
Katibu Tawala Mkoa Kilimanjaro ahimiza ubunifu katika kutatua kero za wananchi.
Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Kiseo Yusuph Nzowa ametoa wito kwa watumishi wa Umma kuwa wabunifu katika utatuzi wa kero za wananchi kwa kutafuta majawabu ya kero husika ili kuendelea kujenga imani ya jamii juu ya viongozi wao.
Katibu Tawala Nzowa ametoa agizo hilo leo (Julai 24, 2025) wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata wapya walioajiriwa kuanzia mwezi Julai, 2024/2025
“Sisi wote ni watendaji wa serikali lazima pale ulipo wewe uwe wa kwanza kutafuta jawabu la kero yoyote inayoibuka katika eneo lako ili ujenge imani kwa unaowaongoza na uwe msaada kwa viongozi wa juu katika kutafuta suluhu ya changamoto zinazoibuka katika eneo lako” Alisema Nzozwa
Katibu Tawala Nzowa amesisitiza utatuzi wa kero kwa kuzingatia muda tangu tatizo lilipotoke huku akisema ni vyema watendaji wa Serikali kutatua kero kwa wakati wakitumia ubunifu, weledi na ufahamu wanaojengewa mara kwa mara ili kutimiza malengo tarajiwa.
Mafunzo hayo kwa Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata katika kanda ya kasikazini yanawashirikisha washiriki kutoka Mikoa ya Arusha, Manyara, Tanga, Kilimanjaro na Manyara.
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2