
MAKAMU WA RAIS WA ZIMBABWE AIPONGEZA TANZANIA KWA KUTOA MAFUNZO YA KUWAWEZESHA VIONGOZI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mheshimiwa Kanali Mstaafu Kembo Campbell Mohadi yuko katika ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania na katika ziara hiyo ametembelea chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha, mkoani Pwani.
Wakati wa ziara hiyo Mhe. Mohadi amekutana na wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaopatiwa mafunzo ya uongozi katika chuo hicho yanayolenga kuwajengea uwezo viongozi, ambapo amepongeza juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka programu za kuwajengea uwezo viongozi wao.
Mafunzo hayo ya Uongozi kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa yameanza tarehe 29 Agosti hadi 04 Septemba, 2025 na yanaratibiwa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi (UONGOZI INSTITUTE).
Comments
Please sign in to leave a comment.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2