
MAJUKUMU YA OR-TAMISEMI KATIKA DIRA YA TAIFA 2050
Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) inabeba jukumu muhimu katika kutekeleza Dira ya Taifa 2050 kwa kuhakikisha maendeleo jumuishi na endelevu katika ngazi za chini ya utawala. Kupitia mifumo ya Ugatuaji wa Madaraka (D by D), OR-TAMISEMI ina wajibu wa kuhakikisha kuwa maendeleo yanapangwa na kutekelezwa kwa kuzingatia mahitaji halisi ya wananchi katika Majiji, Miji, Miji midogo, Mitaa na Vijiji.
Moja ya majukumu makuu ya OR-TAMISEMI ni kusimamia utekelezaji wa maendeleo katika ngazi za mitaa kwa kuhakikisha huduma bora za kijamii kama elimu, afya, miundombinu ya vijijini na kwenye miji, Utawala Bora katika ngazi ya msingi na miundombinu mingine ya msingi inayopatikana kwa wananchi wote ambapo kupitia Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri Ofisi ya Rais TAMISEMI hufanikisha mipango jumuishi ya maendeleo inayozingatia mazingira na changamoto za kila hususani kwenye ngazi za msingi.
Katika kuhakikisha rasilimali na mipango ya maendeleo inasimamiwa kwa ufanisi, OR-TAMISEMI ina jukumu la kuimarisha uwezo wa taasisi za mitaa katika kupanga, kutekeleza na kufuatilia miradi. Hili linahusisha uimarishaji wa mifumo ya ukusanyaji wa mapato ya ndani, matumizi sahihi ya fedha za umma, na kuhimiza uwajibikaji katika ngazi zote za serikali za mitaa.
Vilevile, Ofisi ya Rais TAMISEMI itawajibika kukuza utawala bora kwa kushirikisha wananchi katika kupanga na kufanya maamuzi ya maendeleo ya maeneo yao utakaochangia kujenga msingi wa haki, usawa na uwajibikaji katika Serikali za Mitaa kwa lengo la kuongeza imani kwa wananchi na kwa Taasisi za Umma.
Majukumu mengine ni pamoja na uendelezaji wa miji midogo na vijiji kwa kuweka mazingira rafiki ya kiuchumi na kijamii, pamoja na kuunganisha mipango ya Mikoa na Halmashauri na vipaumbele vya Kitaifa na Kimataifa.
Kwa ujumla, Ofisi ya Rais TAMISEMI ni muhimili wa msingi katika kutekeleza Dira ya Taifa 2050 ikiwa na dhamira ya kuhakikisha kuwa maendeleo yanawafikia wananchi wote.
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2