
MAAFISA BAJETI WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI NA WELEDI KATIKA KAZI
Na. Angela Msimbira,OR-TAMISEMI
Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Bi. Angelista Kihaga, amewataka Maafisa Bajeti wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili, uadilifu na weledi ili kuhakikisha mipango ya maendeleo inatekelezwa ipasavyo.
Akizungumza leo Septemba 9,2025 kwenye mafunzo ya uandaaji wa mipango na bajeti kwa Maafisa Bajeti wa Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri yanayoendelea katika Chuo cha Mipango Jijini Dodoma, Bi. Kihaga alisema wajibu wa maafisa hao ni kuhakikisha rasilimali za umma zinapangwa na kutumika kwa tija, kwa manufaa ya wananchi.
“Ni wajibu wenu kuhakikisha mnazingatia maadili ya kazi na kufanya kila jambo kwa weledi. Taifa linawategemea katika kuhakikisha bajeti mnazoandaa zinagusa mahitaji ya wananchi na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi,” amesema Bi. Kihaga.
Aidha, amesisitiza kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuongeza ufanisi katika uandaaji na utekelezaji wa bajeti, huku akiwataka washiriki kutumia fursa hiyo kujifunza kwa bidii na kubadilishana uzoefu.
Mafunzo hayo yamehudhuriwa na maafisa bajeti zaidi ya 100 kutoka mikoa mbalimbali nchini. Hili ni kundi la tatu kushiriki mafunzo hayo, ambapo kesho inatarajiwa kuanza kundi la nne.
Comments
Please sign in to leave a comment.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2