction Ltd ya Morogoro chini ya usimamizi wa TARURA wilayani Ukerewe, mradi huo umetekelezwa kwa muda wa mwaka mmoja.
Comments
Please sign in to leave a comment.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2