
BENDERA YA TANZANIA YAPEPEA JUU KATIKA MASHINDANO YA FEASSA
OR-TAMISEMI, Kenya
Timu ya Tanzania imeendelea kuonyesha ushindani kwenye ya michezo ya shule za Msingi na Sekondari ya nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki (FEASSA) yanayoendelea mjini Kakamega, Kenya.
Katika mchezo wa Netiboli Tanzania iliibuka na ushindi wa magoli 39–25 dhidi ya Rwanda, matokeo yanayoongeza matumaini ya kufanya vyema katika hatua za makundi.
Kwa upande wa Soka Tanzania ilionyesha umahiri mkubwa ilipocheza na Kenya na kukubali kipigo cha goli 1–0 kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Bukhungu, mbele ya umati mkubwa wa mashabiki.
Vilevile kwa upande wa mpura wa Wavu wasichana Tanzania ilionyedha kiwango bora na kuibuka na ushindi wa seti 3–0 dhidi Uganda, wakidhihirisha uwezo na ubora wao kwenye mchezo huo.
Ushiriki wa Tanzania katika michezo mbalimbali ya FEASSA unaendelea kuimarisha na kukuza vipaji na kudumisha mshikamano wa kijamii kupitia michezo miongoni mwa vijana wa Afrika Mashariki
Comments
Please sign in to leave a comment.
Matangazo Muhimu
Soma matangazo na taarifa rasmi ili kuendelea kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Wizara.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WALIMU WA KUJITOLEA 128 SHULE ZA MSINGI 128 KWA AWAMU YA PILI GPE TSP
ORODHA YA WALIMU WA KUJITOLEA 128 GPE TSP AWAMU YA PILI
ADDITIONAL BEST INDICATORS 2025
BASIC EDUCATION STATISTICS 2025
Generic ESMP for CERC Interventions under DMDP2