
“Mbadiliko ni mtu siyo cheo” - Mtanda
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Said Mtanda ametoa wito kwa Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata kutumia elimu zao kuibadilisha jamii kimtizamo na kimaendeleo akisisitiza kuwa wasingoje kuwa viongozi wakubwa ili kuleta mabadiliko chanya katika maeneo yao ya uongozi.
Mtanda ametoa rai hiyo jijini Mwanza wakati akihitimisha mafunzo ya siku mbili ya maafisa tarafa na watendaji wa Kata wapya walioajiriwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2025 kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu, Shinyanga, Tabora, Geita na Kagera.
Amesema Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata ni miongoni mwa ngazi za awali kabisa za utumishi wa umma ambazo ni msingi wa ufanisi wa shughuli za serikali kwa watu wake hivyo kuwataka walete mabaliko tarajiwa na serikali akisisitiza kuwa mabadiliko yanaletwa na mtu na siyo cheo.
“Degree mlizonazo ni uwezo wa kazi, degree siyo karatasi, degree ni uwezo wa kuonesha mtu ameiva, twende na maarifa ila degree tuziache nyumbani watumikieni wananchi ili wao wenyewe waseme huyu kweli ni kiongozi mwenye taaluma hakika alitufaa” alisema Mtanda.
Kadhalika amewahimiza maafisa hao kuzingatia taratibu za kiserikali kila wanapofanya mawasiliano akisisitiza bidii na nidhamu ya kazi kuanzia ofisini mpaka kwa jamii wanayo ihudumia.
Comments
Please sign in to leave a comment.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2